Dec 28, 2013

Nini maana ya Rooting katika Android OS.

Mtengeneza simu yoyote anapoitengeneza simu yake huweka mipaka ambayo yule mtumiaji anapoitumia bidhaa hiyo hawezi kuivuka mipaka hiyo kwa hali ya kawaida.Pia hata mitandao ya simu mfano.Vodacom,Airtel inapouza simu hasa smartphones(ambazo zinatumia sim card za mitandao yao tu) huweka apps zao ambazo kwa hali ya kawaida huwezi kuzifuta wala kuzirekebisha.Hapa ndipo mfumo wa kufanya rooting ulipotokea ili kuweza kutatua hili tatizo.

Rooting ni mchakato wa kuifanya smartphone ya Android kuweza kufikiwa mpaka pale ambapo mtengeneza simu hiyo ameweka mipaka.Hii ina maana kwamba rooting inakupa uwezo wa kufuta apps ambazo zimekuja na simu(pre-installed apps),kuweza kubadilisha au kuboresha operating system nzima ya simu,kuweza kurekebisha source code ili kuweza kubadili baadhi ya commands katika operating system na mambo mengine kadhalika.

Android OS imetengenezwa kwa msingi wa operating system ya kompyuta inayoitwa Linux OS.Inatumia Kernel(ni programu ambayo kazi yake ni kufanya michakato ya taarifa zinazotoka na kuingia katika programu nyingine katika kompyuta,hutafsiri taarifa zote za programu mbalimbali katika CPU ya kompyuta) ya Linux.

Unapofanya rooting unakuwa umeingia ndani ya operating system ya Android na kuweza kufanya lolote lile.Hii inapelekea simu husika kuwa katika usalama mdogo hasa katika kushambuliwa na programu hatari(malicious softwares) ambazo zinaweza kuchukua taarifa kutoka katika simu bila ruhusa ya mmiliki.


Mchakato wa rooting unatofautiana kati ya smartphone moja ya Android na nyingine,kuna njia mbalimbali.Unaweza kutumia programu ya kompyuta au kwa kutumia simu yenyewe tu.Baada ya kufanya rooting app inayoitwa Superuser itakuwa installed katika simu husika.Hii itahusika na kutoa ruhusa katika michakato yote itayofanyika katika smartphone.


Faida ni nyingi sana za kufanya rooting.Kuna baadhi ya simu mfano Huawei huwezi badilisha maandishi(fonts),hii itawezekana pale utapofanya rooting,na pia kuweza kuchagua themes,kufanya installation ya custom rom na mengineyo mengi.

Hasara ni kwamba warranty yako inakuwa batili na iwapo simu yako itapata tatizo lolote la kiufundi basi hautaweza kurekebishiwa kwa kutumia warranty yako,huwezi pata updates rasmi(official firmware updates).Mchakato wa rooting unahitaji umakini kidogo kwa sababu pale unapokosea simu inaweza haribika jumla na kuwa isiyo na matumizi(bricked smartphone).

No comments :

Post a Comment