Dec 10, 2014

Devices maalumu kwa ajili ya kupiga "selfie" photos.

Utazikuta katika Instagram, Twitter, Snapchat na kadhalika, tena kwa wingi mno. Ni wazi kabisa selfies zimechukua nafasi kubwa sana ya maisha ya watu wengi katika zama hizi za kidijitali, ukianzia watoto, vijana mpaka wazee. Selfie ni picha inayopigwa ikijumuisha mtu mmoja au zaidi na mpiga picha huwa ni mmoja wa wahusika/mhusika waliopo katika hiyo picha, kwa lugha fupi ni picha ya kujipiga mwenyewe. Neno hili limetokana na maneno ya lugha ya kiingereza yanayomaanisha picha ya kujipiga mwenyewe "self-taken photo" na kufupishwa kwa kifupi "selfie". Pamoja na kwamba historia ya selfies inaanzia tangu karne ya kumi na nane lakini wakati huu ndipo tendo hili limeshika hatamu haswa, hii ni kutokana na uwezo wa devices kama smartphones na digital cameras zinazokuwezesha kuchukua picha zenye ubora wa hali ya juu, devices hizi pia ni rahisi kuzibeba(portable). Tuangalie baadhi ya devices ambazo zimetengenezwa mahususi kwa ajili ya kupiga selfies zenye ubora.
Selfie ya Barack Obama, Helle Thorning-Schmidt na David Cameron. Moja ya selfies zilizowahi kuleta gumzo kidogo!


HTC Desire Eye.

HTC Desire Eye
Imezoeleka ya kwamba smartphone nyingi huwa na kamera ya mbele(secondary camera/front facing camera) yenye 2MP(Mega Pixels), ni tofauti sana kwa HTC Desire Eye, ina camera ya mbele yenye 13MP(Mega Pixels) ikiwa pamoja na dual-LED flash, hii ndiyo smartphone ya kwanza katika historia kuwa na camera ya mbele yenye megapixels kubwa kiasi hicho, kamera yake ya nyuma ina 13MP pia nayo ikiwa na dual-LED flash. Ukiwa na smartphone hii unaweza piga selfies hata nyakati za usiku katika sehemu zisizo na mwanga kwa kutumia kamera ya mbele kwa sababu ya uwepo wa dual-LED flash.


Sony Xperia C3.

Sony Xperia C3
Kwa miaka mingi kampuni ya Sony inasifika katika katika kuwa na teknolojia ya hali ya juu, kuanzia kutengeneza movies, game consoles za Playstation, cameras hadi smartphones. Wamedhihirisha hilo kwa kutengeneza Sony Xperia C3, ikiwa na camera ya mbele yenye 5MP na LED flash ambayo inafahamika kama "soft LED flash" , sifa za flashlight hii ni kwamba pale unapopiga selfie kwa kutumia flashlight, haitatoa mwanga ambao utaumiza macho yako. Hivyo basi, utaweza kupiga selfie nyingi unavyoweza bila kuumia macho. Kamera yake ya mbele ina 8MP ikiwa na LED flash pia.


Selfie Stick.

Matumizi ya Selfie Stick.
Hii ni aina ya fimbo ambayo hutumika kupiga selfie pale unapohitaji picha inayochukua sehemu kubwa ya mwili au inayohusisha watu wengi. Inafanya kazi kwa kuchomeka smartphone/digital camera yako katika holder(ikiwa katika landscape mode[ubavu]), holder hiyo ipo mbele ya fimbo na kisha upande mwingine wa fimbo hiyo maalumu ndipo utashikilia, unaweza kuongeza au kupunguza urefu wa fimbo hiyo vile unavyopendelea. Inakuwezesha kupiga picha bila kuweka self-timer katika smartphone yako kwa sababu ina button maalumu katika sehemu ya kushikilia zinazokuwezesha kufocus, kuzoom na pia kupiga picha. 


Zipo devices nyingi sana kwa ajili ya selfie lakini nilizotaja hapo juu ndizo zinafahamika sana na watu wengi. Kwa upande wa smartphones, selfie hupigwa hata kwa kutumia camera ya nyuma lakini kwa kutumia ya mbele ni rahisi mno kwa sababu unaweza kuona ni wapi unapoelekeza camera yako kwa picha bora zaidi. Ingawa kuna watu ambao wapo vizuri sana katika kupiga selfie kwa kutumia camera ya nyuma!



No comments :

Post a Comment