Oct 19, 2013

Ijue Foxconn,kiwanda kikubwa kuliko vyote duniani cha kutengeneza vifaa vya kielectroniki.Hapa ndipo iPhone zinapotengenezwa.

Kwa jina lingine kinajulikana kama Hon Hai Precision Industry Company Ltd. lakini maarufu kinajulikana zaidi kama Foxconn.



 Kampuni hii imeanza mwaka 1974,huko wilaya ya Tucheng,New Taipei jimbo la Taiwan lililopo nchini China.Ilianzishwa na Bwana Terry Gou na ndiye rais na mwenyekiti wa kampuni hiyo mpaka sasa.Ndiyo kampuni kubwa ya kuzalisha vifaa vya kielectroniki kuliko zote duniani,ina wafanyakazi wapatao milioni moja laki mbili na thelatini elfu mpaka kufikia mwaka 2012.

Kiwanda hiki hakizalishi bidhaa kwa brand yake bali hutengenezea kampuni nyingine na kuweka brand za kampuni hizo.Hutengenezea bidhaa makampuni mengi ya Ulaya,Marekani na Japan.Makampuni mengi sasa huzalisha bidhaa nchini China kwa sababu ya unafuu wa kuzalisha bidhaa hizi ukilinganisha na maeneo mengine kama Ulaya na Marekani.

 Baadhi ya bidhaa wanazotengeneza ni kama simu za iPhone,iPad,iPod,tablet za Kindle,kompyuta za HP,na game consoles za Xbox,Nintendo Wii U na Play Station.


Kampuni hii imeingia katika migogoro mingi katika utoaji wake wa ajira,ukizingatia hii ndiyo  kampuni kubwa binafsi nchini China inayotoa ajira kwa wingi.Mwaka 2012 kampuni ya Apple iliipa kazi Chama cha ajira za halali kufanya ukaguzi katika kiwanda hicho ili kuangalia mazingira ya kazi yakoje baada ya kuwepo tetesi kwamba kuna vijana wadogo chini ya umri wa miaka 16 wanaofanya kazi katika kiwanda hicho.

 Kampuni hii haina kiwanda China tu bali ina viwanda sehemu nyingine za Asia kama India na mabara mengine kama Ulayana Amerika ya Kusini.




No comments :

Post a Comment