Nov 29, 2014

Tatu bora ya smartphones za hali ya juu(high end) mwezi Novemba.

Uchaguzi wa smartphone umekuwa mgumu sana siku hizi, hasa inapofika wakati wa kuchagua ni smartphone ipi ambayo utatumia pesa yako kuinunua. Ugumu huu ni suala la kawaida, hutokana na kwamba aina za smartphones zimekuwa nyingi mno. Watengenezaji waliokuwepo tangu miaka ya nyuma wanazidi kutoa matoleo mapya mara kwa mara, wale wapya nao wanaamka kila siku kuingia katika ushindani wa biashara hii. Afgreenwireless tunakusaidia kukupa listi ya smartphones tatu ambapo kati ya hizi utapata moja inayokufaa kutokana na mahitaji yako. Katika tatu bora hii tumeangalia vitu vikuu kama; uwezo wa battery, uwezo wa processor, ubora wa display, uimara na mengine baadhi. Tumeangalia pia mifumo mbalimbali ya maisha watu wanayoishi, mtu wa ushirika(corporate person) hawezi kuwa na mfumo wa maisha sawa na mwanafunzi wa chuo ambaye anapendelea muziki na sanaa. Watatofautiana vitu vingi katika maisha yao, hata mahitaji yao ya smartphones yatakuwa tofauti. Tumejitahidi kuangalia utofauti kama huu katika kuishi kwa kuangalia mahitaji ya kila mtu katika high end smartphones.



1. HTC One M8

HTC One M8
HTC One ni mfululizo (series) wa high end smartphones kutoka HTC ambazo zinaipa chati sana kampuni hii kwa kukubaliwa sana na watumiaji, si tu kwa sababu HTC ni kampuni inayotumia teknolojia kubwa na ya hali ya juu katika utengenezaji wa smartphones zake, bali pia ni miongoni mwa smartphones zenye muonekano mzuri sana wa umbo.
HTC One M8 ndiyo flagship kwa sasa. Miongoni mwa sifa za kipekee za flagship hii zinazofanya kuwashinda wapinzani wake kama Sony Xperia Z2 na Samsung Galaxy S5 ni kama HTC kutumia Metal Case Body ikilinganishwa na plastiki kwa smartphones nyingine, sifa hii inafanya M8 kuwa na uimara mkubwa sana na kuhimili hali ngumu. Sifa nyingine ni Stereo Speakers za mbele zenye built-in amplifiers zinazotoa stereo sound yenye nguvu kubwa sana, hii ni sifa muhimu kwa watumiaji wanaopenda kusikiliza muziki kwa kutumia speakers za simu.
Pia M8 ina kamera ya mbele yenye 4MP(Ultra pixels capable) na yenye dual-LED na dual tone flash, sifa hii ni mahususi kwa kutengeneza effects kwenye picha, pia ina rekodi video katika ubora wa 1080progressive pixels (Full HD). Kamera ya mbele yenye 5MP yenye uwezo wa kurekodi video katika kiwango cha 1080p Full HD ni kigezo kikubwa kinacho wapiku wapinzani wake, inakupa picha bora kabisa za selfie.
Display  ya M8 ni Super LCD3 (Liquid Crystal Display 3) capacitive touchscreen yenye ukubwa wa inchi 5.0, ikiwa na resolution ya (1080 x 1920 pixels). Ujazo wa display hii ni 441 ppi na inalindwa na Gorilla Glass 3 ikiwa na HTC Sense UI 6.0. Kwa sifa za display hii, hakika ni imara na yenye mwonekano mzuri na wa hali ya juu sana kutokana na kuwa na pixel density kubwa (441).
Inapatikana katika matoleo mawili ya 16GB na 32GB zikiwa na uwezo wa kuongeza microSD card hadi 128GB, na ukubwa wa RAM katika matoleo yote mawili ni 2GB. Processor yake ni ya Quad Core( CPU nne) kila moja ikiwa na spidi ya 2.3GHz.
Ina battery lisilotoka (non-removable) lenye uwezo wa 2600 mAh.
HTC One M8 inatoka na Android OS v4.4.4 Kitkat lakini unaweza upgrade mpaka Android 5.0 Lollipop pale utapotolewa rasmi.

Sifa (Specifications) nyinginezo

  • Ina uwezo wa mtandao wa 4G LTE(Long Term Evolution).
  • Ina Teknolojia mpya ya Fast Battery Charging yenye uwezo wa kuchaji 60% ndani ya dakika 30.
  • Kamera yenye uwezo wa kurekodi video na kupiga picha kwa wakati mmoja.
  • Toleo la China na Asia lina CPU yenye spidi ya 2.5 GHz.
  •  Ipo ndani ya chipset ya Qualcomm Snapdragon 801.


2. Google's Motorola Nexus 6

Je, Unapendelea phablet ? Nexus 6 inafaa zaidi. Kama hauna tatizo na smartphones zenye display na umbo kubwa na pia haujali kubeba simu kubwa katika mfuko wako, basi hili ndilo chaguo likufaalo.
Kinachofanya Nexus 6 kuonekana tofauti na wapinzani wenzake kama Samsung Galaxy Note 4, LG G3 na Sony Xperia Z3 ni kwamba device yoyote ya Nexus huwa ni ya kwanza kupata software update ya Android OS, hivyo siku zote utakuwa mstari wa mbele katika kupata updates. Phablet hii imetengenezwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Google na Motorola, ikumbukwe kwamba mnamo mwaka 2012 Google aliinunua kampuni ya Motorola na mwaka huu mwanzoni aliiuza kwa kampuni ya China inayojihusisha na utengenezaji wa kompyuta inayofahamika kama Lenovo.
Google's Motorola Nexus 6
Ni Android device ya kwanza kuja katika box ikiwa na latest software ya Android, inayofahamika kama Android Lollipop 5.0. Hauhitaji kununua Sony Xperia Z3 kwa vile ina uwezo wa kuzuia maji(water tight) kwa sababu hata Nexus 6 ina uwezo huo pia.
Ina display yenye ukubwa wa inchi 6 yenye resolution ya (1440 X 2560) huku ikiwa inatumia teknolojia ya AMOLED(Active Matrix Organic Light Emitting Diode) ambayo ina muonekano murua sana wenye kukupa sharp images, ina kiasi cha pixel density 493ppi. Display hii ipo protected na Gorilla Glass 3, inapatikana katika modeli ya 32GB na 64GB zote mbili zikiwa na RAM yenye 3GB. Processor yake ni ya Quad Core( CPU nne) kila moja ikiwa na spidi ya 2.7GHz. 
Ina battery yenye uwezo wa 3220mAh, imezidiwa na battery ya BlackBerry Passport lakini utofauti huu hauonekani sana katika matumizi.

Sifa(Specifications) nyinginezo.

  • Ina uwezo wa mtandao wa 3G na 4G.
  • Ina camera ya nyuma(primary/ rear camera) yenye uwezo wa 13MP  na pia camera ya mbele(secondary camera) yenye uwezo wa 2MP. Camera ya nyuma ina uwezo wa kuchukua Full HD(2160p).
  • Ipo ndani ya chipset ya  Qualcomm Snapdragon 805, ikiwa ni chipset ya juu kidogo kuliko Snapdragon 801 ambayo ndiyo chipset ya HTC One M8 na BB Passport.



3. BlackBerry Passport

BlackBerry Passport
Pengine wewe ni mpenzi wa smartphones zenye physical qwerty keypads, na simu za full touchscreen hazikuletei ladha kama ile unayopata katika physical qwerty keypads smartphone. BlackBerry Passport yupo kwa ajili yako. Siku hizi soko la smartphones limetawaliwa na simu kama za Samsung, Apple, HTC na nyinginezo ambazo zote zinatumia teknolojia ya full capacitive touchscreen.
Smartphone hii ya BlackBerry imetengenezwa mahususi kwa watu wale wanaofanya kazi muda wowote na mahali popote, ukiwa na physical qwerty keypads ni rahisi kuandika barua pepe ndefu sana bila kupata matatizo ya kutype na cha kushangaza zaidi ni kwamba; keypads hizi sio kwa ajili ya kutype tu, zinakuwezesha kunavigate kama vile unavyotumia trackpad,utakavyo tembeza kidole chako kwenda juu au chini ukiwa unagusa hizo keypads na display pia itapanda juu au chini kwa hiyo hakuna haja ya kutumia touchscreen katika kunavigate.
Ina battery yenye uwezo mkubwa inayokuwezesha kufanya kazi siku nzima bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa chaji katikati ya siku, battery hii ina uwezo wa 3450mAh(milli-ampere hour). Ina display yenye resolution ya (1440pixels X 1440pixels) yenye ukubwa wa 4.5 inch, display hii ina muonekano maridadi kabisa wenye kukupa taswira iliyo ya hali ya juu ikiwa na kiasi cha 453ppi(pixel per inch)/pixel density ikiwa protected na kioo cha Gorilla Glass 3, ni display inayotumia teknolojia ya IPS LCD(In-Plane Switch Liquid Crystal Display).
Faida za kutumia display ya aina hii ni kwamba, inakupa muonekano mzuri katika viewing angle kubwa, hii ina maana hata ukiwa unatazama display hii kiubavu bado utaweza kuona clearly na pia inakupa touchscreen response ya haraka sana unaipogusa, pamoja na kwamba inatumia nishati kubwa kidogo ya umeme ukilinganisha na display nyinginezo kama SUPER-AMOLED au SUPER LCD's lakini suala hili halina madhara katika smartphone hii kwa sababu ya uwepo wa battery yenye uwezo mkubwa.
 Processor yake ni Quad Core( Central Processing Unit(CPU) nne) na kila moja ikiwa na spidi ya 2.26GHz(Giga Hertz), hii ni processor yenye uwezo mkubwa wa kutafsiri taarifa nyingi kwa wakati mmoja bila kuathiri ufanyaji kazi wa simu na kiasi cha chaji katika battery. Kwa miaka mingi, BlackBerry amekuwa akitengeneza smartphones zake kwa kuzingatia uimara wa simu ili kuepuka matatizo ya mipasuko pale simu inapodondoka. Simu imetengenezwa na plastic body lakini inahimili misukosuko mingi sana ukizingatia kwamba ipo equipped na Gorilla Glass 3 pia.

Sifa(Specifications) nyinginezo. 
  •  Ina support 4G LTE(Long Term Evolution).
  • Internal storage yenye uwezo wa 32GB na pia uwezo wa kuweka micro sd card(memory) yenye ukubwa hadi 128GB.
  • RAM(Random Access Memory) yenye uwezo wa 3GB.
  • Camera ya nyuma(primary camera) yenye uwezo wa 13MP ikiwa na LED Flash na uwezo wa kuchukua video za Full HD(1080p) na pia camera ya mbele yenye 2MP. 
  • Inatumia operating system(OS) ya BlackBerry 10.3 OS.
  • Ipo ndani ya chipset ya Qualcomm Snapdragon 801.

No comments :

Post a Comment