Dec 31, 2013

Taswira ya mwaka 2013 katika teknolojia ya smartphones.

Mwaka 2013 ndiyo unaisha hivyo huku tukikaribisha mwaka mwingine wa 2014.Pamoja na kwamba tunategemea mengi sana katika mwaka ujao hasa katika nyanja ya teknolojia,nikilenga zaidi katika teknolojia ya smartphone.Kuna mengi sana ambayo yamejiri mwaka 2013.


KUPOROMOKA KWA MAKAMPUNI MAKUBWA YA TEKNOLOJIA.

Aliyekuwa CEO wa BlackBerry Bwana Thorsten Heins
Yaliyozoeleka kama makampuni makubwa ya teknolojia kwa miaka mingi iliyopita mfano BlackBerry na Nokia yamepata majanga makubwa katika biashara.BlackBerry kaporomoka kabisa kiasi cha kwamba mpaka ilifika hatua ya kuuza kampuni hiyo lakini uzuri ni kwamba mwisho wa siku uamuzi huo haukufikiwa na uamuzi mbadala ulikuwa ni kubadili uongozi,Bwana Thorsten Heins aliyekuwa CEO wa kampuni hiyo aliondolewa na baadhi ya viongozi wengine pia.Nafasi ya Thorstein imechukuliwa na CEO wa mpito anayeitwa Bwana John S. Chen,kampuni hii imepata hasara ya mamilioni ya dola.Nokia nae imembidi anunuliwe na Microsoft pamoja na kwamba wananchi wa Finland hawajapendelea hatua hii,huku ndipo nyumbani mwa kampuni ya Nokia.Nokia hana ujanja zaidi ya kukubali uamuzi huo,yote haya ni ili kulifanya kampuni liendelee kuwa hai na kuendelea na uzalishaji.


Achana na Google na Android yake,Apple mwaka huu kapeta kwelikweli.Amepata mapato ya kutosha.Tumeona kazindua iPhone 5S na iPhone 5C zote mbili zikija na operating system yao mpya iitwayo iOS 7,pamoja na kwamba iPhone 5C ilikuwa na lengo la kuwa iPhone ya bei nafuu lakini imevutia kiasi kidogo sana cha watu katika soko.Sio mbaya maana mauzo makubwa sana ya iPhone 5S yameifunika hasara ya mauzo ya iPhone 5C.Windows Phone zinajikongoja kwa kasi nzuri na kwa uhakika zitapeta mwakani,tumeona zikiwa maarufu zaidi ya iPhone katika baadhi ya sehemu za Ulaya.Apps nyingi maarufu katika Android na iOS sasa zinapatikana katika simu za Windows Phone 8 mfano Instagram na nyinginezo nyingi kama games za Angry Birds na kadhalika.


KUNUNULIWA KWA MAKAMPUNI YA TEKNOLOJIA.

Kuanzia kushoto.Aliyekuwa CEO wa Nokia,Stephen Elop na CEO wa Microsoft Steven Ballmer
Tukiachilia mbali Nokia kununuliwa na Microsoft,Google kanunua makampuni baadhi kama Waze,Makani Power na makampuni mengine yanahusika na kuunda roboti.Hii ina maana kwamba ununuzi huu una lengo kubwa hasa ambapo hivi karibuni Google wametangaza kuwekeza katika teknolojia ya roboti,haya yote tutayaona mwakani.


KITKAT SASA SIO CHOCOLATE TU,PIA NI VERSION YA OPERATING SYSTEM YA ANDROID.

Android amezindua operating system inayokwenda kwa jina la KitKat akitumia jina hilo toka katika bidhaa maarufu ya chocolate inayotengenezwa na kampuni ya Nestle.Android version hii imetoka huku lengo lake kuu likiwa ni kutumika katika simu nyingi sana za Android hadi zenye kiasi chenye RAM ya uwezo wa 512MB.
Logo rasmi ya Android 4.4 KitKat.


SMARTPHONES NA OPERATING SYSTEM MPYA ZACHIPUKA.

Jolla Phone ikitumia OS ya Sailfish.
Mnamo mwezi wa nne mwaka huu Firefox OS ilizinduliwa,OS hii nayo ni huru(Open source software) kama ilivyo Android na ikiwa katika msingi wa Linux(Kernel).Watengeneza OS hii ndiyo wanaomiliki browser maarufu ya mtandao inayojulikana kwa jina la Mozilla Firefox.Pia tumeona Samsung wameonesha baadhi ya smartphone zao zitazotumia OS ya Tizen.Sio hao tu,huko nchini Finland waliokuwa wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Nokia walikaa chini kwa pamoja na kuja na simu inayoitwa Jolla Phone ikitumia OS ya Sailfish ikiweza pia kukubali kutumia apps za Android.Hawa wote mwaka huu umekuwa wa mchipuko kwao,joto wataloleta katika soko litaonekana vizuri mwakani.





SMARTWATCH ZAONEKANA.

Samsung Galaxy Smartgear


Kimsingi,huu ulikuwa ni mwaka wa smartwatches.Lakini hatujaziona ziking'ara katika anga hizi za teknolojia kama watu wengi walivyotegemea.Hivi karibuni Samsung amezindua phablet ya Galaxy Note 3 ambayo inakuja na saa yake maalumu inayoitwa Smartgear.Unaweza kupiga picha,kusikiliza muziki na mambo mengine mengi katika saa hiyo huku ikiwa imeunganishwa na Galaxy Note 3 kwa njia ya Bluetooth.







Una lolote la kuchangia kuhusu yaliyojiri mwaka 2013 katika nyanja ya teknolojia ya smartphone?Usisite kutoa maoni yako hapo chini.

No comments :

Post a Comment