Nov 24, 2014

Majuto baada ya kufanya update ya software katika smartphone.

Tulio wengi huwa na shauku kubwa sana wakati tunasubiri Operating System(OS) mpya ku update devices zetu, iwe ni tablet au smartphone... shauku ni ile ile. Mategemeo yetu makubwa huwa ni kwamba tunajua tutapata features nyingi mpya, muonekano (User Interface) utaboreshwa na pia baadhi ya matatizo(software bugs) yaliyokuwepo katika version ya OS iliyopita yatapata ufumbuzi. Software update inaweza fanyika kwa njia mbalimbali, kama kutumia programu ya kompyuta(desktop manager) kwa kuunga smartphone/tablet kwenye kompyuta kwa kupitia USB( Universal Serial Bus) na kisha kufanya update process. Njia nyingine haihitaji kutumia kompyuta na pia wala haikuhitaji kuwa na utaalamu wowote wa kiufundi ili kuweza kukamilisha process hii, inafahamika kama OTA(Over The Air) update. Kinachofanyika katika process hii ni kwamba itakuja notification ya kukujulisha kama software mpya inapatikana, utatakiwa kuidownload hiyo software na baada ya hapo utakubali kufanya update na baada ya process hiyo kumalizika utakuwa na software mpya na tayari kuanza kufurahia features mpya. Lakini je! ni mara zote huwa tunafurahia software mpya?


Software updates zipo mahususi kwa ajili ya kusolve matatizo na kuleta vitu vipya na si kuharibu mambo na kutufanya kujuta kufanya update hiyo. Ni mara nyingi sana pale software update inapotoka huleta matatizo mengi baada ya watu kufanya update hiyo. Hivi karibuni, software update ya Android Lollipop 5.0 ilitoka kwa kupitia OTA update. Devices zilizotakiwa kupata update hii ni Nexus 5 na Nexus 7(2012&2013). Lakini hali ni mbaya kwa watumiaji wa Nexus 7(2013), wengi wanalalamika kuhusu matatizo mengi kama video kutocheza vizuri, application nyingi zinaacha kufanya kazi ghafla(apps crash) na mengine baadhi. Matatizo haya si mara ya kwanza kutokea katika historia ya software updates za Android, watumiaji wengi wa Nexus 7(2012) walipata tatizo la kufeli kwa sensors kama gyrometer na accelerometer baada ya kufanya update ya Andoid KitKat  mnamo mwaka jana, na mpaka leo hii Google hajaweza kusolve tatizo hilo kwa njia yoyote. Hali hii inachanganya kidogo, inaleta wasiwasi na kusitasita pale unapotaka kufanya software update. Inafika mahala linaonekana kama ni jambo la bahati nasibu, unaweza update na usipate tatizo lolote au ukafanya update na ikawa majanga haswa!

Nexus 7(2013)

Imembidi Google kuacha kuendelea kutoa OTA update hii ya Android Lollipop 5.0 mpaka pale tatizo hili litapopata marekebisho. Haijulikani ni lini hasa software update hii itakuja tena, pengine wiki mbili au zaidi kuanzia sasa. Pengine wataweza rekebisha kasoro zote na kuleta update iliyo kamili bila matatizo(glitch free).

Kwa upande wa Apple, mambo ni yaleyale tu. Kama ni mfuatiliaji utakuwa unakumbuka hekaheka zilizokuwepo mtandaoni siku update ya iOS 8 ilipotoka kwa smartphone za iPhone 4S, iPhone 5 na iPhone 5S. Malalamiko yalitanda katika mtandao wa Twitter watu wakilalamika update inahitaji kiasi takribani 6GB of free space, kisicho cha kufurahisha ni kwamba baada ya kumaliza kufanya update free space inabaki vilevile bila kutumika. Ilipelekea watu kupoteza data zao muhimu sana kama picha, documents, miziki na kadhalika kwa sababu inakubidi kufuta vitu ili kupata free space hiyo na hasa pale ambapo memory ya smartphone yako inakaribia kuwa full. Na hata baada ya kufanya updates, baadhi ya matatizo yalizidi kutokea kama simu kupoteza mtandao mara kwa mara, Touch ID sensor katika iPhone 5S ilikuwa inasumbua katika kufanya kazi kwa ufasaha, battery kuisha haraka, Wi-Fi kusumbua pale unapotaka kujiunga kwenye hotspot, apps kuacha fanya kazi ghafla au kuganda(stuck).

Limekuwa ni swala la kawaida kuzungukwa na software updates zenye madhara kwa device zetu. Ushauri wangu: naielewa sana shauku ya kusubiri software update na kutaka update pale tu inapotoka, jifunze kuizuia. Update inapotoka subiri angalau siku nne huku ukipitia majadiliano(tech forums) mbalimbali katika mtandao na kuona watu wanaotumia device yako wanasemaje baada ya kufanya update. Utapoona shangwe ni nyingi kuliko malalamiko, basi hapo upo salama kufanya update.


No comments :

Post a Comment