Jul 17, 2015

Jinsi ya kupata "Developer options" katika smartphone ya Android.

Kuna wakati ambao unahitaji kuweka upya operating system(stock firmware) ya smartphone yako, pengine unahitaji kuweka custom rom(custom firmware) au kuroot smartphone hiyo na mengine mengi ambayo yatahusisha kubadili mfumo wa operating system ya smartphone yako kwa namna moja au nyingine. Katika kufanikisha michakato niliyotaja hapo awali kuna mlolongo wa hatua ambazo utatakiwa kupitia, moja ya suala la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba "USB debugging mode" imewashwa(activated), na hili chaguo lipo ndani ya developer options.

USB debugging mode ipo mahususi kwa ajili ya kazi za uendelezaji wa programu(software development), hufanikisha uhamishaji wa programu/data kutoka vyanzo visivyo rasmi(unknown sources), husaidia watengeneza programu kufanya majaribio(app testing) ya software wanazotengeneza katika smartphone zao na mambo mbalimbali ukijumuisha na niliyotaja hapo mwanzo wa makala hii. 

Baadhi ya smartphone huja na chaguo la developer options likionekana wazi ndani ya mipangilio(settings), kwa bahati mbaya smartphone nyinginezo chaguo hili huwa halionekani na utahitaji kufata hatua rahisi tu ili kuweza kupata developer options. Makala hii itakuelekeza namna ya kupata developer options endapo smartphone yako ni mojawapo ya zile zisizoonyesha developer options.

1. Ingia katika mipangilio(settings).


2. Bonyeza chaguo la About phone/About.



3. Bonyeza chaguo la "Build number" mara saba mfululizo.



Hakikisha unabonyeza sehemu hii mara saba mfululizo, utapobonyeza mara ya tatu 
itakuambia "You are 4 steps away to become a developer". Endelea kubonyeza mpaka mara ya saba ambapo itaandika "You are now a developer". Utaporudi katika settings utakuta developer options inaonekana, na sasa utaweza kutumia developer options na kuweza kuwasha(activate) USB debugging mode na kupata machaguo mengine mengi. 


TAHADHARI(CAUTION)!

Developer options ina machaguo(options) mengi ndani yake na USB debugging mode ni mojawapo. Hakikisha unawasha(activate) chaguo pale tu unapofahamu kwa usahihi matumizi/chaguo ya chaguo hilo. Kufanya mabadiliko(modifications) yoyote katika kipengele cha developer options ambayo huyafahamu malengo yake kunaweza pelekea simu yako kutofanya kazi namna inavyotakiwa(misbehave). 

No comments :

Post a Comment