Jan 20, 2015

Ubaya wa Android OS.

Wengi wetu tunapenda kutumia devices za Android. Hii inatokana na mambo mengi, mfano urahisi katika kuitumia, unafuu wa bei za devices za Android na mambo mengine mengi. Lakini pamoja na faida tele zilizopo katika matumizi ya Android OS, bado kuna vitu ambavyo ni tatizo na pengine vinapelekea baadhi ya watu kutumia devices zilizo na operating system nyingine, mfano mzuri iOS.

Nexus 7(2013), tablet ya Google iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Asus.

Android Fragmentation, moja ya tatizo kubwa sana katika Android OS. Huleta usumbufu kwa developers wa applications za Android hadi watumiaji wa apps hizo. Android Fragmentation hutokea pale software inaposhindwa kufanya kazi au kufanyiwa installation katika device husika. Hali hii hupelekea baadhi ya smartphones kushindwa kupata latest version za Android OS kutokana na kuwa na hardware(chipset) ambayo haina uwezo wa kusupport software hiyo. Smartphones nyingi ambazo huathirika na tatizo hili ni zile hali ya chini(low end smartphones) na zilizo za hali ya katikati(mid-range smartphones), na yote ni kwa sababu software updates nyingi za Android huitaji devices zilizo na hardware za kisasa zaidi. Ukitazama kwa update ya Android KitKat, ni smartphones chache sana zilizoweza kupata software update hii, smartphone nyingi zimeishia katika Android Jellybean 4.3 na hazitapata software update yoyote siku za mbeleni. 

Katika upande wa developers, huwabidi kubadili version ya apps zao kila software update ya Android inapotoka., pasipo kufanya hivyo apps zao hazitaweza fanya kazi katika latest software update husika. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa ngazi(level) ya mfumo unaofahamika kama API(Application Programming Interface), ambapo kila Android version ina mfumo tofauti wa API. Developer asiposupport mfumo huo, app yake haitaweza kufanya kazi katika software update husika. Kuna apps ambazo husupport API za Android version za juu tu, hii ina maana wale watumiaji wa Android version za chini hawataweza kutumia apps hizi. Mfano, miaka ya nyuma app maarufu ya Instagram ilikuwa ikipatikana katika Android Jellybean 4.0 na kuendelea, hii ilipelekea watumiaji wa Android Froyo(2.2), Android Gingerbread(2.3) na Android Honeycomb(3.0) kutoweza tumia app hii. Muda baadaye Instagram walianza kusupport API za version hizo zote tatu, na ndo mpaka leo unaweza kuona Instagram inasupport hadi simu zitumiazo Android Froyo(2.2), ambayo ni version ya kizamani sana kwa sasa.

Kwa ujumla, Android Fragmentation hufanya smartphones nyingi kukosa software updates zaidi baada ya kipindi kifupi tu. Hii inakubidi kununua smartphone nyingine inayoweza support software update ya juu iliyo na latest hardwares. Tofauti na iPhones, zitumiazo operating system ya iOS. Katika iOS, device zote hupata software update kwa pamoja. Hakuna inayoweza kukosa update kwa sababu ya tatizo la hardware. Ukiangalia update iOS 8, smartphones zote za Apple zimepata update, kasoro iPhone 4 ambayo iko ipo discontinued. Kwa upande wa Android, Lollipop 5.0 inaonekana kupatikana katika smartphones ambazo ni flagships tu, kwa zile za kawaida ni baadhi tu zitaweza kupata update hii, na si ajabu hata zile zilizo na sifa ya kuwa na hardware zilizo latest nazo kukosa update ya Lollipop 5.0. 

Katika smartphones zote zilizopo mpaka sasa, asilimia 80% ya malwares(malicious softwares) au kwa jina lililozelekea "virus" hushambulia smartphones zitumiazo operating system ya Android. Pamoja na kwamba iOS nayo hushambuliwa na malware lakini ni mpaka pale utapofanya mchakato unaofahamika kama jailbreaking, sawa na kufanya rooting katika Android OS. Kwa iPhones ambazo hazipo jailbroken, zipo salama. Kushambuliwa huku na malware kwa Android huitaji kufanya factory reset ya smartphone mara kwa mara ili kuondoa matatizo haya, na pia ujue ya kwamba app yoyote unayodownload katika smartphone yako ya Android itayokuahidi kulinda simu yako kutokana virusi, haina msaada wowote pale unapopata shambulio. 

Nadhani inatakiwa kufika wakati ambapo Google(ambae ni mmiliki wa Android OS), watengeneza smartphones(mfano. Samsung, HTC), watengeneza processors na chipset(mfano. Qualcomm, MediaTek) na watengeneza third party apps(mfano Whatsapp, Instagram) kukaa pamoja na kuelewana ili kuweza kufanya tatizo hili kupatiwa ufumbuzi kwa kuwepo utaratibu mzuri, wanachofanya kwa sasa ni kila mmoja kumtupia lawama mwenzake katika kusababisha tatizo hili. Mwisho wa siku, wasumbukao ni watumaji. 

No comments :

Post a Comment