Jul 7, 2015

Na Hii Ndiyo Njia Nyingine Rahisi Ya Kuroot Android Yako

Ikiwa wewe ni mfuatilia wa blogu hii kwa hakika hii haitakuwa mara yako ya kwanza kukutana na makala inayohusiana na kuroot smartphone za Android. Lakini ikiwa wewe ni mpya katika blogu hii au ungependa kujua zaidi nini maana ya rooting katika Android na inafanya nini hasa, unaweza kusoma makala yetu iliyotangulia "Nini maana ya Rooting katika Android OSHAPA. Hapo awali tulishaandika njia mojawapo ya kuroot smartphone za Android kwa kutumia app ya towelroot, pia unaweza soma makala nzima "Njia rahisi kabisa ya kuroot smartphone ya Android OSHAPA.

Makala hii inakuletea njia nyingine ya kuroot smartphone yako ya Android kirahisi kwa kutumia app inayoitwa Kingo ROOT. Unaweza kuroot kwa kutumia app hii kwa njia mbili, kwa kupitia PC au kwa njia ya moja kwa moja bila kutumia PC. Njia hizo mbili zinaelezewa hapa chini;

i. MOJA KWA MOJA KWENYE ANDROID YAKO (APK ROOT)

Njia hii ni rahisi zaidi, unachotakiwa kufanya ni kupakua app ya Kingo ROOT, unainstall app hio, kisha unaifungua na kubonyeza sehemu moja tu (single click) na kuacha mchakato wa kuroot uendelee, baada ya kumalizika utapata ujumbe ukikwambia kama rooting imefanikiwa au la!

1. Pakua (download) app ya KingoROOT  HAPA

2.  Install 

     Kumbuka
   Ili kuinstall app hii, lazima uwe umeruhusu simu yako kuweza kuinstall apps kutoka katika vyanzo    visivyo rasmi (unknown sources).
   Kama bado, Ingia katika "Settings" ya simu yako, kisha nenda katika "Security". Ndani ya security    tafuta mahala palipoandikwa "unknown sources", hakikisha sehemu hii ipo activated.

3. Baada ya kuinstall, fungua app hio, kisha bonyeza "ROOT"

4. Subiri mpaka rooting ikamilike kwa 100%

Root
Rooting

5. Baada ya kukamilika, app hio hio itakwambia kama rooting imewezekana au la!

6. Ili kuhakiki kama kweli imewezekana, funga app hiyo na kisha fungua tena, kwa sasa mahali ambapo paliandikwa "No ROOT" hapo mwanzo sasa patakuwa "Have ROOT" ikimaanisha rooting imefanikiwa.

Root Imewezekana
Ina root access

 ii. KWA NJIA YA KUTUMIA PC 

1. Pakua programu ya Android ROOT HAPA

2. Install programu hiyo kwenye PC yako.

3. Baada ya kukamilika kuinstall, ifungue.

4. Unganisha smartphone yako ya Android kwenye PC yako kupitia USB.

     Kumbuka
     Hakikisha "USB Debugging Mode" ipo activated katika smartphone yako, kama haipo activated bonyeza HAPA ili kupata maelezo namna ya kuiwezesha. 
    
 5. Baada ya hilo zoezi kukamilika, sasa unaweza kuiona smartphone yako katika programu ya Kingo ROOT kwenye PC yako. 
    
KingoROOT katika PC

 6. Kama Android yako ilikuwa bado haina root,  hapo unaweza ukairoot, lakini pia kama ungependa kuondoa root au kuiroot smartphone yako tena, machaguo yote hayo unayo kupitia programu hii.

Baada ya kuroot, pakua na install "Kingo SuperUser" kwenye smartphone yako HAPA au HAPA.

SuperUser ndiyo app inayokuwezesha kudhibiti (control) apps zote ambazo zinahitaji root access ili kufanya kazi. Tofauti na apps nyingine zinazofanya kazi ya kuroot (kama vile towelroot), Kingo ROOT ina SuperUser yake maalum ambayo ndiyo hio uliyoishusha hapo juu.



Je, imekusaidia? Hakikisha inamsaidia na rafiki yako pia,  Share!!  & Comment!!


No comments :

Post a Comment