Jan 30, 2015

Mtiririko mzima wa version za Android OS.

Android OS ni operating system ya simu inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi sana duniani kote, ikitumika katika zaidi ya asilimia 80% ya smartphone zote zilizopo ulimwenguni. Moja ya vitu vinavyoifanya OS hii kupata umaarufu ni kutokana na kwamba ni mradi wa chanzo cha wazi na huru(Open Source Project), ina maana kwamba, mtengeneza smartphone yoyote atayependelea kutumia OS hii ana ruhusa kuitumia lakini kwa kuzingatia masharti ambayo yamewekwa na Google ambaye ndiye mmiliki ili kuruhusu smartphone husika kupata huduma za Google(Google Services). Ndiyo maana unaona Samsung, HTC, Sony, Xiaomi n.k wote wanatumia OS hii. Tofauti na OS nyingine kama iOS na BlackBerry OS ambazo hizi chanzo chake hakipo wazi(Closed Source), na ni mmiliki ndiye mwenye ruhusa ya kuitengeneza, kuiboresha na kutumia katika smartphone zake mwenyewe tu(Proprietary ownership).

Tangu kuanza kutumika rasmi kabisa katika smartphones, mnamo mwaka 2008. Kumekuwa na versions mbalimbali za Operating System hii. Versions nyingi za Android OS hufahamika kwa majina ya vyakula vilivyo na wingi wa sukari(confectioneries). Kila version hutoka ili kuleta maboresho ya version ya nyuma. Tuangalie mtiririko mzima nikielezea kwa ufupi, tunaanza na ile ya mwanzo kabisa na mpaka iliyopo sasa.


1. Android 1.0 : Version hii ilikuja na smartphone ya kwanza itumiayo Android OS. Smartphone hii ilikuwa ikifahamika kama HTC Dream, iliyozinduliwa mwaka 2008.
Homescreen ya Android 1.0. 




2. Android 1.1 : Update hii ilitoka miezi minne baada ya uzinduzi rasmi wa HTC Dream, ilileta mabadiliko makubwa sana na kuifanya OS hii kuwa na spidi zaidi ukilinganisha na version ya nyuma.

3. Android 1.5 Cupcake : Update hii ndiyo ya kwanza kutumia jina la confectionery food, ilileta features mpya. Hakukuwa na haja ya physical keyboard ukilinganisha na versions za nyuma, ilileta keyboard iliyo katika touchscreen( virtual keyboard). Icon nyingi zilibadilika muonekano wake pia.

4. Android 1.6 Donut : Version hii ilileta features kama "text-speech-engine", inayokuwezesha kusikiliza ujumbe mfupi wa maneno uliotumiwa bila kuusoma, features nyingine zilizoboreshwa zilikuwa katika Market, ambayo kwa leo tunaifahamu kama Google Play Store.

5. Android 2.0 na 2.1 Eclair : Version hii ilileta maboresho katika upande app ya kutuma sms, kuboresha muonekano mzima wa User Inteface(UI) na pia kuweka feature ya GPS(Global Positioning System) katika Google Maps na kukuwezesha kukupa hata uelekeo wa mahali uendapo. Android 2.1 ilitoka na smartphone ya Nexus One, device ya kwanza kutolewa chini ya mradi wa Google ufahamikao kama Nexus.

6. Android 2.2 Froyo(Frozen Yoghurt) : Hii ndiyo version ya kizamani ambayo angalau unaweza kukuta mpaka leo kuna baadhi ya watu wanaendelea kuitumia, apps nyingi za Android zinasupport kuanzia version hii na kuendelea juu, lakini ina muda mchache tu kutokuwa na matumizi tena(obsolete). Version hii ilileta maboresho makubwa katika kuongeza speed ya kuperuzi katika mtandao, maboresho makubwa katika ufanyaji kazi wa simu(overall perfomance) na uwezo wa kuhamisha apps kutoka katika storage ya simu kwenda katika storage ya micro SD card(memory card).

7. Android 2.3 Gingerbread : Version hii ilibadili kabisa muonekano wa Android OS(UI). Kila kitu kilibadilika na kufanya OS hii kuonekana iliyokomaa zaidi, ilileta support ya smartphone zenye kamera ya mbele(front facing camera). Ilizinduliwa na smartphone ya Samsung Galaxy S.

Baadhi ya screenshots za Gingerbread.
8. Android 3.0 Honeycomb : Version hii ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya tablets. Hakukuwa na smartphone yoyote iliyotumia OS version hii, bali tablets tu. Smartphones zenye Android 2.3 Gingerbread zilizo na uwezo wa kupata update ziliruka mpaka Android 4.0 Ice Cream Sandwich bila kupitia Honeycomb. Version hii ilitumika mahususi katika tablets, lengo la Google likiwa kujibu mapigo kutokana na Apple kuzindua tablet ya iPad.

9. Android 4.0 Ice Cream Sandwich : Ilitoka kwa mara ya kwanza katika smartphone ya Samsung Galaxy Nexus, smartphone hii ndiyo ya kwanza kwa Android kuwa na display iliyo na uwezo wa kuonyesha katika ubora wa High Definition(HD), katika 720pixels. Ilikuwa na ukubwa kioo chenye nchi 4.65, sio kawaida kwa kipindi hicho. Watu wengi waliiponda kwamba ni smartphone kubwa sana, cha ajabu siku hizi smartphone yenye display ya ukubwa wa nchi 5 ni suala la kawaida tu.

10. Android 4.1 JellyBean : Version hii ilileta umaridadi na ufanisi mkubwa wa Android UI. Animations zikiwa murua kabisa ukilinganisha na OS versions zilizopita, boresho hili lilifahamika kama "Project Butter". Version hii ilikuwa na muendelezo, ikiwa katika subversions za 4.2 na 4.3 Jellybean.

11. Android 4.4 KitKat : Version hii ilitoka ikiahidi kusupport hadi simu zenye kiwango cha chini kabisa( low end smartphones) zenye hadi RAM ya kiasi cha 512MB. Version hii ndiyo iliyoleta support ya Android Wearables mfano smartwatches, fitness tracking devices n.k.


Homescreen ya Android Lollipop.
12. Android 5.0 Lollipop : Ikiwa ni latest version ya Android kwa sasa, Lollipop imeleta mabadiliko makubwa sana katika devices. Nyingi ya high end devices zinaendelea kupata update hii. Ina mabadiliko makubwa katika muonekano wake(UI) na pia inakuongezea uwezo wa battery hadi dakika 90. Katika version hii Google amebadili runtime environment yake, kwa sasa anatumia ART(Android Runtime) ambapo zamani alikuwa akitumia Dalvik Runtime kwa version zote zilizopita. Mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuboresha ubora wa ufanyaji kazi wa apps na kuongeza muda wa smartphone kukaa na chaji.






No comments :

Post a Comment