Apr 21, 2015

Mtazamo wangu kuhusiana na Apple Watch.

Mfuatiliaji yoyote wa teknolojia lazima atakuwa anaifahamu kampuni ya Apple. Umaarufu wake hautokani na kuwa na bidhaa lukuki sokoni kama zilivyo kampuni za Samsung na Sony. Apple anafahamika kwa mbunifu, kuleta bidhaa zilizo na utofauti, na kingine kikubwa kuliko vyote, "vifaa vya kielectroniki vya gharama" kwa kimombo wanasema "pricey products", Apple wenyewe huziita "premium products".

Samsung, mshindani mkubwa wa Apple. Jaribu kufikiria bidhaa zote za kielectroniki anazotengeneza na kisha linganisha na bidhaa za Apple. Unaweza cheka na kuona Apple wako nyuma sana, wana modeli chache za iPhones, iPad na hata kompyuta za Macbook. Lakini na uchache wote huo wa bidhaa( product line) wanazotengeneza lakini ndiyo kampuni yenye thamani kuliko zote duniani. Kampuni hii nailinganisha na kampuni ya Exxon Mobil ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikishikilia nafasi ambayo Apple anaishikilia kwa sasa, Exxon Mobil ina mafanikio makubwa sana kwa sababu wanabaki katika msimamo mmoja wa kuangalia ni wapi zaidi wapo imara na wanaweza pafanyia kazi na kupata faida kubwa, ndivyo hata Apple hufanya. 

Mwishoni mwaka jana Apple alitangaza bidhaa mpya inayofahamika kama "Apple Watch", hii ni smartwatch kama zilivyo LG Watch Urbane, Samsung Galaxy Gear na kadhalika. Apple amechelewa katika upande wa smartwatches na Apple Watch haionyeshi dalili zozote za kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa smartwatches wa sasa kama alivyofanya mwaka 2007 katika teknolojia ya smartphones.

Apple Watch


Apple Watch inatakiwa kuleta mapinduzi ya kiteknolojia katika nyanja ya smartwatches, kila baada ya masaa 18 unahitaji kuichaji Apple Watch yako kama utahitaji kuendelea kuitumia, huwezi kuunganisha Apple Watch katika device yoyote zaidi ya iDevice, user interface yake(UI) inahitaji marekebisho mengi sana ili kuweza kuleta urahisi katika matumizi yake na bila kusahau kubwa zaidi, smartwatch hii ni gharama sana. Bei yake inaanzia dola za kimarekani $350(Takribani Tsh. 630,000) hadi $17,000(Takribani Tsh. milioni 30)(iliyo na madini ya dhahabu katika umbo lake). Ukiangalia suala la bei na mambo mengine niliyotaja mapema inadhihirisha wazi Apple Watch haitakuwa na msukumo mkubwa sokoni. Katika upande wa sifa za kiteknolojia, haina chochote kilicho kipya chenye mvuto!

Unaweza hairisha kununua gari na badala yake ukanunua Apple Watch!

Lakini, kuna suala moja kubwa litalopelekea smartwatch hii kuwa na mauzo makubwa sana. Si teknolojia iliyotumika kuiunda bali "fasheni yake". Apple Watch si kifaa cha kielectroniki kwa wale wanaopenda teknolojia bali ni "alama ya mitindo(fashion icon)", kwa wale wanaopendelea mitindo(fashion).

Unapoangalia kwa umakini, smartwatch nyingi mfano za Samsung, LG na Motorola, msisitizo mkubwa walioweka ni katika kuifanya teknolojia ya smartwatch husika kuwa bora zaidi. Ndiyo maana hapo mwanzo watu wa mitindo hawakuona umaana wa smartwatch hizi, wanunuzi wakubwa ni watu wanaopendelea na kuifahamu teknolojia(tech enthusiasts), kampuni nilizotaja hapo juu na nyinginezo zinapata shida katika kuwafanya watu wa mitindo kufikiria kutumia smartwatch zao, na ndiyo maana unaona smartwatch za sasa hivi zitumiazo Android OS zipo katika mfumo wa kuvutia watu wanaojali mitindo pia, mfano mzuri LG Watch Urbane.

Apple hajapuuzia kabisa suala la mitindo, na ndilo kipaumbele katika Apple Watch. Ameshirikiana na kampuni ya Burberry kwa ajili ya kubuni muonekano mzima wa nje wa Apple Watch. Burberry ni kampuni ya Uingereza iliyo na umaarufu mkubwa sana duniani kutokana na bidhaa zake za nguo, saa, mikoba na kadhalika. Apple Watch itawavutia wale wengi wanaopendelea bidhaa za Burberry na wanaopendelea mitindo kwa ujumla. Kim Kardashian hatoacha kununua Apple Watch! Hatohangaika kwenda kuweka madini ya dhahabu katika Apple Watch kama ambavyo hufanya kwa iPhones zake, hii ni kwa sababu lipo toleo la dhahabu(gold edition), na kwa hakika kuna wakina Kim Kardashian wengi tu duniani ambao $17,000(Tsh. milioni 30) si kitu na watanunua Apple Watch mara moja, hata kama watashindwa pata hela hiyo basi edition ya $350(Tsh. 630,000) isiwapite pia.

Hapo ndipo utapoona mauzo ya Apple Watch yanapanda kwa kasi. Si kwa sababu ya teknolojia bali FASHION. Kama nilivyosema mapema "Apple siku zote hutaka kuwa tofauti na wengine, na sasa tofauti umeiona". Apple Watch itazinduliwa rasmi mnamo tarehe 24 mwezi huu. Usisite kutoa maoni yako kupitia Google Plus kuhusu Apple Watch.

No comments :

Post a Comment