Showing posts with label ios. Show all posts
Showing posts with label ios. Show all posts

Apr 21, 2015

Mtazamo wangu kuhusiana na Apple Watch.

Mfuatiliaji yoyote wa teknolojia lazima atakuwa anaifahamu kampuni ya Apple. Umaarufu wake hautokani na kuwa na bidhaa lukuki sokoni kama zilivyo kampuni za Samsung na Sony. Apple anafahamika kwa mbunifu, kuleta bidhaa zilizo na utofauti, na kingine kikubwa kuliko vyote, "vifaa vya kielectroniki vya gharama" kwa kimombo wanasema "pricey products", Apple wenyewe huziita "premium products".

Samsung, mshindani mkubwa wa Apple. Jaribu kufikiria bidhaa zote za kielectroniki anazotengeneza na kisha linganisha na bidhaa za Apple. Unaweza cheka na kuona Apple wako nyuma sana, wana modeli chache za iPhones, iPad na hata kompyuta za Macbook. Lakini na uchache wote huo wa bidhaa( product line) wanazotengeneza lakini ndiyo kampuni yenye thamani kuliko zote duniani. Kampuni hii nailinganisha na kampuni ya Exxon Mobil ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikishikilia nafasi ambayo Apple anaishikilia kwa sasa, Exxon Mobil ina mafanikio makubwa sana kwa sababu wanabaki katika msimamo mmoja wa kuangalia ni wapi zaidi wapo imara na wanaweza pafanyia kazi na kupata faida kubwa, ndivyo hata Apple hufanya. 

Mwishoni mwaka jana Apple alitangaza bidhaa mpya inayofahamika kama "Apple Watch", hii ni smartwatch kama zilivyo LG Watch Urbane, Samsung Galaxy Gear na kadhalika. Apple amechelewa katika upande wa smartwatches na Apple Watch haionyeshi dalili zozote za kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa smartwatches wa sasa kama alivyofanya mwaka 2007 katika teknolojia ya smartphones.

Apple Watch

Mar 1, 2015

Vidokezo(tips) muhimu katika matumizi ya smartphone ya kila siku.

Katika nyakati hizi za kidigitali, smartphone ni kifaa cha kielectroniki muhimu sana katika maisha ya kila siku. Inakuwezesha kuwasiliana na watu wengine duniani katika njia mbalimbali, hukuwezesha kupata huduma za mtandao(internet) katika kasi kubwa, hukuburudisha na muziki wa hali ya juu na pia kukuwezesha kupiga picha na kuweka kumbukumbu ya matukio muhimu katika maisha yako, si hivyo tu... Unaweza kufanya kazi zako muhimu katika device yako popote pale unapokwenda. Kuna baadhi ya vitu watumiaji wengi wa smartphones hawavifahamu na kwa uhakika hurahisisha matumizi yako ya smartphone kwa kuyafanya kuwa fanisi zaidi. Vidokezo hivi muhimu vitakusaidia katika matumizi yako ya smartphone na kukufanya kufurahia smartphone yako zaidi na zaidi.

Jan 20, 2015

Ubaya wa Android OS.

Wengi wetu tunapenda kutumia devices za Android. Hii inatokana na mambo mengi, mfano urahisi katika kuitumia, unafuu wa bei za devices za Android na mambo mengine mengi. Lakini pamoja na faida tele zilizopo katika matumizi ya Android OS, bado kuna vitu ambavyo ni tatizo na pengine vinapelekea baadhi ya watu kutumia devices zilizo na operating system nyingine, mfano mzuri iOS.

Nexus 7(2013), tablet ya Google iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Asus.

Sep 10, 2014

Most of us are dissapointed.

"Wengi wetu tumesikitishwa", hivyo ndivyo kichwa cha habari kinavyosema. Siku chache zilizopita niliandika makala kuhusu ni vipi na kwanini iPhone 6 itaweza badili muonekano wa teknolojia ya smartphone. Bahati mbaya sana hili limekuwa tofauti, vitu vingi tulivyotegemea kuviona katika simu hizi mbili za iPhone 6 hatujaviona! iPhone 6 4.7 inch inakatisha tamaa kabisa, battery yake ni karibia na ileile iliyopo katika iPhone 5S. Pixel density ni ile ile ya iPhone 5S hadi iPhone 4, hakuna tofauti kubwa sana katika smartphone hii zaidi ya kuwa na display ya ukubwa wa 4.7inch, processor yenye uwezo zaidi na mengine baadhi. Hakuna display ya Sapphire katika model zote mbili, wametumia Gorilla Glass ambayo wanatumia tangu kuanzishwa kwa iPhone. Labda kwa iPhone 6 plus, angalau kuna vitu vya kuvutia. Display yake ni Full High Definition(HD), 1080p resolution. Camera ina Optical Image Stabilisation(OIS) na pixel density yake ina kiasi cha 401ppi(pixel density per inch). Uwezo wake wa battery ni mkubwa kuliko iPhone 6 4.7 inch.



Sep 4, 2014

iPhone 6! pengine itakuwa smartphone bora kuwahi kutengenezwa katika historia.

Ni takribani miaka 16 tangu neno "smartphone" kuanza kutumika, aina hii ya simu ina historia ndefu sana ambapo inarudi hadi miaka ya 1970. Umaarufu wake haswa umekuja mnamo mwaka 1998 ambapo kampuni ya Ericsson ilizindua simu inayoitwa Penelope na hapo ndipo neno smartphone likachipuka. Simu hii ilikuwa na uwezo ambao pengine unaweza kusema ni sawa na ule wa kompyuta. Baada ya hapo makampuni mengine mengi nayo yalianza kutengeneza smartphones, mfano BlackBerry, Nokia, Palm, Dell, HP na kadhalika. Miaka imesonga na tumeona mabadiliko mengi sana katika fani hii ya teknolojia, makampuni yanayotengeneza smartphones ni mengi sana kwa sasa, Operating Systems za simu hizi nazo zipo nyingi, watumiaji wa simu hizi nao wanaongezeka kila siku. Karibia kila mtu anamiliki simu hii.
iPhone 6 upande wa kulia ikiwa na iPhone 5S.

Nov 11, 2013

BBM katika Android inazidi kuwa na mafanikio.

Huenda kutumia smartphone ya BlackBerry kwa sasa kusiwe issue,lakini kutumia BBM kwenye Android na iOS ndiyo ikawa kitu maana au kwa lugha mtaani "habari ya mjini".

Tangu BBM imetoka kwenye Android imeweza kuwa downloaded zaidi ya mara milioni 20.Mwanzoni wengi walikuwa wakidownload app hii na baada ya muda mfupi kuifuta lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda hali ikabadilika,wengi wakawa wanadownload na kuitumia,tena kwa muda mwingi wa siku.


BBM inaweza ikafanya vizuri zaidi na zaidi kama pia itawekwa katika simu za Windows Phone.Lakini hili muda wake ni bado sana.Pamoja na watumiaji wengi wa Android kutumia app hii lakini bado kuna baadhi ambazo wana OS version za Android 2.3(Gingerbread) na Android 2.2(Frozen Yoghurt au Froyo) hawapati app hii kutokana na kwamba mpaka sasa inakubali katika simu zenye Android 4.0(Ice Cream Sandwich) na kuendelea.



Oct 22, 2013

Utoaji wa app ya BBM kwenye Android na iOS umerudi tena.

Jana asubuhi kampuni ya BlackBerry ilitangaza kwamba inaanza kutoa tena app ya BBM kama ilivyoahidi wiki kama nne zilizopita baada ya kuwa na tatizo katika uzinduzi wake lililopelekea kusimamishwa kwa kuendelea kutoa app hii,hali hii ilitokana na watu wengi kuwa na app feki kitu kilichopelekea msongamamo wa mawasiliano kwenye server ya BlackBerry.


Kwa sasa wataoweza kutumia app hii ni wale waliojisajili mapema kwenye tovuti ya bbm.com,wale ambao wamechelewa kujisajili itabidi wasubiri mpaka watapotumiwa email ya kukubaliwa kutumia app hii.

Kwa sasa inapatikana katika Android katika simu za Samsung Galaxy zinazorun Android 4.0 na kuendelea katika store ya Samsung apps.

 Kama tayari umeanza tumia app hii kwenye Android au iOS,share nasi unaionaje.


Jun 13, 2013

Ni kweli iOS 7 italeta mabadiliko makubwa katika historia ya simu za iPhone.

Siku chache zilizopita kampuni ya vifaa vya kielectroniki ya Apple ilizindua Operating System yao mpya inayoitwa iOS 7.Operating System hii imebadili sana muonekano wa sasa wa Operating System zinazotumika katika simu za Apple na maboresho mengi yamefanyika.
UTATA
Toka baadhi ya picha na video za jinsi gani hii Operating System  ilivyo kuonekana watu wengi wameifananisha na Windows Phone 8 katika muonekano wake wa kuonesha running apps,huko Hongkong,China Nokia walipost katika internet picha ikonesha running apps katika simu ta Windows Phone 8 na katika iOS 7 lakini watu wengi walishindwa kutofautisha ipi ni iOS 7 na ipi ni Windows Phone 8.
Lakini hii ni kawaida kwa makampuni kuigana,sababu hata Apple pia wameiga katika Operating System kongwe ya WebOS,kwa hiyo si sahihi sana kusema "copy n paste" bali ni inspiration.
Kwa kuangalia video ya muonekano wa iOS 7 angalia hapa https://www.youtube.com/watch?v=rT_OmTMwvZI&feature=youtube_gdata_player

Jun 5, 2013

BBM inakuja katika Android na iOS tarehe 26 mwezi huu.

BlackBerry wamepost katika akaunti yao ya twitter kwamba application yao maarufu ya kijamii iitwayo BlackBerry Messenger inakuja katika simu za Android na iOS.Nadhani watumiaji wengi wa Android watafurahishwa sana na hiki kitu.Jiandae kupokea BBM.

May 26, 2013

Sababu kumi zinazoweza sababisha Android kumuua iOS.

1.ANDROID INAPATIKANA KATIKA SIMU ZAIDI YA MOJA-kama ni mtumiaji wa Android unakuwa na machaguo mengi ya makampuni yanayotengeneza simu za Android unaweza tumia Samsung,LG,Alcatel,Sony na nyinginezo nyingi lakini ni tofauti na iOS ambapo inapatikana katika simu moja tu ya iPhone wanayotengeneza wenyewe,kwa hili  unajikuta una mipaka ya kuchagua brands.

 2.APPLE WANATENGENEZA SIMU ZA GHARAMA TU(high-end devices)-Kama unapenda simu ya Apple na unataka simu ya bei nafuu huwezi kupata sababu zote ni simu za gharama.Tofauti na Android ambapo kuna smartphones za bei nafuu hadi laki moja.

 3.ANDROID KUIBADILI MUONEKANO WAKE KADIRI UNAVYOTAKA(Customisation)-Unaweza kubadili muonekano wa Android kirahisi,mfano.kuweka custom rom ambapo huwezi fanya hiki kitu katika simu za iPhone.

4.GOOGLE PLAYSTORE YA ANDROID INA APP NYINGI NZURI ZA BURE TOFAUTI NA APP STORE YA iOS-Unapata application nyingi sana nzuri katika Android bure tofauti na iOS ambapo apps nyingi nzuri ni za kulipia.

5.ANDROID INA MUONEKANO MZURI NA FEATURES NYINGI KWA APPS ZINAZOTENGENEZWA NA GOOGLE KAMA GOOGLE+,GOOGLE MAP,YOUTUBE,GMAIL NA NYINGINEZO.
6.WIDGETS-hivi ni vidirisha vidogo ambavyo huonesha application inavyoendelea kwa kukupa updates ambapo vinapatikana katika Android na iOS hana feature kama hii.

7.iPHONE HAZINA SEHEMU YA KUWEKEA MEMORY CARD-Simu za Apple iPhone hazina sehemu ya kuwekea memory card(sd card slot) ambapo simu nyingi za Android zina card slot kwa hiyo inakuwa rahisi kuonegeza ukubwa ukubwa wa memory.

 8.NI RAHISI KUSHARE DATA KATIKA ANDROID- Kwa kutumia NFC na Android Beam ni rahisi kuhamisha data kutoka device moja kwenda nyingine kwa kubonyeza mara moja.

 9.ANDROID NI RAHISI KUTUMIA-Kwa mtu ambaye hajawahi kutumia smartphone kabla na hata mtumiaji mwingine ataona kuna ugumu katika kutumia iPhone kuliko kutumia Android.

 10.ANDROID INAKU HARAKA KULIKO iOS-Kila siku watumiaji wengi wapya wananunua simu za Android kuliko iOS.

May 21, 2013

Windows Phone inakua haraka kuliko Android na iOS,imesema ripoti ya hivi karibuni.


Katika miezi ya karibuni tumeona msukumo mkubwa sana kwa Windows Phone.Ripoti iliyotolewa na Kantar World Panel imeonesha ukuaji katika miezi mitatu iliyopita.Windows Phone imekua kwa 1.5% kutoka Februari mpaka Machi,iOS imekua kwa 0.2% na Android imeporomoka kwa 1.9%.Kuanzia mwaka jana muda kama huu Windows Phone imekua kwa 3.7%.Nokia pekee imekua kwa asilimia kutoka 1% mpaka 4% katika hisa sokoni katika mwaka mmoja.


Sababu ya ukuaji huu imetokana na watuniaji wa simu zisizo smartphones(feature phones).52% ya wale waliohamia kutumia Windows Phone walikuwa watumiaji wa simu za kawaida(feature phones).Hicho ni kiasi kikubwa zaidi ya watumiaji wa Android na iOS.Inamaanisha watu ambao hawajawahi kutumia smartphones walivutiwa na kutumia simu za Windows.Hiki ni kitu kizuri na kwa sasa inashikilia na nafasi ya tatu baada ya Android na iOS.

May 14, 2013

BlackBerry Messenger(BBM) inakuja katika android na iOS

Kampuni ya kutengeneza smartphone ya Research In Motion inayotengeneza simu aina ya blackberry imeamua kuifanya software yake maarufu kama BBM kuwa cross-platform application(yaani inayopatikana katika OS zaidi ya moja) kama zilivyo social apps nyingine kama Viber na Whatsapp. BBM imekuwa moja katika ya application maarufu sana katika simu za BlackBerry,CEO wa RIM Mr. Thorstein Heins ametangaza katika kiangazi kinachokuja kwa majira ya marekani BlackBerry messanging itapatikana kama thrid party app katika mobile operating system maarufu kama iOS na android.Kwa sasa,BBM ina features kama chats,kutumiana picha,sauti na video na vinginevyo. Thorstein amesema itakuja na maboresho makubwa kama video calling,kushare screen na vinginevyo ambavyo kwa sasa vinapatikana katika operating system ya bb10 ambayo inapatikana katika simu kama blackberry z10 na q10.Itapatikana katika ios zinazotumia ios 6.0 na kuendelea na kwa android kuanzia ice cream sandwich na kuendelea.Kwa hiyo,kuwa makini unaponunua simu ya iphone au android ili usije kosa bbm integration katika simu yako

Asilimia 74.4% ya simu katika robo ya kwanza ya mwaka 2013 zinatumia android,iOS ikiachwa nyuma tena kidogo

Kampuni ya moja ya takwimu iitwayo Gatner imetoa ripoti ikieleza mauzo ya simu katika robo ya kwanza ya mwaka 2013,Android ikiwa inaongoza operating systems nyingine

Katika smartphones 210 milioni zilizouzwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya  mwaka huu,156 milioni zinatumia android.Huo ni muongezeko wa juu wa asilimia 17.5 ukiangalia kipindi kama hiki kwa mwaka jana.


Research in motion watengenezaji wa BlackBerry ni wa tatu wakiwa wameuza simu zipatazo 6.2 milioni,wakati microsoft ikiwa ikishusha pumzi kwa mauzo ya 6 milioni katika opearting system yake mpya. Samsung anaendelea kuwa namba moja katika watengeneza smartphones na anashikilia asilimia 30% ya mauzo yote,Kampuni ya Korea Kusini imeuza simu 64.7 milioni.Hiyo ni mara mbili ya simu kampuni ya Apple walizouza,wakiwa na mauzo ya asilimia 18.2% na kuuza simu 38.3 milioni.Unaweza kuona makampuni mengine katika chati hapo chini. Jumla ya mauzo ya simu kwa kampuni zote ni 425 milioni,ikiwa ni ukuaji wa ailimia 0.7% tu ukilinganisha na mwaka jana.Kiukweli gap kati ya Nokia na Samsung limeongezeka ukilinganisha na mwaka jana tofauti ilipokuwa 6 milioni tu lakini sasa ni karibu 37 milioni,hii inaifanya Samsung kuwa mbali sana.