Jan 23, 2015

Sasa, WhatsApp Inapatikana Katika Desktop

Ikiwa wewe ni mtumiaji wa WhatsApp na ungependa kutumia Instant Messenger hii pamoja na apps nyingine za Android katika desktop yako huna budi kuweka emulator ili kufanikisha hilo. Miongoni mwa emulators maarufu na zinazopendwa kutumiwa ni BlueStacks pamoja na YouWave, kwa hakika watumiaji wa WhatsApp katika desktop wanazifahamu.

Lakini, si mara zote emulator hizi hukubali kufanya kazi kirahisi katika desktop, zipo ambazo huhitaji mazingira maalum ili kufanya kazi, kwa mfano emulator kama Andy au GenyMotion zinahitaji Virtual Machine (kama vile VirtualBox) pamoja na processor yenye teknolojia ya "Virtualization" ili kufanya kazi. Hili si suala dogo kwa sababu wapo ambao hushindwa kabisa kutimiza mahitaji hayo.

Ikiwa sababu kubwa ya kuinstall emulator katika desktop machine yako ni kupata ladha ya WhatsApp katika desktop tu, basi kuanzia sasa huhitaji emulator yoyote kwa sababu WhatsApp inapatikana katika desktop bila hata kuwa na emulator yoyote!.


Labda niondoe mkanganyiko hapo, hii haimaanishi kwamba kuna toleo jingine jipya la WhatsApp limetoka (standalone) ambalo unaweza "install" messenger hio na kutumia katika desktop yako, hapana. Kinachofanyika hapa ni kukuwezesha kutumia WhatsApp app iliyo kwenye smartphone yako katika desktop, hili linafanikishwa kupitia web browser yako (web app), hivyo conversations na sms zote zinabaki katika simu yako.

Kwa sasa WhatsApp Web inapatikana katika Android, BlackBerry OS na Windows Phone, kwa sababu ya "Apple platform limitations" huduma hii haipatika katika iOS.


Mwonekano wa WhatsApp katika Desktop

    Mahitaji:
  • Toleo la mwisho(latest) la WhatsApp, fanya update.
  • Google Chrome Browser, kuanzia toleo la 36 au juu zaidi
  • Unahitaji kuwa online katika smartphone yako ili kuwa online katika desktop pia.
Kwa sababu za kiusalama mchakato wa ku-login unafanyika kwa kutumia QR (Quick Reference) code na sio kwa username na password.
  • Kupata option ya WhatsApp Web pamoja na control settings nyingine kulingana na platform (OS) unayotumia, fuata maelezo katika picha




Umeitumia? Umeionaje? Usiache kutoa maoni yako. Na kama umependa makala hii usiache kushare link na mwenzio.

No comments :

Post a Comment