![]() |
Tab hii imekuwa designed na Google wenyewe na kutengenezwa na kampuni ya Asus. |
VIPIMO.
Ukilinganisha na Nexus 7(2012) kizazi cha kwanza,tab hii imepunguzwa unene na upana,lakini urefu ukiongezeka.Ni nyembamba sana ikiwa na milimita 8.7 za unene,ina milimita 114 za upana huku kizazi cha kwanza ikiwa na milimita 120 na katika urefu ina kiasi cha milimita 200 wakati kizazi cha kwanza ikiwa na milimita 198.5.
UZITO.
Ina uzito wa gramu 240,kizazi cha kwanza ina uzito wa gramu 340.Unaweza kuona ni jinsi gani imekuwa nyepesi katika kubeba.
KIOO.
Inatumia display ileile iliyotumika katika kizazi cha kwanza aina ya LED-backlit IPS LCD capacitive touchscreen,kioo kinacholinda display ni Gorilla Glass kinachozuia michubuko.
Naweza kusema mpaka sasa,hii ndo tablet ya Android yenye kioo kinachotoa muonekano mzuri kuliko tabs zote.Ina kiasi cha pixel density 323.Na display yake ina ukubwa wa nchi 7 ukipima katika mstari wa diagonal.Unaweza kugusa hadi vidole kumi kwa wakati mmoja katika touchscreen,hii inaifanya iwe bora kwa kucheza games.
KUMBUKUMBU.
Haina sehemu ya kuweka memory card,lakini ziko za aina mbili.Yenye uwezo wa 16GB na 32GB wa ukubwa wa kumbukumbu wa ndani(internal memory).
MAWASILIANO.
Zipo za aina mbili,yenye kutumia mawasiliano ya GSM,yenye 3G na 4G(LTE)(Hii unaweka line ya simu aina ya microsim) pamoja na Wi-Fi na ile yenye Wi-Fi tu.Ina Bluetooth,NFC na pia inakubali wireless charging.
KAMERA.
Ina kamera ya nyuma yenye megapixel 5,lakini haina flash.Kamera ya mbele ina megapixel 2 na hii inafaa kwa kupiga simu za video kwa kutumia Skype au Google Hangouts.Kamera zote hizi mbili zinaweza kuchukua video za ubora wa hali ya juu(HD).
OPERATING SYSTEM.
Tab hii ilipozinduliwa ilikuwa inakuja katika boksi ikiwa na Android Jelly Bean 4.3,lakini sasa unaweza ku-update tab hii mpaka Android 4.4.2 Kitkat ambayo ni version ya sasa ya Android OS.
![]() |
Inacheza games katika kiwango cha juu kabisa. |
PROCESSOR.
Ina processor yenye CPU nne(Quad-core processor) yenye spidi ya 1.5GHz huku kizazi cha kwanza ikiwa ni Quad-core pia lakini yenye spidi ya 1.2GHz.
SENSORS.
- Accelerometer-Kazi yake ni kuhisi nguvu ya uvutano wa dunia na kujigeuza kioo pale unapoilaza au kuisimamisha.
- Proximity-Kazi yake ni kuhisi mwili unapoisogelea karibu,kwa kutumia mionzi ya Infrared,pale utapoiweka sikioni au kusogeza mkono karibu basi display itajizima.Hii ni hasa unapoweka sikioni,sensor inahisi mwili na display inazima ili kuokoa chaji wakati wa kuongea na simu.
- Ambient Light Sensor-Kazi yake ni kuhisi mwanga,hii inasaidia kukupa uono mzuri wakati unatumia tab yako,mfano katika giza sensor hii huisi mwanga kidogo na kupunguza kiasi cha mwanga katika display ili usiumie macho.
- Gyrometer-Hii inapima kugeuka kwa simu au tab(orientation),inatumika hasa katika kucheza game mfano za magari.
Ina battery yenye uwezo wa 3950mAh,inakaa kwa muda wa masaa kumi katika matumizi ya mfululizo.Ni tab yenye kutunza chaji vizuri sana.
Ninadhani hili ni chaguo bora kwa kila mtu ambaye anafikiria ni tab ipi nzuri ya Android ya kununua,si ghali sana ukilinganisha na tab zingine kama iPad mini 2.
No comments :
Post a Comment