Showing posts with label android. Show all posts
Showing posts with label android. Show all posts

Jul 17, 2015

Jinsi ya kupata "Developer options" katika smartphone ya Android.

Kuna wakati ambao unahitaji kuweka upya operating system(stock firmware) ya smartphone yako, pengine unahitaji kuweka custom rom(custom firmware) au kuroot smartphone hiyo na mengine mengi ambayo yatahusisha kubadili mfumo wa operating system ya smartphone yako kwa namna moja au nyingine. Katika kufanikisha michakato niliyotaja hapo awali kuna mlolongo wa hatua ambazo utatakiwa kupitia, moja ya suala la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba "USB debugging mode" imewashwa(activated), na hili chaguo lipo ndani ya developer options.

USB debugging mode ipo mahususi kwa ajili ya kazi za uendelezaji wa programu(software development), hufanikisha uhamishaji wa programu/data kutoka vyanzo visivyo rasmi(unknown sources), husaidia watengeneza programu kufanya majaribio(app testing) ya software wanazotengeneza katika smartphone zao na mambo mbalimbali ukijumuisha na niliyotaja hapo mwanzo wa makala hii. 

Baadhi ya smartphone huja na chaguo la developer options likionekana wazi ndani ya mipangilio(settings), kwa bahati mbaya smartphone nyinginezo chaguo hili huwa halionekani na utahitaji kufata hatua rahisi tu ili kuweza kupata developer options. Makala hii itakuelekeza namna ya kupata developer options endapo smartphone yako ni mojawapo ya zile zisizoonyesha developer options.

Jul 8, 2015

Mahangaiko ya HTC ili kuwa na smartphones zenye kamera bora.

Miaka ya nyuma, Samsung amelalamikiwa sana kuhusu matumizi ya plastiki na ubunifu (design) hafifu wa smartphone zake. Yote yamepita na sasa imebaki historia, Kiswahili kizuri tunasema "ya kale". Ninasema " ya kale" kwa sababu sasa hivi Wakorea Kusini hawa wametambua ubunifu bora na unaokwenda na wakati, hili linajidhihirisha katika flagship smartphones zao za sasa, Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge ambazo muundo wake wa nje umetengenezwa kwa kutumia metali ya Aluminum na Kioo kigumu (tempered glass) kinachozuia michubuko(scratch resistant) kinachofahamika kama Gorilla Glass 4. High-Tech Computer Corporation, wanafahamika maarufu zaidi kama HTC wanajua ubunifu bora wa smartphones, sio siri! Na hata wakati Samsung analalamikiwa kwa kutumia plastiki katika Samsung Galaxy S4 mnamo mwaka 2013, HTC alifahamu vizuri zaidi jinsi ya kutumia Aluminum na sio plastiki katika kutengeneza umbo la nje la HTC One M7, iliyokuwa mpinzani (rival) wa Galaxy S4.

Japokuwa HTC anafahamu vizuri ubunifu wa simu na ndiye wa kwanza kutumia metali kwa kiasi kikubwa katika uundaji wa smartphone zake, suala la kushindwa kuwa na kamera nzuri katika smartphone hizo linamnyima usingizi kabisa. Si kwamba kamera ya HTC One M8 (flagship yao ya 2014) ni mbaya, lakini ina ubora gani ukiifananisha na kamera ya smartphone kama LG G3 au Sony Xperia Z3 kwa mfano, ambao wote hawa ni wapinzani wake (rival smartphones).

Jun 26, 2015

BlackBerry inayotumia Android OS! wazo zuri?

Ni takribani wiki mbili sasa zimekuwepo tetesi nyingi mtandaoni zihusuzo kampuni ya BlackBerry kuwa na mipango ya kutengeneza smartphone ambayo itatumia operating system(OS) inayomilikiwa na Google, Android OS. Wakanada hawa kwa sasa wapo katika mahangaiko ya kurudisha soko la smartphones zao ambalo lilipokonywa na kampuni kama Apple na Samsung miaka takribani sita iliyopita. Tangu kuwepo kwa uongozi wa Bwana John Chen ambaye ni mkurugenzi(CEO) wa kampuni hii kwa sasa, BlackBerry imekuwa ikiona mafanikio japokuwa ni taratibu katika nyanja mbalimbali za biashara zao.

John Chen

Feb 26, 2015

Apps tatu muhimu za Android kwa ajili ya kusomea vitabu.

Smartphones zimebadili sana mifumo ya maisha yetu. Tofauti na simu za kawaida (features phones) ambazo kazi yake kubwa ni kupiga, kupokea simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms). Smartphones zina mambo mengi sana unayoweza kufanya ndani yake. Katika nyakati hizi za utandawazi pamoja na mabadiliko ya kidigitali, si lazima tena kununua vitabu vikiwa katika mfumo wa karatasi (hard copy). Unaweza nunua vitabu vikiwa katika mfumo wa digitali (digital edition/soft copy) na kusoma popote pale uendapo katika smartphone/tablet yako. Lakini, kuweza kufanikisha suala hili ni lazima uwe na application ambayo itasoma aina hii ya vitabu katika kifaa (device) chako. Vitabu, majarida na nyaraka nyingine huwa katika mifumo ya pdf, epub au mobi. Tuangalie apps tatu rahisi na muhimu kutumia katika kuwezesha suala hili.

Jan 30, 2015

Mtiririko mzima wa version za Android OS.

Android OS ni operating system ya simu inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi sana duniani kote, ikitumika katika zaidi ya asilimia 80% ya smartphone zote zilizopo ulimwenguni. Moja ya vitu vinavyoifanya OS hii kupata umaarufu ni kutokana na kwamba ni mradi wa chanzo cha wazi na huru(Open Source Project), ina maana kwamba, mtengeneza smartphone yoyote atayependelea kutumia OS hii ana ruhusa kuitumia lakini kwa kuzingatia masharti ambayo yamewekwa na Google ambaye ndiye mmiliki ili kuruhusu smartphone husika kupata huduma za Google(Google Services). Ndiyo maana unaona Samsung, HTC, Sony, Xiaomi n.k wote wanatumia OS hii. Tofauti na OS nyingine kama iOS na BlackBerry OS ambazo hizi chanzo chake hakipo wazi(Closed Source), na ni mmiliki ndiye mwenye ruhusa ya kuitengeneza, kuiboresha na kutumia katika smartphone zake mwenyewe tu(Proprietary ownership).