1.LG Google Nexus 5.
Moja ya vitu vinavyonifanya kuipenda sana smartphone hii ni kutumia user interface(UI) ya Nexus. Kwa sasa inatumia Android 4.4 Kit Kat.Uzuri wa wa device za Nexus ni kwamba zenyewe huwa zinakuwa za kwanza kabisa kupata updates za operating system software.Nexus 5 inakuja katika boksi ikiwa tayari na Android 4.4 Kit Kat na hii ndiyo device iliyotumika kuzindua version hii ya Android ya Kit Kat.Simu hii imetengenezwa kwa ubia wa Google na LG. Sifa zake ni hizi:
- Ina display yenye ukubwa wa inchi 4.95na pixel density kiasi cha 445ppi yenye uwezo wa kuonesha full high definition(HD) katika 1080pixels.
- Display hii inalindwa na kioo cha Gorilla Glass 3 ambacho kinazuia michubuko na kuvunjika kwa hali ya juu.
- Ni smartphone inayotumia aina ya mawasiliano ya GSM,ina uwezo wa 3G na 4G(LTE). Inatumia sim card ndogo(micro sim).
- Inakuja katika boksi ikiwa na Android 4.4,baada ya hapo unaweza update mpaka Android 4.4.2 ambayo ni version ya sasa ya Android.
- Processor yake ina uwezo wa 2.3Ghz huku ikiwa ni quadcore(yenye CPU nne),ina RAM ya 2GB.Hii inaifanya kuwa bora kabisa katika kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja bila kuathiri kasi ya utendaji na pia inafaa sana kwa kucheza games.
- Kamera ya nyuma ina 8MP ikiwa na LED flash kwa ajili ya kupiga picha katika mwanga hafifu,kamera hii inatoa picha zenye ubora sana ikiweza kurekodi video za Full HD(1080p) na pia ina kamera ya mbele yenye 1.3MP.
- Inakuja katika aina mbili yenye 16GB na yenye 32GB,simu hii haina uwezo wa kuweka memory card.
- Ina NFC(Near Field ).
- Ina sensor za proximity,ambient light sensor na accelerometer.
- Battery yake ina uwezo wa 2300mAh,ni kiwango kizuri inaweza kukaa hadi masaa saba katika matumizi mazito. Inakubali pia Wireless Charging.
2.LG G2.
Kitu kimoja ninachopenda kuhusu smartphone hii ni uwezo wake wa hali ya juu wa kuweza kukaa na chaji kwa muda mrefu. Ina battery yenye uwezo mkubwa wa kutunza chaji. Pamoja na kwamba display yake imezidiwa kidogo na display ya Nexus 5,LG G2 ikiwa na 424ppi. Zote zinatumia display ya IPS LCD capacitive display.
- Ukubwa wa display yake ni inchi 5.2,ikiweza kuonesha Full HD katika 1080p.
- Display yake inalindwa Gorilla Glass 2,pamoja hiki kioo kiko nyuma ya Gorilla Glass 3 lakini kwa watu wengi wanalalamika kuhusu ubora wa Gorilla Glass 3,inaonekana kinaonesha michubuko sana kuliko Gorilla Glass 2.
- Nayo pia inatumia mawasiliano ya GSM ina 3G na pia 4G(LTE). Inatumia micro simcard.
- Mpaka sasa inatumia Android version ya Jelly Bean 4.2.2,hamna update zaidi lakini siku za mbeleni itaweza pata update ya Android 4.4 Kit Kat.
- Ina processor ya quadcore ikiwa na uwezo wa 2.26GHz na ikiwa na RAM yenye 2GB.
- Kamera yake ya nyuma ina 13MP ikiwa na LED flash na ikiweza kuchukua video za Full HD katika 1080p,na kamera ya mbele ina 2.1MP ikiweza nayo kuchukua picha na video za Full HD.
- Zinakuja zikiwa katika aina mbili,yenye internal memory ya 16GB na 32GB,zote zina RAM yenye uwezo wa 2GB.
- Ina NFC.
- Kitu kingine kizuri kuhusu simu hii ni kwamba unaweza kuitumia kama remote katika vifaa vya nyumbani ambavyo ni vya LG mfano TV,mashine ya kufulia na hata pia fridge.Kwa hiyo unaweza kuwa na remote moja tu kwa vifaa vyako vyote vya nyumbani(home appliances).
- Ina sensor za ambient light sensor,proximity na accelerometer.
- Ina battery yenye uwezo wa 3000mAh yenye kuweza kukaa muda mrefu sana.
3.Sony Xperia Z1.
Smartphone hii ni muendelezo wa smartphone ya Sony Xperia Z .Inajulikana pia kama Sony Xperia Honami. Sifa moja nzuri sana kuhusu hii smartphone ni kwamba inazuia maji kuingia ndani ya simu hii,unaweza kuizamisha katika maji kwa umbali wa mita 1 na ikakaa kwa muda wa nusu saa bila kuingia maji. Hii inafaa sana kwa wale wanaopenda kuogelea na pia inakuepusha na zile bahati mbaya za kuangusha simu katika maji.
- Inatumia display ya capacitive yenye pixel density ya 441ppi ikiwa ukubwa wa inchi 5,inaweza onesha Full HD katika 1080p.
- Kioo chake kinazuia michubuko na kuvunjika.
- Inazuia maji na uchafu kuingia katika simu.
- Inatumia mawasiliano ya GSM ikiwa na 3G na pia 4G(LTE).
- Inatumia Android 4.2.2 Jelly Bean,inaweza kuwa updated mpaka Android 4.4.2 Kit Kat.
- Ina kamera ya nyuma yenye 20.7MP na LED flash na ya mbele ina 2MP,Sony ni kampuni ambayo wanatengeneza smartphone zenye kamera ya ubora wa hali ya juu sana.Simu hii ina kamera nzuri mno.
- Ina processor ya quadcore(CPU nne) ikiwa na uwezo wa 2.26GHz na RAM yenye uwezo wa 2GB.
- Tofauti na smartphone hizo mbili zilizotangulia hii ina sehemu ya kukuwezesha kuweka memory card,na pia ina internal memory ya kiasi cha 16GB.
- Ina sensor zote kama zilizopo katika LG Google Nexus 5.
- Ina battery yenye uwezo wa 3000mAh.
No comments :
Post a Comment