Jul 8, 2015

Mahangaiko ya HTC ili kuwa na smartphones zenye kamera bora.

Miaka ya nyuma, Samsung amelalamikiwa sana kuhusu matumizi ya plastiki na ubunifu (design) hafifu wa smartphone zake. Yote yamepita na sasa imebaki historia, Kiswahili kizuri tunasema "ya kale". Ninasema " ya kale" kwa sababu sasa hivi Wakorea Kusini hawa wametambua ubunifu bora na unaokwenda na wakati, hili linajidhihirisha katika flagship smartphones zao za sasa, Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge ambazo muundo wake wa nje umetengenezwa kwa kutumia metali ya Aluminum na Kioo kigumu (tempered glass) kinachozuia michubuko(scratch resistant) kinachofahamika kama Gorilla Glass 4. High-Tech Computer Corporation, wanafahamika maarufu zaidi kama HTC wanajua ubunifu bora wa smartphones, sio siri! Na hata wakati Samsung analalamikiwa kwa kutumia plastiki katika Samsung Galaxy S4 mnamo mwaka 2013, HTC alifahamu vizuri zaidi jinsi ya kutumia Aluminum na sio plastiki katika kutengeneza umbo la nje la HTC One M7, iliyokuwa mpinzani (rival) wa Galaxy S4.

Japokuwa HTC anafahamu vizuri ubunifu wa simu na ndiye wa kwanza kutumia metali kwa kiasi kikubwa katika uundaji wa smartphone zake, suala la kushindwa kuwa na kamera nzuri katika smartphone hizo linamnyima usingizi kabisa. Si kwamba kamera ya HTC One M8 (flagship yao ya 2014) ni mbaya, lakini ina ubora gani ukiifananisha na kamera ya smartphone kama LG G3 au Sony Xperia Z3 kwa mfano, ambao wote hawa ni wapinzani wake (rival smartphones).


Turudi nyuma kidogo, mnamo mwaka 2013. HTC One M7 ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Machi mwaka huo. Smartphone hii ilitumia teknolojia inayofahamika kama Ultrapixel katika kamera yake ya nyuma (primary camera), teknolojia hii ni ya HTC (proprietary) na ndiyo ilikuwa inatumika kwa mara ya kwanza kabisa (first ever before....). Kamera ya Ultrapixel ina ubora wa resolution ya 4 megapixels, ambapo kwa muda huo smartphone nyinginezo za hali ya juu zilikuwa zikitumia kamera zenye 8 au 13 megapixels. Teknolojia hii inawezesha kupiga picha zilizo na pixels (viunda picha) zilizo na ukubwa(size) ya 4 micrometer za mraba (micrometer square), smartphones nyinginezo huwa na size ya pixel kati ya 1 hadi 1.96 micrometer za mraba kwa kila pixel iliyopo katika picha. Wataalamu na wachambuzi wa teknolojia ya smartphones na kamera walihoji kuhusiana na teknolojia ya Ultrapixel. Katika hali ya kawaida, unapoongeza size ya pixel unasababisha kamera kutoa picha zilizo na ubora wa hali ya chini hasa katika sehemu yenye mwanga hafifu, si hivyo tu! Inaweza pelekea pia kamera kukosa umakini (sensitivity) katika uchukuaji wa picha.

Kwa kamera zenye resolution ya 13 megapixels na kuendelea, size ya pixel huzidi kupungua ili kufanya picha kuwa maaridadi (sharp and detailed) zaidi.

Kwa upande wa HTC walidai ya kwamba, kutumia pixel ya size kubwa kutaongeza ubora wa picha na umakini tena hasa nyakati za usiku, lakini haya yote hayakuwa ukweli kwa asilimia kubwa mpaka leo hii. HTC One M8 (toleo la mwaka 2014) ilitumia teknolojia ya Ultrapixel pia, lakini teknolojia hii haijavutia sana watumiaji wa smartphones ambao ubora wa kamera ni kipaumbele kikubwa sana kwao, wengi waliona ni bora kununua smartphones nyinginezo kama Samsung Galaxy S5 au LG G3.
Kwa mwaka huu HTC ameendelea na toleo lingine la HTC One, ikifahamika kama "HTC One M9". Kilicho tofauti na matoleo yaliyopita nyuma ni kwamba M9 haijatumia Ultrapixel katika kamera ya nyuma (primary camera), kamera ya nyuma ni ya kawaida yenye 20 megapixels na ya mbele (secondary camera) ndiyo imetumia Ultrapixel camera yenye 4 megapixels.

HTC One M9

Pamoja na mabadiliko haya, kamera ya HTC One M9 imelalamikiwa na baadhi ya watumiaji wa smartphone hii. Kamera inaonekana kuwa na tatizo la kushindwa kutoa rangi sahihi na za ukweli ( poor color accuracy), HTC ameshatoa software update ili kurekebisha suala hili. Software update inaweza kuondoa tatizo hili iwapo tu linasababishwa na tatizo la software ya kamera, kama tatizo linasababishwa na hardware, hakuna jinsi nyingine ya kuondoa tatizo hili.

Bado HTC hajaweza fikia mahala ambapo hata yeye mwenyewe anaweza kusema ameridhishwa na ubora wa kamera zake. Kwa sasa yupo katika mchakato wa kutengeneza smartphone nyingine ambayo itakuwa ni flagship yake mpya na itafahamika kwa jina la "Aero".  Kwa mujibu wa HTC, smartphone hii italeta mabadiliko makubwa sana na nyakati mpya kwao kwa upande wa kamera ambapo haijawahi kutokea kabla katika historia yao. 

No comments :

Post a Comment