Televisheni za ubora wa 4K (Ultra-High Definition)
Siku hizi, watu wengi wanapowaza kununua televisheni mawazo yote huwa katika flatscreen TV. Lakini, kinachofanya TV hizi kuwa ghali si ukubwa wake, ni aina ya teknolojia itumikayo katika hizi TV, kuanzia software yake, display inayotumika na ubora wa vifaa vingine viundavyo TV hiyo. 4K TV ni aina ya runinga yenye uwezo wa kuonyesha ubora wa picha ulio na kiwango cha 4096 (4K) pixels katika resolution ya upana (horizontal resolution), resolution hii kwa jina lingine inafahamika kama Ultra-High Definition (UHD).
4K TV zina uwezo wa kutoa ubora wa picha mara nne zaidi ya Full-HD TV ambazo horizontal resolution yake ni 1080pixels, kuna baadhi ya 4K TVs ambazo zina umbo la kujikunja pia (Curved TVs). TV nyingi za flatscreen zilizo nafuu zina uwezo wa aitha HD katika 720pixels au Full-HD katika 1080pixels. LG na Samsung ni kampuni zilizo maarufu sana na zenye mafanikio makubwa katika teknolojia hii, pia Sony, Philips, Toshiba, Panasonic na Asus hawapo nyuma katika utengenezaji wa TV za teknolojia hii.
Kitaalamu zaidi ubora wa 4K si sawa na Ultra-HD, 4K ni kubwa kuliko Ultra-HD kwa sababu 4K ina resolution ya 4096 x 2160 pixels wakati Ultra-HD ikiwa na resolution ya 3840 x 2160pixels. Si tofauti kubwa sana hasa kwa mtumiaji wa TV hizo lakini linapokuja suala la matangazo ya kibiashara, hilo linahusika.
Si tu 4K pekee ndiyo iliyopata nafasi ya kutikisa teknolojia ya TVs kwa 2014, tumeona pia LG, Dell na Apple wakiwa katika hali ya kushindana baada ya kutengeneza PC monitors zenye displays za ubora wa 5K. Kutokana na kutumia teknolojia ya kisasa, TVs na monitor hizi si za bei ndogo, kwa mfano PC monitors ya Dell inagharimu US$2,000 sawa na Tsh. 3,400,000. Hii ni changamoto kwa mtumiaji wa kawaida. Lakini, kadiri muda unavyozidi kwenda teknolojia hii itazidi kushuka gharama yake.
iOS 8 na Android Lollipop 5.0 ni software updates zilizotolewa mwaka 2014 na Apple na Google kwa mtiririko. iOS 8 ikichukua nafasi ya iOS 7 na Android Lollipop 5.0 ikichukua nafasi ya Android KitKat 4.4. iOS 8 ilitolewa mnamo mwezi wa tisa ikiahidi kuleta maboresho makubwa sana katika simu za iPhones. Mengi yalijiri muda mfupi baada ya update hii kutoka, kwanza, ilitolewa kwa njia ya OTA(Over The Air) na baada ya muda ilianza patikana kupitia iTunes. Ilileta shida pale ambapo ilihitaji kiasi cha 6GB ya internal memory ili kuweza kukamilisha updating process, kisichofurahisha ni kwamba internal memory hii haikutumika kabisa baada ya kukamilika kwa process ya update, ilipelekea watu kupoteza data mbalimbali katika iPhones zao. Hata wale waliofanikiwa kufanya update walipata matatizo kama simu kupoteza network mara kwa mara, battery kuisha mapema, apps kuacha kufanya kazi ghafla na mengineyo. Apple walitoa baadhi ya software updates ndogondogo(minor updates) ili kurekebisha matatizo yaliyojitokeza ambapo kwa simu nyingi matatizo haya yalipata ufumbuzi.
Tarehe 12 mwezi Novemba Android Lollipop ilitolewa rasmi kwa njia ya OTA, ikipatikana kwa devices za Nexus na Google Play Edition. Watumiaji wengi wa tablet ya Nexus 7(2013) walipata matatizo katika devices zao kama kushindwa kucheza video vizuri mara baada ya kufanya update hii. Google aliacha kutoa update ya software hii na baada ya wiki chache aliendelea tena kutoa update hii ikiwa na maboresho zaidi, pamoja na kwamba matatizo yaliyojitokeza mwanzo kwa sasa hayapo kutokana lakini kuna malalamiko ya kwamba battery inaisha chaji mapema.
![]() |
Tofauti ya picha kati ya Full-HD na Ultra-HD |
Kitaalamu zaidi ubora wa 4K si sawa na Ultra-HD, 4K ni kubwa kuliko Ultra-HD kwa sababu 4K ina resolution ya 4096 x 2160 pixels wakati Ultra-HD ikiwa na resolution ya 3840 x 2160pixels. Si tofauti kubwa sana hasa kwa mtumiaji wa TV hizo lakini linapokuja suala la matangazo ya kibiashara, hilo linahusika.
Si tu 4K pekee ndiyo iliyopata nafasi ya kutikisa teknolojia ya TVs kwa 2014, tumeona pia LG, Dell na Apple wakiwa katika hali ya kushindana baada ya kutengeneza PC monitors zenye displays za ubora wa 5K. Kutokana na kutumia teknolojia ya kisasa, TVs na monitor hizi si za bei ndogo, kwa mfano PC monitors ya Dell inagharimu US$2,000 sawa na Tsh. 3,400,000. Hii ni changamoto kwa mtumiaji wa kawaida. Lakini, kadiri muda unavyozidi kwenda teknolojia hii itazidi kushuka gharama yake.
Devices za Nexus zaongezeka
Si tu kwamba Google inajihusisha na masuala yahusuyo softwares na kuuza matangazo, wanajihusisha na hardware pia. Hushirikiana na kampuni kubwa duniani kutengeneza devices kama smartphones na tablets, mradi huu unafahamika kwa jina la Nexus. Nexus smartphone ya kwanza ilizinduliwa mnamo mwezi Januari 2010 ikipewa jina la Nexus One, ambapo Google alishirikiana na HTC. Miaka miwili baadaye walizindua tablet ya Nexus 7 wakishirikiana na Asus. Kumekuwa na mfululizo wa devices hizi na kwa mwaka 2014 tumeona Nexus devices mbili mpya, Nexus 6 na Nexus 9.
Nexus 6 imetengenezwa kwa ushirikiano na Motorola Mobility, ni smartphone yenye sifa zote za kuitwa phablet ikiwa na display ya AMOLED yenye ukubwa wa inchi 5.96 (1440 X 2560pixels) ikiwa na pixel density ya 493ppi Quad High Definition (QHD). Hakika hii ni display yenye muonekano mzuri sana wa picha, sifa nyingine katika smartphone hii ni uwepo wa dual front-facing speakers zinazotoa sauti nzuri kwa muziki, kuangalia movie na hata katika kucheza games. Nexus 6 ni muendelezo (successor) wa Nexus 5 iliyotoka mwaka 2013.
Kwa upande wa Nexus 9(inafahamika pia kama HTC Volantis) ambayo imetengenezwa kwa ushirikiano na HTC ina display ya IPS LCD (In-Plane Switch Liquid Crystal Display) ikiwa na ukubwa wa inchi 8.9 na pixel density kiasi cha 281ppi, ina resolution ya 1536x2048 pixels.
Nexus 6 na 9 zina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kutokana na betri zake kuwa na uwezo mkubwa. Cha kuvutia zaidi katika devices hizi ni kwamba zinakuja zikiwa tayari na latest version ya Android OS, Android Lollipop 5.0. Devices za Nexus zote hupewa kipaumbele pale software update ya Android OS inapotoka.
![]() |
Motorola Nexus 6 |

Smartphones zaanza kutumia fingerprint scanners
Biometrics ni vipimo vinavyofanywa katika mwili wa binadamu ili kupata utambulisho wa kipekee wa mhusika na kuruhusu matumizi ya huduma fulani kwa mtu aliyehakikiwa pekee. Fingerprint ni moja ya vipimo hivyo, kikiwa na ufanisi wa hali ya juu. Huhusisha kuscan imprints za vidole hasa kidole gumba. Fingerprint inatumika katika matumizi mbalimbali mengi yakiwa ni ya kiusalama na hata malipo.
Lakini kwa mwaka 2014 tumeona teknolojia hii ikihamia katika upande wa Smartphones. Apple, Samsung, HTC na Huawei ni makampuni ya mwanzo kabisa katika kutumia teknolojia hii katika flagships smartphones zao. Smartphones kama Samsumg Galaxy S5, Samsung Galaxy Note 4, iPhone 6 na iPhone 6 plus kutoka Apple, Huawei Ascend Mate 7 na HTC One Max ndizo zenye uwezo wa kuscan fingerprint.
Ikumbukwe pia mwishoni mwa mwaka 2013, Apple walitoa iPhone 5S mwezi Septemba ikiwa ndio smartphone ya kwanza kutoka Apple kuwa na fingerprint scanner.Tofauti na passwords na pattern locks ambazo zinaweza kupatikana au hata kuhisiwa na kumwezesha mtu kupata access katika smartphone husika, fingerprint inakupa usalama na uhakika wa smartphone yako pamoja na data zake hata endapo itaibiwa au kupotea. Ni mmiliki wa smartphone hiyo tu ndiye mwenye uwezo wa kuifungua.
![]() |
Malipo kwa kutumia fingerprint scanner. |

Majanga ya software updates

Tarehe 12 mwezi Novemba Android Lollipop ilitolewa rasmi kwa njia ya OTA, ikipatikana kwa devices za Nexus na Google Play Edition. Watumiaji wengi wa tablet ya Nexus 7(2013) walipata matatizo katika devices zao kama kushindwa kucheza video vizuri mara baada ya kufanya update hii. Google aliacha kutoa update ya software hii na baada ya wiki chache aliendelea tena kutoa update hii ikiwa na maboresho zaidi, pamoja na kwamba matatizo yaliyojitokeza mwanzo kwa sasa hayapo kutokana lakini kuna malalamiko ya kwamba battery inaisha chaji mapema.
Huawei azidi kupata nafasi sokoni
Huawei Technologies Co.Ltd ni kampuni kutoka China inayojihusisha na kutengeneza vifaa vya mawasiliano pamoja na kutoa huduma za mawasiliano. Ni kampuni kubwa zaidi duniani kwa utengenezaji wa vifaa vya mawasiliano(Telecommunications equipments and infrastructure), karibia kila mnara wa mtandao wa simu utaokwenda ni ngumu kukosekana kifaa cha Huawei. Katika upande wa smartphone kwa mwaka 2014 Huawei ameonyesha uwezo mkubwa sana wa kiteknolojia katika safu hii. Amezindua smartphones kama Huawei Ascend Mate 7, Huawei Ascend P7, Huawei Honor 6 na nyinginezo. Smartphones hizi zina kiwango sawa na pengine zaidi ukilinganisha na smartphones brand nyingine kama Samsung, Sony n,k.
Miongoni mwa hatua za mafanikio ambazo zimefanywa na Huawei ni kuanza kuuza bidhaa zake kupitia mtandao (online), na mafanikio yamejionyesha zaidi katika mfulululizo wa Honor smartphones ambapo kwa mwaka mmoja ameweza kuuza smartphones takriban million 19 za modeli hiyo. Kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao ndiyo lengo la makampuni mengi ya smartphones kwa sababu ya kupunguza gharama za usafirishaji ambazo huchukua hadi asilimia 30 ya gharama ya kifaa chote. Biashara kwa njia ya mtandao(e-commerce) ndiyo mfumo unaofanywa na makampuni kama Apple na Xiaomi na ndiyo kitovu cha mafanikio makubwa yalofikiwa na Xiaomi.
Smartphone hii inasupport Android OS, lakini inatumia custom version ya Android OS ambayo inafahamika kama Cyanogenmod, Cyanogenmod inaongozwa na aliyewahi kuwa developer wa software za Samsung, Bwana Steve Kondik. Cyanogenmod inakuwezesha kufanya customization nyingi sana katika smartphone hii tofauti na smartphone nyingine zinazotumia official Android OS kutoka Google.
Kwa upande wa kamera, ina 13MP kwa nyuma na mbele ni 5MP na kamera zote zinaweza chukua video katika ubora wa HD. One ina betri lenye nguvu ya 3100mAh na pia inatoka na Android OS v4.4.2 (KitKat)
Kwa sifa hizo flagship hii inawekwa kundi moja na HTC M8, Samsung Galaxy Note 4 , LG G3 na iPhone 6 Plus. Ikiwa inalingana kwa sifa na high-end smartphones hizo, huku zikizidiana mambo machache, toleo la GB 16 linapatikana kwa kiasi cha US$299.99, huku HTC M8 ikipatikana kwa US$716.69. Tofauti ya bei na sifa zake ni kubwa kiasi cha kuipa umaarufu ghafla katika soko la smartphones.
OnePlus One haipatikani kwenye maduka ya smartphones ya kawaida, ila tu kwenye website yao. Kitu kingine ni kwamba hata ukitaka kununua smartphone hii kwenye website yao, ni mpaka uwe na mwaliko (invitation) ndiyo ufanikishe jambo hilo, au usubiri iingie soko la jumuiya (general public) kwa kipindi kifupi cha muda ambapo kwa muda huu walitoa nafasi yenye kikomo kwa mtu yoyote kununua mpaka tarehe 25 mwezi Decemba kama zawadi ya msimu wa sikukuu.
Haya ni baadhi ya mambo yaliyojiri katika mwaka wa 2014 kwa upande wa teknolojia ya smartdevices. Mambo mengi mazuri yatakuwepo katika mwaka ujao wa 2015. Mengi yatayojiri katika mwaka ujao chimbuko lake limeanzia katika mwaka 2014. Tegemea mambo mengi sana ya kusisimua katika mwaka ujao wa 2015.
![]() |
Huawei Honor 6 |
OnePlus ateka "attention" ya soko la smartphones
OnePlus ni kampuni kutoka China iliyoanzishwa mnamo December 2013 na aliyekuwa Vice President wa kampuni ya Oppo, Bwana Pete Lau. Kampuni hii imepata umaarufu wa ghafla kutokana na bidhaa yake iliyotengeneza na kuiingiza sokoni mwezi April 2014. OnePlus One, ni flagship smartphones kutoka OnePlus iliyoleta gumzo si tu baada ya kuingia sokoni, ila hata kabla ya kuzinduliwa rasmi. OnePlus One ni moja kati ya high-end smartphones zilizotoka kwa mwaka 2014 lakini tofauti kubwa na high-end smartphones nyingine ni bei yake.
OnePlus One inapatikana katika matoleo mawili ya 16GB na 64GB, huku yote yakiwa na display ya inchi 5.5 LTPS LCD kwa resolution ya 1920x1080pixels huku ikiwa na 401ppi, display hii inalindwa na Corning Gorilla Glass 3. Chipset yake ni Snapdragon 801 ikiwa na processor yenye core nne (Quad-core) zenye uwezo wa 2.5GHz kila moja, na RAM ya GB 3.Smartphone hii inasupport Android OS, lakini inatumia custom version ya Android OS ambayo inafahamika kama Cyanogenmod, Cyanogenmod inaongozwa na aliyewahi kuwa developer wa software za Samsung, Bwana Steve Kondik. Cyanogenmod inakuwezesha kufanya customization nyingi sana katika smartphone hii tofauti na smartphone nyingine zinazotumia official Android OS kutoka Google.
Kwa upande wa kamera, ina 13MP kwa nyuma na mbele ni 5MP na kamera zote zinaweza chukua video katika ubora wa HD. One ina betri lenye nguvu ya 3100mAh na pia inatoka na Android OS v4.4.2 (KitKat)
Kwa sifa hizo flagship hii inawekwa kundi moja na HTC M8, Samsung Galaxy Note 4 , LG G3 na iPhone 6 Plus. Ikiwa inalingana kwa sifa na high-end smartphones hizo, huku zikizidiana mambo machache, toleo la GB 16 linapatikana kwa kiasi cha US$299.99, huku HTC M8 ikipatikana kwa US$716.69. Tofauti ya bei na sifa zake ni kubwa kiasi cha kuipa umaarufu ghafla katika soko la smartphones.
OnePlus One haipatikani kwenye maduka ya smartphones ya kawaida, ila tu kwenye website yao. Kitu kingine ni kwamba hata ukitaka kununua smartphone hii kwenye website yao, ni mpaka uwe na mwaliko (invitation) ndiyo ufanikishe jambo hilo, au usubiri iingie soko la jumuiya (general public) kwa kipindi kifupi cha muda ambapo kwa muda huu walitoa nafasi yenye kikomo kwa mtu yoyote kununua mpaka tarehe 25 mwezi Decemba kama zawadi ya msimu wa sikukuu.
Haya ni baadhi ya mambo yaliyojiri katika mwaka wa 2014 kwa upande wa teknolojia ya smartdevices. Mambo mengi mazuri yatakuwepo katika mwaka ujao wa 2015. Mengi yatayojiri katika mwaka ujao chimbuko lake limeanzia katika mwaka 2014. Tegemea mambo mengi sana ya kusisimua katika mwaka ujao wa 2015.
No comments :
Post a Comment