1.Whatsapp Messenger.

- Utambulisho wako ni namba yako ya simu.
- Inapatikana bure kwa mwaka mmoja na baada ya hapo utalipia kiasi cha $0.99.Lakini kwa watu wengi huwa inatokea mwaka ukiisha muda wa kutumia unaongezwa,Whatsapp wanafanya hivi kukwepa kukosa watumiaji wengi.
- Ni rahisi sana kutumia ukilinganisha na apps nyingine pinzani kama Viber ambapo unakuta mfano kutuma picha ni mchakato mrefu kidogo tofauti na Whatsapp.
- Unaweza kutuma SMS,picha,ujumbe wa sauti na video bila kikomo.
2.Google+ Hangouts.
App hii inakuwezesha kuwasiliana na marafiki wanaotumia Google+ lakini kwa sasa imeongezewa uwezo mwingine ambapo itakuwezesha kutuma SMS na MMS huku ukiendelea kuwasiliana na marafiki zako katika Google+. Ni app nzuri sana kwa sababu unafanya haya yote katika sehemu moja.
- Unaweza chat kwa njia ya video(Hangouts video chat),hii itahitaji uwe na kifurushi cha data kikubwa au uwe umejiunga na wireless internet(Wi-Fi) yenye kasi.
- Unaweza tuma picha.
- Na pia kwa kutumia MMS unaweza tuma picha,ujumbe wa sauti kwa mtu asiye na app hii. lakini ana simu yenye uwezo wa internet.
3.Facebook Messenger.
App hii inakuwezesha kuchat na marafiki zako wanaotumia mtandao wa Facebook,imeboreshwa sana katika Android na iOS.Unaweza kujua ni nani ambaye anatumia app hii na pia kuweza kumualika yule ambaye hana app hii aanze kuitumia.Inakuonesha pia wale marafiki ambao hawana app hii lakini wapo online kwa muda huo.
- Unatuma sms bila kikomo.
- Unaweza kutuma picha na ujumbe wa sauti(voicenote).
- Inakuwezesha kutext hata wale wasio marafiki zako katika Facebook lakini ni watumiaji wa mtandao huu.
- Inakuwezesha pia kuwasiliana kwa njia ya video(video calls)
No comments :
Post a Comment