Jan 10, 2014

Je!wewe ni mzazi na unataka kujua kila anachofanya mwanao katika smartphobe yake?hii hapa itatatua tatizo hilo.

Je!wewe ni mzazi na unataka kujua kila afanyacho mwanao katika smartphone yake?Basi nadhani simu hii itakufaa.


Kampuni inayojulikana kwa jina la Kurio wamezindua simu ambayo inaitwa Kids Phone.Unaweza kujua kila afachanyo mtu katika simu yake.

Unaweza kufahamu muda apps zinapofunguliwa na pia chochote kinachofanyika katika apps hizo,unaweza kuweka kikomo cha matumizi ya internet katika simu ya mwanao,pia unaweza kupata taarifa(notifications)  kuhusu mahali alipo na pia kupata taarifa pale anapovuka mipaka mfano mkoa mmoja kuelekea mwingine.

 Kampuni hii wana mfumo kabambe unaomuwezesha mzazi kuweza kuchagua mitandao ipi mwanae atembelee na vitu gani atavyoweza kudownload na kuangalia katika mtandao. Ili kuwezesha hili inatakiwa mzazi na mtoto wote wawe na smartphone hii. Simu zote hizi zinakuja zikiwa na display ya inchi 4 na yenye uwezo wa pixel density 213ppi(pixel per inch).Ina RAM yenye uwezo wa 1GB na huku ikitumia Android OS version ya Jelly Bean 4.2.2. Ina internal memory yenye ukubwa wa 8GB na unaweza kuweka memory card hadi yenye ukubwa wa 32GB.

Nadhani ukiamua kufanya utafiti mdogo tu. Ukachukua wazazi na watoto wao. Ukiwauliza wazazi wote wanaonaje kuhusu hii simu watasema "simu hii ni nzuri sana!itasaidia kwa kiwango cha hali ya juu wazazi kujua nini hasa wafanyacho watoto katika simu zao". Kwa upande wa watoto watasema"simu hii haina maana kabisa na kitu kama simu ni cha binafsi,haiwezi kumuhusu mtu yoyote ninachofanya katika simu yangu",hili ndilo litakuwa jibu la vijana wengi.Ni changamoto sana kwa kampuni hii.


































No comments :

Post a Comment