Feb 26, 2015

Apps tatu muhimu za Android kwa ajili ya kusomea vitabu.

Smartphones zimebadili sana mifumo ya maisha yetu. Tofauti na simu za kawaida (features phones) ambazo kazi yake kubwa ni kupiga, kupokea simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms). Smartphones zina mambo mengi sana unayoweza kufanya ndani yake. Katika nyakati hizi za utandawazi pamoja na mabadiliko ya kidigitali, si lazima tena kununua vitabu vikiwa katika mfumo wa karatasi (hard copy). Unaweza nunua vitabu vikiwa katika mfumo wa digitali (digital edition/soft copy) na kusoma popote pale uendapo katika smartphone/tablet yako. Lakini, kuweza kufanikisha suala hili ni lazima uwe na application ambayo itasoma aina hii ya vitabu katika kifaa (device) chako. Vitabu, majarida na nyaraka nyingine huwa katika mifumo ya pdf, epub au mobi. Tuangalie apps tatu rahisi na muhimu kutumia katika kuwezesha suala hili.

Mantano Reader Premium.

App hii inapatikana katika PlayStore kama ya bure ikiwa na features chache za msingi(lite) na pia kama utahitaji kutumia features zote (premium version) itabidi kulipia dola $5.87 za Kimarekani
(sawa na takribani Tsh. 10,000). Uzuri wa apps za Android zinazohitaji malipo katika ununuzi wake huweza patikana bure kabisa kwa njia ambayo wengi tunaifahamu kama pirating, apps hizi huwa zipo cracked, hii ina maana ya kwamba features zote ambazo zinafunguka kwa kuhitaji malipo utazikuta zikiwa tayari zimefunguliwa na tayari kutumika bila kikwazo chochote.

Si vitabu tu, unaweza soma hata majarida yaliyo katika pdf na epub.


App hii ina features nyingi sana. Kuanzia muonekano wake mpaka vitu ilivyosheheni. Inaweza kusoma mafaili yaliyo katika mfumo wa pdf, epub, epub2 na epub3. Hii inakuwezesha kusoma aina mbalimbali ya mafile ukitumia app moja tu.

Inakuwezesha kuchagua ukubwa wa kava za vitabu katika kabati(bookshelf).


  • Ina uwezo wa kuchagua ukubwa kava la nje la kitabu (thumbnail) pale lionekanapo katika kabati (shelf) la vitabu vyako, ina features nyingi katika kuwezesha kupangilia maktaba yako.
  • Inakuwezesha kuchagua rangi ya nyuma (background color) unaposoma kitabu. Unaweza chagua themes ambazo zinakuja na app (pre-installed) au kutengeneza ya kwako kulingana na vile unavyopendelea.

Unaweza chagua rangi ya nyuma(background colour) unayopendelea.

  • Unaweza badili ukubwa wa maandishi (fonts) na aina ya maandishi unayohitaji kwa vitabu vilivyopo katika mfumo wa epub, epub2 na epub3.
  • Inakuwezesha kusoma kwa kutumia night mode ambayo huleta muonekano wa nyuma (background color) ambao una rangi nyeusi ili kuepusha kuumia macho hasa unaposoma kitabu nyakati za giza. 
  • Inakuwezesha kufanya highlight.
  • Unaweza kuachagua namna mbalimbali za jinsi kurasa za kitabu zinavyofunguka. 
  • Ni rahisi sana kuingiza vitabu kutoka katika kumbukumbu ya simu yako (phone storage) na kuanza kusoma katika Mantano Reader. Pia unaweza pata vitabu kutoka katika online store iliyopo katika app hiyo.
    Download Mantano Reader Premium iliyo na features zote bila kulipia gharama yoyote:Download 1 au Download 2.



    Universal Book Reader(UB Reader).

    App hii inapatikana katika Playstore kama app ya bure. Lakini huonyesha matangazo(advertisements/ads), hutaweza kufungia(lock) vitabu ambavyo pengine usingetaka mtu yoyote kuvisoma zaidi ya wewe mwenyewe na pia hakuna uwezo wa kusikiliza kitabu bila ya kusoma(text-to-speech). Vipengele vyote hivi vitaanza fanya kazi pale utapolipia dola $4.99(sawa na takribani Tsh. 8,500). Inasupport vitabu vilivyopo katika mifumo (extensions) ya pdf, epub, epub2 na epub3 lakini haina features nyingi kama ilivyo kwa Mantano Reader. Ni rahisi zaidi kuitumia na haihitaji muda mrefu kuweza kuizoea.

    Unaweza highlight aya au mstari ili kuuweka katika kumbukumbu.


    • Inakuwezesha kuchagua maandishi (fonts) unayohitaji na kuweza badili ukubwa wa maandishi hayo katika vitabu vyote vilivyopo katika mfumo wa epub.
    • Pamoja haina uwezo wa kubadili ukubwa wa makava (thumbanail) katika maktaba yako, lakini unaweza chagua muonekano (view) unaohitaji aitha grid au list.
    • Inakupa urahisi wa kuingiza vitabu vyako kutoka katika kumbukumbu ya simu (phone storage) na kuingia katika maktaba kwa kubonyeza tu "import books". Haijalishi kitabu kitakuwa katika kabrasha (folder) lipi, UB Reader itatambua kitabu hicho na kukiweka katika maktaba.
    • Inakuwezesha kuchagua muonekano wa nyuma (background color) unaposoma kitabu, hauwezi kutengeneza background color ya kwako kama ilivyo katika Mantano Reader. 
    • Inakuwezesha kuchagua jinsi vitabu vyako vinavyofunguka. 
    • Inakuwezesha kuhighlight na pia kuweka kumbukumbu pale ulipoishia kusoma kitabu husika.
    • Ina stoo ya vitabu inayokuwezesha kupata vitabu kutoka katika mtandao.

    Download UB Reader Premium isiyo na ads na yenye vipengele vyote: Download .


    Adobe Reader.

    App hii inapatikana bure kabisa katika Playstore na hauhitaji kulipia kiasi chochote ili kuweza kutumia vipengele (features) vyake vyote. Ni tofauti na apps nilizoelezea hapo juu, hii inaweza kusoma vitabu vilivyo katika mfumo wa pdf tu, hutaweza soma vitabu vya epub au mfumo mwingine katika app hii. Ina features chache sana ukilinganisha na apps nyingine. Features zilizopo ni kwa ajili ya kukuwezesha tu kusoma file za pdf kwa urahisi.

    Utaweza kusoma file za pdf tu katika Adobe.


    • Inakuwezesha kuweka kumbukumbu pale ulipoishia kusoma.
    • Inakuwezesha kufanya highlight ya mistari muhimu utayohitaji kukumbuka.
    • Inakuwezesha kushare kitabu husika unaposoma kwa mtu mwingine kupitia Bluetooth au Gmail.
    • Ina uwezo wa kukuonyesha vitabu vyote ulivyosoma muda mfupi uliopita(recent read document). 
    Download Adobe Reader kutoka Playstore: Download.

    Namna ya kuinstall Mantano Reader Premium na UB Reader Premium.

    Kwa vile app hizi hutadownload kutoka Playstore, itakubidi kufanya installation mwenyewe(manually) au sideloading kama inavyofahamika. Fuata hatua hizi ili kukamilisha.

      1. Download file kutoka katika link nilizoweka hapo juu.
      2. Baada ya hatua ya kwanza kukamilika, ingia katika menu ya simu halafu settings halafu security halafu unknown sources. Hakikisha katika unknown sources pana tick(checked) au pako on.
      3. Rudi nyuma na tafuta file lako la app ulilodownload.
      4. Bonyeza hilo file na kisha "install".
      5. Baada ya installation app yako ipo tayari kwa kutumika.











No comments :

Post a Comment