Mar 1, 2015

Vidokezo(tips) muhimu katika matumizi ya smartphone ya kila siku.

Katika nyakati hizi za kidigitali, smartphone ni kifaa cha kielectroniki muhimu sana katika maisha ya kila siku. Inakuwezesha kuwasiliana na watu wengine duniani katika njia mbalimbali, hukuwezesha kupata huduma za mtandao(internet) katika kasi kubwa, hukuburudisha na muziki wa hali ya juu na pia kukuwezesha kupiga picha na kuweka kumbukumbu ya matukio muhimu katika maisha yako, si hivyo tu... Unaweza kufanya kazi zako muhimu katika device yako popote pale unapokwenda. Kuna baadhi ya vitu watumiaji wengi wa smartphones hawavifahamu na kwa uhakika hurahisisha matumizi yako ya smartphone kwa kuyafanya kuwa fanisi zaidi. Vidokezo hivi muhimu vitakusaidia katika matumizi yako ya smartphone na kukufanya kufurahia smartphone yako zaidi na zaidi.




1. Namna ya kukumbuka namba ya mwisho kupiga muda mfupi uliopita.


Pengine kuna namba ya simu uliyopiga muda mfupi uliopita na inatokea kwamba namba hiyo haipo katika phonebook yako. Huna haja ya kuanza kuitafuta mahali pengine popote. Ingia katika menu ya simu halafu chagua phone baada ya hapo bonyeza dialpad baada ya hapo bonyeza sehemu ya kupiga simu(mara nyingi huwa katika rangi ya kijani) namba ya mwisho kabisa uliyopiga katika simu yako itajionyesha.
Bonyeza kitufe cha kupiga mara moja tu. 


2. Namna ya kuweka kituo(fullstop) unapoandika SMS au maandishi yoyote.

Huna haja ya kuweka kituo kila mara unapomaliza kuandika sentensi. Hupoteza muda sana hasa pale unapoandika barua pepe(e-mail) ndefu au sms ndefu. Unapofika mwisho wa sentensi yako, badala ya kubonyeza sehemu iliyo na kituo(fullstop) bonyeza kitufe cha kuweka nafasi(space keypad) mara mbili tu kwa mfululizo. Itaweka kituo na kuacha nafasi moja kwa kuanza sentensi mpya, huna haja ya kuweka herufi kubwa, anza sentensi mpya na herufi ya kwanza itakuwa kubwa(capital letter) yenyewe(automatically).

Bonyeza space mara mbili mfululizo. 


3. Namna ya kuanza na herufi kubwa katika sentensi. 

Inaweza tokea kwamba umeweka kituo(fullstop) mwenyewe(manually) na haujatumia njia niliyoelekeza hapo juu. Huna haja ya kubonyeza sehemu ya kuweka herufi kubwa ili kukuwezesha kuanza sentensi mpya ikiwa na herufi kubwa. Bonyeza kitufe cha kuweka nafasi(spacebar) mara moja na kisha anza kuandika sentensi yako, herufi ya kwanza itakuwa kubwa(capital letter yenyewe(automatically).

Bonyeza sehemu ya kuweka nafasi(spacebar) na kisha anza sentensi mpya.


4. Namna ya kurekebisha neno pale unapokosea.

Unapotype, maneno yote unayokosea hupigiwa mstari mwekundu kukufahamisha kwamba hayapo sawa. Huna haja ya kukumbuka sana jinsi yanavyoandikwa kwa usahihi. Bonyeza neno husika ulilokosea, yataokea maoni(suggestions) yakionyesha usahihi wa neno hilo. Chagua unalohitaji na neno hilo litajisahihisha papo hapo.

Chagua neno linalofaa kusahihisha kulingana na unachoandika. 


5. Namna ya kuifanya keyboard yako kujifunza maneno. 

Kwa mfano unachagua keyboard inayotambua(support) maneno ya Kiingereza tu, pengine English(UK). Kila utapoandika neno la Kiswahili au lugha nyingine yoyote, neno hilo litapigiwa mstari mwekundu hata kama lipo sahihi, hii ni kutokana na keyboard husika kutotambua lugha hiyo. Ili kuifanya keyboard yako kujifunza maneno hayo pale unapoandika neno la lugha nyingine na una uhakika neno hilo lipo sahihi, libonyeze neno husika na kisha chagua "add to dictionary". Muda mwingine utapotype neno hilo halitaonyesha kukosewa kwa sababu tayari lipo katika kamusi(dictionary) ya simu yako.

Utachagua "add to dictionary" neno husika halitaonekana kama limekosewa mara nyingine utapoliandika. 


Vidokezo(tips) hivi vipo karibia katika mobile operating systems zote. Muonekano waweza kuwa tofauti lakini namna ya ufanyaji kazi wa vidokezo hivi unafanana. 

No comments :

Post a Comment