Dec 31, 2014

Yaliyojiri Mwaka 2014 Katika Teknolojia Ya Smartdevices (1/2)

Mwaka 2014 umefika ukingoni. Ni mambo mengi sana yamefanyika katika huu mwaka. Katika upande wa teknolojia, tumeona hatua na maendeleo makubwa sana katika nyanja hii, ikumbukwe pia huu ndio mwaka ambao Internet imetimiza miaka 20. Tutaangazia mambo yaliyokuwa gumzo katika mwaka 2014 hasa katika teknolojia ya smartphones, tukigusa katika sehemu mbalimbali kukuwezesha wewe msomaji kutambua ni yapi hasa yaliyojiri na kuleta msisimko.


Uzinduzi wa HTC M8
Mnamo mwezi March mwaka huu HTC alizindua flagship smartphone hii, ikiwa ni muendelezo wa mfululizo wa HTC One smartphones, ambapo ndio smartphone iliyopewa jina rasmi la HTC One. Toleo la nyuma(predecessor) wake ni HTC M7. Asilimia kubwa ya umbo lake la nje limetengenezwa kwa madini ya Aluminium. Ina maboresho na mabadiliko baadhi ukilinganisha na M7. M8 imetokea kupendwa na watumiaji wengi sana wa smartphones ikiwa na display ambayo ina muonekano murua kabisa ikitumia teknolojia ya Super LCD3 capacitive display katika kiwango cha pixel density ya
441ppi(pixels per inch), ukubwa wa display hii ni inchi 5. Kilicho cha kuvutia katika smartphone hii ni uwezo wake wa kutunza chaji kwa muda mrefu, ni aina ya smartphone inayokufanya kutohisi wasiwasi pale unapoamka asubuhi na kwenda katika shughuli zako za kila siku, itakuwa na wewe mpaka muda wa jioni na kuhakikisha
kwamba unakamilisha kile ulichopanga kufanya kwa siku hiyo, ina betri yenye uwezo wa 2600mAh.
HTC One M8
Kwa upande wa kamera HTC ametumia teknolojia ileile iliyotumika katika HTC M7, teknolojia hii inaitwa "Ultra Pixel", inahusisha kutengeneza kamera yenye sensor inayoundwa na pixels zenye size ya 2micrometre(micron), tofauti na smartphones nyinginezo nyingi kama Samsung Galaxy S5, Sony Xperia Z3, LG G3 ambazo sensors zake za kamera zinaundwa kwa kutumia pixels zenye size ya 1 hadi 1.4 micrometre(micron). Teknolojia hii imelalamikiwa na watu wengi katika ubora wa picha inazotoa, hasa nyakati za usiku. HTC mwenyewe, alidai ya kwamba teknolojia hii inaongeza ubora zaidi wa picha, ina kamera mbili za nyuma "duo camera" zinazokuwezesha kutengeneza picha katika mtindo wa 3D. Inatumia Operating System ya Android KitKat 4.4.4, lakini pia kuna version yake ya Windows Phone 8, sitaongelea version hii. Hapo mwakani mapema itaweza kupata update ya Android Lollipop 5.0.1. Pamoja na kwamba smartphone hii ina baadhi ya changamoto mfano katika upande wa kamera hasa kutokana na kukosa OIS(Optical Image Stabilisation), lakini unapoiangalia kiujumla utatambua ya kwamba ni moja ya smartphones bora kabisa ambazo HTC ameshawahi kutengeneza, ni sahihi pia kusema ni moja ya smartphones bora kabisa kwa mwaka 2014.


Nokia kununuliwa na Microsoft

Miongoni mwa makampuni yaliyo katika wakati mgumu katika soko la smartphones ni Nokia. Akiwa anashuka siku hadi siku na kukumbwa na majanga mengi katika soko lake, si jambo la kushangaza kusikia sasa yupo chini ya Microsoft, baada ya kuhangaika kwa muda katika kutafuta njia mbadala ya kurudi sokoni.  Mnamo mwezi Septemba Microsoft ilitangaza kuinunua Nokia kwa US$ 7.2 billion (trillioni 12.54 Tshs.) na mkataba ambao Microsoft na Nokia wameingia ni katika upande wa smartphones za Lumia ambazo zina Operating System ya Windows Phone. Sasa, Nokia Lumia ni Microsoft Lumia.
Waliokuwa CEOs, Steve Ballmer(Microsoft)
 na Stephen Elop(Nokia) 
Hili ni jambo  la mafanikio kwa Microsoft kwa kuinunua Nokia, moja ya waliowahi kuwa watengenezaji wakubwa wa mobile devices. Microsoft alishapotea kwenye ramani ya smartphone kufuatia kuporomoka kwa soko lake la mobile devices kama vile PDA (Personal Data Assistant) huko miaka ya nyuma, hivyo kumiliki kampuni kama Nokia pengine kunaweza rudisha hadhi yake. Nokia ataendelea kutengeneza bidhaa zake nyingine kama simu za kawaida (features phones) zikiendelea kutumia brand logo ya Nokia, kasoro kwa smartphones za Lumia ambazo zitatengenezwa na Microsoft.


Teknolojia ya Virtual Reality

Kwa kiasi kikubwa teknolojia hii katika miaka ya nyuma ilikuwa ikionekana ni ya kufikirika tu (science fiction) katika TV series kama Star Trek: The Next Generation iliyotengenezwa mnamo miaka ya 1990 na nyinginezo. Pamoja na kwamba teknolojia hii imekuwa ikitumika kwa miaka mingi katika majeshi mbalimbali, hasa ya anga katika kufundisha wanajeshi kuendesha ndege za kivita na pia katika viwanda vya utengenezaji magari, kama kampuni ya Ford, lakini kwa sasa matumizi yake yanazidi kuongezeka, siku chache mbeleni tutaiona ikitumika majumbani. Virtual Reality ni aina ya teknolojia inayotumia uwezo wa kompyuta kutengeneza mazingira halisi katika hali ya kufikirika (3D environment), hii inahusisha milango yote ya fahamu kuhisi uwepo wa mazingira hayo kuanzia kuhisi, harufu, sauti, miguso na kadhalika. Teknolojia hii ndiyo inayowawezesha marubani kujifunza kuendesha ndege akiwa amekaa kwenye kachumba kadogo lakini akihisi kuendesha ndege halisi na kuhisi yupo angani kiukweli, ina matumizi mengi sana katika kutengeneza mazingira ya kufoji yaliyo sawasawa na yale halisi.

Oculus Rift VR headset
Mwaka wa 2014 teknolojia hii imechukua nafasi kubwa sana, na lengo hasa la teknolojia hii ni kuleta msisimko wa hali ya juu hasa kwa wanaopenda kucheza video games na kuangalia 3D movies, kwa kutumia teknolojia hii inayohusisha kuvaa kifaa maalumu katika kichwa chako (head mounted device/headset) chenye waya mrefu unaounganishwa katika TV utaweza kucheza video games huku ukihisi kuwepo katika video game hiyo, utaweza kusikia sauti halisi, hisia halisi, kwa wengine hufikia hadi mtu kuhisi amekufa kweli kama ikitokea katika video game anayocheza ameuawa, inaleta msisimko ulio halisi sana na wenye mvuto. Kampuni nyingi zimewekeza katika teknolojia hii lakini ni baadhi ambazo zimeonyesha nia ya wazi kabisa katika kuhakikisha teknolojia hii inafika majumbani mapema mwaka 2015. Oculus Rift, Sony na Samsung ndizo kampuni zenye bidhaa hizi ambapo kwa muda huu zipo katika majaribio (beta testing) na ukusanyaji wa maoni ya watumiaji wa teknolojia.
  • Oculus Rift device yao inaitwa Oculus VR.( Oculus Rift imenunuliwa na Facebook).
  • Sony device yao ipo chini ya mradi unaoenda kwa jina la "Project Morpheus" na device hii itatumika sambamba katika game consoles za PlayStation 4.
  • Samsung nao device yao inafahamika kama Samsung Gear VR, katika upande wa software wameshirikiana na Oculus Rift. 


Uzinduzi wa iPhone 6 na iPhone 6 Plus

iPhone 6 Plus na iPhone 6
Septemba 19, mwaka 2014 Dunia ilikuwa "busy" na kuchangamka, uchangamfu huu ulitokana na uzinduzi wa kizazi kingine cha smartphones za Apple, iPhone 6 na iPhone 6 Plus. Mwaka 2013 Apple alizindua iPhone 5S na iPhone 5C. Ni mara ya kwanza kwa Apple kutengeneza smartphone yenye display kubwa, iPhone 6 ina display yenye inchi 4.7 huku iPhone 6 Plus ikiwa na display yenye inchi 5.5, iPhone 6 Plus ni kwa wale walio na mapenzi na phablets. Model zote hizi mbili zina display ambazo zina uwezo wa kuonyesha video katika 1080p(Full-HD), modeli zote zilizopita zilikuwa zina uwezo wa 720p(HD) tu, zikiwa na 326ppi(Pixels Per Inch). iPhone 6 ina pixel density ileile ya 326ppi lakini iPhone 6 Plus ina 401ppi.iPhone 6 Plus inaweza jikunja na kupelekea kuvunjika iwapo mgandamizo ni mkubwa vya kutosha, kinachopinda hasa ni umbo lake la nyuma (chassis) lililotengenezwa kwa madini ya Aluminium.
Kupinda kwa iPhone 6 Plus, maarufu kama bendgate
Tatizo hili pia lilionekana katika iPhone 6, kwa upande wa Apple hakuwahi kusema kwamba tatizo hili linatokana na makosa ya utengenezaji(manufacturing defects) na kudai ya kwamba waliopata tatizo hili ni watu wachache sana. Swala hili lilitawala sana katika mitandao kama Twitter ambapo lilikuwa linajulikana kama "bendgate", makampuni kama Samsung, LG, Asus na mengine walitengeneza vijitangazo vya masihara kwa Apple. Cha kuvutia zaidi, siku chache baada ya skendo hiyo iPhone 6 Plus ilionekana kushinda smartphone nyingi pinzani kama HTC M8 katika video nyingi za kulinganisha uimara wa smartphones. Modeli zote hizi mbili zina NFC(Near Field Communication), maboresho makubwa katika camera, uwezo zaidi wa battery na kadhalika.


Smartwatches zakamata macho ya watu

Moto 360
Hizi ni devices zinazoangukia katika kundi la wearable devices, si devices mpya sana kuwepo katika ulimwengu wa teknolojia, lakini kwa mwaka 2014 tumeona mapinduzi makubwa katika teknolojia yake. Smartwatches kama Samsung Gear S, Gear Live, Motorola Moto 360 na LG G Watch pamoja na smartwatches nyingine kama Pebble watch, iWatch, Asus Zenwatch, Sony Smartwatch 3 n.k zimeleta mwonekano mpya katika ulimwengu wa smartwatch. Smartwatch inaunganishwa na smartphone kwa njia ya bluetooth.

  • Smartwatches zinakuwezesha kufanya mambo mengi mbali na kuangalia muda, hukuonyesha notifications mbalimbali kutoka katika simu yako kama sms au e-mail inapoingia au wakati  simu inapigwa.
  • Unaweza fanya settings za simu yako kama vile kubadili profiles mbalimbali za ringtones.
  • Kucheza na kudhibiti (control) muziki.
  • Unaweza pata huduma ya GPS na mwongozo wa uelekeo.
  • Tengeneza memos, alarm na reminders kwa njia ya sauti.
  • Huduma ya hali ya hewa.
  • Huduma ya Google search kwa njia ya sauti (OK, Google!), inayokuwezesha kuset pamoja na kupata search results mbalimbali kupitia mtandao.
Smartwatches zinapatikana zikiwa na Operating Systems mbalimbali nyingi zikiwa zina Android OS na zinajulikana kama Android Wear, lakini chache kama Samsung Gear S haipo katika mfulizo huu yenyewe ikiwa na Tizen OS kutoka Samsung. Android Wear zinakuwezesha kuinstall apps ambazo zipo compatible kutoka Play Store katika Smartwatch yako, apps ambazo zinaongeza matumizi ya kifaa chako. Kwa sasa Smartwatch sio kifaa muhimu sana kwa mtu wa kawaida lakini kadri muda unavyozidi kwenda labda zinaweza pata kukubalika na watumiaji wa kawaida.


BlackBerry bado yupo hai

Watu wengi walidhani kampuni hii ya Canada ingepotea katika ramani hapo mwaka 2013, miezi michache baada ya uzinduzi wa smartphone ya BlackBerry Z10 inayotumia Operating System ya BlackBerry 10 yenye muonekano na uwezo tofauti kabisa ukilinganisha na smartphones za BlackBerry zilizopita. Smartphone hii iliingiza hasara ya takribani dola za kimarekani 4.4bilioni(sawa na takribani trillioni 7.4 za Kitanzania). Pamoja na kwamba kampuni hii imepita katika wakati mgumu sana lakini imeweza kupambana na mpaka sasa mambo yanazidi kuwa mazuri.
BlackBerry Passport
Kwa mwaka 2014, wamezindua modeli tatu za smartphones, BlackBerry Z3, BlackBerry Passport, na BlackBerry Classic. Chini ya uongozi mpya wa Bwana John S. Chen, wameingia mkataba na kampuni ya Foxconn katika utengenezaji wa smartphones zao. Foxconn wanatengeneza pia bidhaa za kampuni ya Apple kama iPhones, wanatengeneza game consoles za Microsoft Xbox na nyingine nyingi. BlackBerry Passport na BlackBerry Classic zina physical qwerty keypads, lakini displays zake ni touchscreen pia. Bado kuna watu walio na mahitaji makubwa ya smartphones zilizo na physical keypads.


Xiaomi, kampuni inayokua haraka sana

Xiaomi mi4.
Wote tunafahamu ya kwamba Huawei ni kampuni ya China inayofahamika sana duniani kuliko kampuni nyingine zinazotengeneza smartphones katika nchi hiyo. Lakini hali hii ipo karibuni kubadilika. Xiaomi, kampuni inayozidi kupata umaarufu kila kukicha inayofananishwa na Apple kuanzia bidhaa zake hadi jinsi CEO wake anavyovaa. Bwana Lei Jun ndiye CEO na mmiliki wa kampuni hii, mara kadhaa huvaa T-shirt na jeans alizokuwa akivaa marehemu Steve Jobs (mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Apple). Xiaomi wana sera nyingi tofauti ukilinganisha na kampuni nyingine zilizopo nchini China. Bidhaa zao zote kuanzia smartphones hadi tablets huwa haziuzwi sehemu nyingine yoyote ile mbali na katika tovuti yao, hawana mkataba na kampuni yoyote ya uchuuzi(third party vendors) katika kunadi bidhaa zao.
Marehemu Steve Jobs(kushoto) na Lei Jun(kulia).
Moja ya picha ambazo hufananisha watu hawa wawili.
Pamoja na kwamba bidhaa zao huwa na ulingano mkubwa na bidhaa za kampuni ya Apple kama nilivyoainisha hapo mwanzo lakini ni kampuni iliyo na mauzo makubwa sana nchini China na hata nje ya nchi hiyo, kwa sasa ina thamani ya dola za kimarekani 45bilioni(sawa na trilioni 76 za kitanzania). Smartphones za Xiaomi zinatumia firmware ya MIUI ambayo ipo katika Android OS, software hii inaweza kuwa installed katika smartphones nyingine za Android kama custom ROM, mfano katika smartphones za Samsung. Kinachopelekea Xiaomi kupata mafanikio makubwa na kuzidi kujizolea umaarufu ni kwa sababu bidhaa zake huwa katika bei nafuu kabisa na pia zikizingatia ubora. Mwaka 2014, Xiaomi amepata mafanikio makubwa sana kwa kushika nafasi ya tatu kwa makampuni yanayotengeneza smartphones baada ya Samsung ambaye anashika nafasi ya kwanza na Apple akishika nafasi ya pili. Hii ni hatua kubwa kwa kampuni yenye umri wa miaka minne tu kwenye biashara huku ikizishinda kampuni kongwe kama Lenovo na LG.

Makala hii inaendelea sehemu ya pili, kusoma sehemu ya pili:BONYEZA HAPA

No comments :

Post a Comment