Feb 3, 2015

Sony ana wakati mgumu katika biashara ya smartphones.

Sony Xperia ni moja ya smartphones bora, zikitumia Android operating system. Zipo katika aina mbalimbali, kuanzia zile za kiwango cha chini(low end) mfano Xperia U, kiwango cha kati(midrange) mfano Xperia C na mpaka zile za kiwango cha juu(high end) mfano Xperia Z3. Nyingi ya modeli hizi zinafahamika kwa kuwa na uwezo wa kuzuia maji na vumbi(water and dust resistant).


Sony Xperia Z3.

Pamoja na hayo yote, Sony anapata hasara katika biashara hii. Mwaka jana walivunja rekodi ya mauzo ya gaming console yao ya PlayStation 4. Lakini faida hii ilisawazishwa na hasara iliyotokana katika mauzo ya smartphones pamoja na televisheni. Kampuni hii ya Kijapan ipo katika mipango ya kupunguza utengenezaji wa smartphones na televisheni kwa pamoja.

Wana mipango ya kuegemeza bajeti kubwa katika biashara ya gaming console za Playstation ambazo kiuhalisia zinafanya vizuri katika soko, na pia katika biashara ya kutengeneza kamera za smartphones(image sensors) ambazo hutumika katika smartphones kama iPhones, Oppo n.k.

Si kwamba wataacha kutengeneza smartphones kabisa, bali watapunguza namba ya modeli zilizopo. Wanachojali zaidi ni kupata faida nzuri katika soko. Lakini hali pengine inaweza pelekea kuwakatisha tamaa wateja wao wakubwa ambao wengi wapo mabara ya Asia na Ulaya. Pamoja na kwamba watapoteza masoko mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yanatawaliwa na Samsung na Apple, lakini wataondokana na hasara wanayoipata sasa.

Sony ana bidhaa nzuri sana, kinachompelekea kukosa masoko ni kushindwa kujitangaza vya kutosha kama kampuni za Samsung na LG zifanyavyo. Watu wengi hununua televisheni za Samsung na LG kuliko za Sony, yote hii ni kwa sababu Sony hajitangaza vya kutosha. Bidhaa zake nyingi zina gharama kuliko wapinzani wake, si kwamba zina specifications bora kuliko za Samsung au LG. Lakini wanakosa kufanya uchanganuzi mzuri katika kujua ni vipi wanaweza kupambana katika soko na kuvuta watumiaji wengi wa bidhaa zao.

No comments :

Post a Comment