Jan 28, 2014

Nini maana ya "Phablet"?

Katika kukua kwa suala lolote,basi hata misamiati inayohusiana na swala hilo itaongezeka. Mfano katika biashara kati ya jamii na jamii,hapo lazima mwisho wa siku yatazaliwa maneno mapya. Hali hii ipo pia katika teknolojia ya smartphones.

 Ni nini hiki kitu kiitwacho Phablet,kuna maana kadhaa zinazoweza kueleza kuhusu kifaa hiki cha kielectroniki.

  • Phablet ni kifaa cha kielectroniki chenye sifa za smartphone na sifa za tablet.Smartphone+Tablet=Phablet,limechukuliwa kijineno "Ph" katika Smartphone na "ablet" katika neno Tablet.Hii yote ni kupata neno rahisi la kutamkwa.
  • Ina ukubwa wa kuanzia inchi 5.3na kuendelea na haizidi inchi 7. Smartphones nyingi ukubwa wake huwa hauzidi inchi 5.2 na tablet nyingi ukubwa wake huanzia inchi 7 na kuendelea.


    Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 2.
 Tukirudisha kumbukumbu nyuma kidogo,phablet zilianza kuonekana mnamo mwaka 2011. Samsung alizindua Samsung Galaxy Note N7000. Phablet hii ilikuwa ikitumia stylus(mfano wa pen unayotumia kuandikia katika display za touchscreen),kwa watu wengi ilionekana phablet si kitu cha maana kabisa na kutokana na ukubwa wake ikaonekana ni mzigo. Kipindi hicho smartphone nyingi zilizokuwa ni flagship zilikuwa na kioo cha inchi 4.3 mfano Samsung Galaxy SII na wakati Galaxy Note ilikuwa ina kioo cha inchi 5.3.
Samsung Galaxy Note N7000,phablet ya kwanza ya Samsung.

Samsung alijua wazi kabisa alichokuwa anakifanya. Pamoja na kwamba mwanzoni watu waliona ni kitu cha ajabu lakini taratibu mitazamo ikawa ikibadilika na kuona phablet inafaa hasa na kutokana na kuwa display kubwa. Mwaka 2012 Samsung akazindua phablet nyingine ilijulikana kama Samsung Galaxy Note 2.

Watu wakaanza kuzizoea na mwaka 2013 ndiyo mwaka ambao tumeona phablet za kutosha sio kwa Samsung tu bali na kwa makampuni mengi makubwa. Samsung amezindua phablets kama Samsung Galaxy Mega 6.3,Mega 5.8 na kadhalika. Iliyovuta makini ya wengi ni Samsung Galaxy Note 3 ambayo tangu kuzinduliwa mwaka jana lakini mpaka sasa ndiyo kifaa bomba kabisa.

Sony Xperia Z Ultra.
Makampuni mengine yalioonesha umwamba katika teknolojia ya phablet katika mwaka 2013 ni kama HTC,Sony,Nokia na LG,ukiziangalia phablet za makampuni haya zinafanana na smartphone ambazo ni flagship zao mfano. HTC One phablet yake ni HTC One Max,zinafanana muonekano lakini tofauti ipo katika ukubwa wa umbo na sifa(specifications) za phablet huwa chini kidogo. Yapo makampuni mengi yenye phablet pia lakini hayakubamba kama ilivyo kwa kampuni nilizotaja hapo juu.Nadhani mwaka huu wa 2014 ni mwaka wa kutegemea mengi sana katika teknolojia ya simu kwa ujumla. Tutaona phablet nyingi sana zikizinduliwa,tablet zenye hadi ukubwa wa inchi 20,simu zenye kioo cha kujikunja(tayari tushaanza kuona kwa LG G Flex) na mengine mengi sana.

No comments :

Post a Comment