Oct 5, 2014

BlackBerry Passport versus iPhone 6 plus; Kazi versus Starehe.

Mwezi jana, yaani Septemba umekuwa bize sana katika ulimwengu wa teknolojia, hasa ya smartphones. Apple alizindua model nyingine ya iPhone zikiwa ni model mbili, iPhone 6 na iPhone 6 plus. Pia alizindua smartwatch. BlackBerry hajafa, anadunda kama kawaida na hakusita kuleta flagship nyingine katika mwezi huohuo wa Septemba, BlackBerry Passport! ndivyo inavyojulikana. Huawei pia alizindua simu zake za line ya Ascend Mate, sitamzungumzia sana kwa sababu si mhusika katika makala hii.

iPhone 6 plus

Linapokuja swala la kuchagua simu ipi ni bora zaidi ya nyingine au simu ipi inafaa zaidi kununua, specifications si jambo pekee linaloweza kukupa suluhisho la utata huu. Mtindo wa maisha(lifestyle) ni moja ya swala la kuzingatia katika kujua ni simu ipi inakufaa. Hii ina maana kubwa sana! iPhone 6 plus na BlackBerry Passport
zote ni smartphones tena za hali ya
juu(high end), lakini linapokuja swala la utendaji kazi(functionality) kuna utofauti kwa kiasi fulani, na usipojua unachokihitaji unaweza kuangukia katika mikono isiyo sahihi. Naweza kukupa mfano mdogo tu; kati ya HTC M8 na Sony Xperia Z3, ni simu ipi inafaa kwa ambaye yupo katika activities za photographing? jibu ni rahisi, Sony Xperia Z3 na ni kwa sababu Z3 ina camera nzuri ya yenye kiwango zaidi ya M8. Kama mtu huyu atachagua M8(kwa sababu ya dual primary camera) au smartphone nyingine yoyote yenye camera performance iliyo flat pia hata kazi zake zitakuwa flat, hiyo ni hasara. Tuone ni vipi tunalinganisha na kutofautisha specs sambamba na functionality ya BlackBerry Passport pamoja na iPhone 6 plus.
BlackBerry Passport

UMBO(FORM FACTOR).


Umbo la BlackBerry Passport ni la ajabu kidogo, ili kushika simu hii kwa mkono mmoja inahitajika kuwa na kiganja kipana, ni pana sana na ni fupi ukilinganisha na flagship smartphones nyingi za sasa na inafanana na LG Vu, ina vipimo vya(128x90.3x9.3)mm. Tofauti na iPhone 6 plus, Passport ina IPS LCD display yenye ukubwa inchi 4.5 na physical qwerty keypads ambazo zipo katika mistari mitatu tu(3 rows). Keypad hizi zina uwezo wa kuhisi kidole chako kinapopita juu yake, kama utamove kidole kuanzia keypad za mstari wa juu kwenda chini basi display nayo itashuka, vivyo hivyo utapopeleka kulia kwenda kushoto au kinyume. Hii ina maana ni keypads lakini wakati huohuo zinaact kama trackpad. iPhone 6 plus ni pure phablet, na hii ndiyo phablet ya kwanza kabisa kwa Apple, kwa nyuma inafanana kiasi fulani na HTC M8. Ni full touchscreen, ina display ya LED-Backlit IPS LCD yenye ukubwa wa inchi 5.5. Kwa sifa za umbo katika simu hizi mbili, Passport inafaa sana kwa mtu ambaye anatuma emails mara nyingi na muda mwingi anafanya kazi kwenye simu kwa sababu ya uwepo wa physical keypads, kwa upande mwingine ukubwa wa display ya 6 plus unafaa sana kwa kuangalia movies kucheza games na kadhalika.
LG Vu, smartphone inayofanana umbo na BlackBerry Passport.


UBORA WA DISPLAY NA CAMERA.


Zote hizi zinatumia teknolojia ya IPS LCD, sifa za display za aina hii huwa zinatoa rangi halisi na iliyo na mwanga wa kutulia(warm brightness). BlackBerry Passport ina pixel density ya kiasi cha 453ppi(pixel per inch) na iPhone 6 plus ina 401ppi. Passport ina appear kuwa sharp zaidi lakini 6 plus inang'aa zaidi(bright), kwa kifupi display zote hizi mbili ziko karibuni sawa, hakuna tofauti kubwa sana na pia zote zinaweza display 1080p videos(Full HD). Katika swala la camera, Passport imemzidi 6 plus kwa megapixels. Passport ikiwa na 13MP huku 6 plus ikiwa na 8MP, zote mbili zina OIS(optical image stabilization) inayofanya picha kuonekana sharp na zenye rangi halisi, iPhone 6 ina dual led flash(taa za mwanga kwa ajili ya camera) inayosaidia kukupa mwanga mkali zaidi wakati wa kupiga picha katika mwanga hafifu, hasa nyakati za usiku. Display za simu zote hizi mbili zipo protected na Gorilla Glass 3, lakini kwa iPhone 6 plus ina features  zaidi kama Oleophobic(fat-fear) coating ambayo inazuia kioo kubaki na alama za vidole( zitokanazo na jasho au mafuta) wakati unatumia simu yako, hii inafanya kioo kubaki clear na utaweza kuona vizuri hata nje katika mwanga wa jua mkali.


NGUVU YA UTENDAJI KAZI(PROCESSING POWER) NA BATTERY LIFE.


Passport ina processor ya Snapdragon 801 SoC(System on Chip) ambayo inasifika sana kwa kutumia nishati kidogo ya umeme bila kuathiri utendaji wake wa kazi. Processor hii ina uwezo wa spidi ya 2.26GHz ikiwa na CPU nne(Quad Core) na pia ina GPU(Graphics Processing Unit) aina ya Adreno. iPhone 6 plus ina processor ya ARM inayoitwa Cyclone yenye uwezo wa spidi ya 1.4GHz ikiwa na CPU mbili(Dual Core) ikitumia GPU ya Power VR GX6450. Unaweza kuona kwamba 6 Plus kapitwa mbali sana kwa kuangalia specs za processing power, ukweli ni kwamba: performance ya simu hizi zote mbili ni karibu sawasawa, hii ni kwa sababu Apple's iOS iko well optimised na inaweza perform haraka hata kwa CPU yenye uwezo wa kawaida, ni tofauti na OS nyingine mfano Android, huitaji processing power kubwa ili kuperform kwa haraka zaidi. Battery ya Passport ni kubwa sana ikiwa na uwezo 3450mAh(milli Ampere hour) huku 6 plus ikiwa na 2915mAh, Passport inazidi masaa kama mawili katika matumizi. Lakini battery zote hizi mbili ni bora. Kampuni zote hizi mbili miaka iliyopita zimekuwa zikipata malalamiko kutoka kwa wateja wao katika ubora wa battery, ni hakika wote wametambua tatizo hili na wameleta maboresho.


OPERATING SYSTEM.


Zote zinazotumia OS mpya kabisa katika macho yetu. iOS 8 katika iPhone 6 plus na BlackBerry OS 10.3 katika BlackBerry Passport. iOS 8 haijabadilika sana kimuonekano (UI) ukilinganisha na iOS 7, baadhi ya vitu vimeongezwa na vingine kurekebishwa. BlackBerry OS 10. 3 ina utofauti mkubwa sana OS 10.2, muonekano wake (UI) umeboreshwa maradufu na features nyingi nyingi zimeongezwa. Utofauti mkubwa unaokuja katika OS hizi ni huu, number ya apps katika stores zao. BlackBerry ana apps chache sana katika store yake ukilinganisha na iOS ambaye mpaka sasa anaongoza kwa kuwa na apps nyingi katika store yake kwa OS platform zote. Pamoja na kwamba sasa unaweza kutumia asilimia 98 ya apps za Android(Thanks to Android Runtime) katika BlackBerry 10 device, lakini bado hicho si kivutio kwa wale wapenzi wa apps. Watu wengi hutaka apps maalumu kwa OS(native apps). Kama wewe ni mpenzi wa apps, tena native. BlackBerry 10 devices zote si mahala pako.


STORAGE.


BlackBerry Passport inakuja katika model moja tu ya storage, yenye 32GB. Ikiwa na RAM ya 3GB, unaweza pia kuweka micro sd card hadi yenye uwezo wa 128GB. iPhone 6 plus ina model za 16GB,64GB NA 128GB zote hizi zikiwa na RAM yenye uwezo wa 1GB, hauwezi kuweka memory card, ina maana unakuwa limited katika swala la storage.

Kwa specs. zote na comparisons hapo juu. Jukumu la kujua una mfumo gani wa maisha na unahitaji simu ipi linabaki kwako wewe mtumiaji. Na baada ya kutambua hilo, specs zitakuaongoza katika kufanya chaguo bora zaidi.


No comments :

Post a Comment