Showing posts with label ios. Show all posts
Showing posts with label ios. Show all posts

Apr 21, 2015

Mtazamo wangu kuhusiana na Apple Watch.

Mfuatiliaji yoyote wa teknolojia lazima atakuwa anaifahamu kampuni ya Apple. Umaarufu wake hautokani na kuwa na bidhaa lukuki sokoni kama zilivyo kampuni za Samsung na Sony. Apple anafahamika kwa mbunifu, kuleta bidhaa zilizo na utofauti, na kingine kikubwa kuliko vyote, "vifaa vya kielectroniki vya gharama" kwa kimombo wanasema "pricey products", Apple wenyewe huziita "premium products".

Samsung, mshindani mkubwa wa Apple. Jaribu kufikiria bidhaa zote za kielectroniki anazotengeneza na kisha linganisha na bidhaa za Apple. Unaweza cheka na kuona Apple wako nyuma sana, wana modeli chache za iPhones, iPad na hata kompyuta za Macbook. Lakini na uchache wote huo wa bidhaa( product line) wanazotengeneza lakini ndiyo kampuni yenye thamani kuliko zote duniani. Kampuni hii nailinganisha na kampuni ya Exxon Mobil ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikishikilia nafasi ambayo Apple anaishikilia kwa sasa, Exxon Mobil ina mafanikio makubwa sana kwa sababu wanabaki katika msimamo mmoja wa kuangalia ni wapi zaidi wapo imara na wanaweza pafanyia kazi na kupata faida kubwa, ndivyo hata Apple hufanya. 

Mwishoni mwaka jana Apple alitangaza bidhaa mpya inayofahamika kama "Apple Watch", hii ni smartwatch kama zilivyo LG Watch Urbane, Samsung Galaxy Gear na kadhalika. Apple amechelewa katika upande wa smartwatches na Apple Watch haionyeshi dalili zozote za kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa smartwatches wa sasa kama alivyofanya mwaka 2007 katika teknolojia ya smartphones.

Apple Watch

Mar 1, 2015

Vidokezo(tips) muhimu katika matumizi ya smartphone ya kila siku.

Katika nyakati hizi za kidigitali, smartphone ni kifaa cha kielectroniki muhimu sana katika maisha ya kila siku. Inakuwezesha kuwasiliana na watu wengine duniani katika njia mbalimbali, hukuwezesha kupata huduma za mtandao(internet) katika kasi kubwa, hukuburudisha na muziki wa hali ya juu na pia kukuwezesha kupiga picha na kuweka kumbukumbu ya matukio muhimu katika maisha yako, si hivyo tu... Unaweza kufanya kazi zako muhimu katika device yako popote pale unapokwenda. Kuna baadhi ya vitu watumiaji wengi wa smartphones hawavifahamu na kwa uhakika hurahisisha matumizi yako ya smartphone kwa kuyafanya kuwa fanisi zaidi. Vidokezo hivi muhimu vitakusaidia katika matumizi yako ya smartphone na kukufanya kufurahia smartphone yako zaidi na zaidi.

Jan 20, 2015

Ubaya wa Android OS.

Wengi wetu tunapenda kutumia devices za Android. Hii inatokana na mambo mengi, mfano urahisi katika kuitumia, unafuu wa bei za devices za Android na mambo mengine mengi. Lakini pamoja na faida tele zilizopo katika matumizi ya Android OS, bado kuna vitu ambavyo ni tatizo na pengine vinapelekea baadhi ya watu kutumia devices zilizo na operating system nyingine, mfano mzuri iOS.

Nexus 7(2013), tablet ya Google iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Asus.

Sep 10, 2014

Most of us are dissapointed.

"Wengi wetu tumesikitishwa", hivyo ndivyo kichwa cha habari kinavyosema. Siku chache zilizopita niliandika makala kuhusu ni vipi na kwanini iPhone 6 itaweza badili muonekano wa teknolojia ya smartphone. Bahati mbaya sana hili limekuwa tofauti, vitu vingi tulivyotegemea kuviona katika simu hizi mbili za iPhone 6 hatujaviona! iPhone 6 4.7 inch inakatisha tamaa kabisa, battery yake ni karibia na ileile iliyopo katika iPhone 5S. Pixel density ni ile ile ya iPhone 5S hadi iPhone 4, hakuna tofauti kubwa sana katika smartphone hii zaidi ya kuwa na display ya ukubwa wa 4.7inch, processor yenye uwezo zaidi na mengine baadhi. Hakuna display ya Sapphire katika model zote mbili, wametumia Gorilla Glass ambayo wanatumia tangu kuanzishwa kwa iPhone. Labda kwa iPhone 6 plus, angalau kuna vitu vya kuvutia. Display yake ni Full High Definition(HD), 1080p resolution. Camera ina Optical Image Stabilisation(OIS) na pixel density yake ina kiasi cha 401ppi(pixel density per inch). Uwezo wake wa battery ni mkubwa kuliko iPhone 6 4.7 inch.



Sep 4, 2014

iPhone 6! pengine itakuwa smartphone bora kuwahi kutengenezwa katika historia.

Ni takribani miaka 16 tangu neno "smartphone" kuanza kutumika, aina hii ya simu ina historia ndefu sana ambapo inarudi hadi miaka ya 1970. Umaarufu wake haswa umekuja mnamo mwaka 1998 ambapo kampuni ya Ericsson ilizindua simu inayoitwa Penelope na hapo ndipo neno smartphone likachipuka. Simu hii ilikuwa na uwezo ambao pengine unaweza kusema ni sawa na ule wa kompyuta. Baada ya hapo makampuni mengine mengi nayo yalianza kutengeneza smartphones, mfano BlackBerry, Nokia, Palm, Dell, HP na kadhalika. Miaka imesonga na tumeona mabadiliko mengi sana katika fani hii ya teknolojia, makampuni yanayotengeneza smartphones ni mengi sana kwa sasa, Operating Systems za simu hizi nazo zipo nyingi, watumiaji wa simu hizi nao wanaongezeka kila siku. Karibia kila mtu anamiliki simu hii.
iPhone 6 upande wa kulia ikiwa na iPhone 5S.