Oct 14, 2014

Battery life, tatizo sugu katika smartphone aina zote.

Moja ya vitu visivyofurahisha katika matumizi ya smartphone ni ubora wa battery. Tatizo hili humkuta kila mtumiaji wa smartphone, lakini hii si kwamba inafanya watu kuacha kutumia simu hizi. Wanaendelea kuzitumia na yote kwa sababu hawana njia nyingine mbadala. Labda, njia mojawapo za kupunguza makali ya kero hii ni kumiliki battery ya ziada endapo smartphone yako ina uwezo wa kutoa battery(removable battery) au kubeba chaja katika mkoba wako. Pamoja na hayo yote, swali moja muhimu sana watu hujiuliza, "pamoja na teknolojia iliyopo sasa, inashindikana kuwepo battery yenye uwezo wa kukaa muda mrefu?



Jibu la swali hili linaweza kuwa "ndiyo" kwa upande mmoja na "hapana" kwa upande mwingine. Teknolojia ya battery za smartphone inayotumika sasa ni ileile iliyokuwa ikitumika miaka ya nyuma wakati simu hizi zinaanza pata umaarufu. Mfumo huu wa teknolojia ya battery unasimama katika msingi usemao:" ili battery iwe na uwezo mkubwa basi inabidi size(area) ya battery hiyo iwe kubwa pia", hii inamaanisha kiasi cha
chaji kitachohifadhiwa kitakuwa kikubwa zaidi. Kanuni
hii ina matokeo hasi katika teknolojia ya smartphones na hasa pale mtengeneza
smartphone
anapoamua kutengeneza smartphone yenye uwezo mkubwa wa battery, kikubwa ni kwamba. Kama mtengeneza smartphone anataka kuunda simu itayoweza kukaa na chaji kwa muda mrefu mfano wa siku nne mfululizo katika matumizi ya kawaida basi itambidi kufanya simu hiyo kubwa sana na pana ili kuweza kuweka battery kubwa itayoweza leta matokeo hayo. Ukirudi kwa watumiaji, hakuna anayetaka simu nene,pana na nzito(bulky). Watu wengi hupendelea simu nyembamba(slim) na nyepesi. Smartphones za kawaida ni ndogo kwa size ukafananisha na phablets au tablets, ndiyo maana unaona hizi mbili zina uwezo mkubwa wa kiasi fulani katika kutunza chaji na yote ni kwa sababu zinabeba battery kubwa, hili linawezekana kwa sababu size ya devices hizi ni kubwa.

Kwa teknolojia hii ya mfumo wa battery, kuna ugumu katika kuweza kupata smartphone yenye uwezo mkubwa sana wa battery huku ukifanya size yake kubaki vilevile. Lakini swali linakuja, kuna ufumbuzi wowote utaoweza kumaliza tatizo hili siku za mbeleni?. Kuna baadhi ya tafiti zimefanyika miaka ya karibuni katika kutafuta suluhisho la tatizo hili, kwa kutumia teknolojia ya nanotechnology, ambayo ni mpya kidogo. Teknolojia hii inatumika katika mambo ya kielectroniki, kibiolojia, kikemia na kadhalika, inadeal na utengenezaji wa material katika msingi wa size ya molekyuli. Kwa maelezo ya kawaida, inawezesha kutengeneza mifumo mbalimbali katika size ndogo sana, mfano sakiti za kidigitali za kielectroniki(integrated circuits), matumizi ya nanotechnology yanawezesha sakiti hizi kuwa ndogo sana na kuwa na vitu vingi. Hii inapelekea kuweza kutengeneza battery ya size ndogo huku ikiwa na uwezo mkubwa. Baadhi ya watafiti katika chuo cha Stanford huko Marekani walifanya tafiti hii na kuleta matokeo chanya.

Pamoja na hayo yote, bado msukumo wa teknolojia ya nanotechnology kuwa kamili(perfect) ni mdogo. Haijawahi jaribishwa katika smartphones na kuona matokeo yake baada ya muda kadhaa, kingine ni kwamba hata kama itawezekana kutumika katika smartphones itakuwa ni gharama kubwa sana. Ni kama zilivyo televisheni za 4K, ni gharama sana ukilinganisha na LED/LCD TV za kawaida na hii ni kwa sababu ni teknolojia mpya. Muda utapopita na teknolojia hii kufanyiwa majaribio na kutafuta namna ya kuzalisha bila gharama kubwa ndipo tutaanza kuona matumizi makubwa ya teknolojia hii.

Wakati mwingine, tatizo la battery katika smartphones linachangiwa na watengenezaji pia, katika maslahi ya kibiashara. Kama ukiwa na smartphone ya Samsung yenye battery imara sana, sidhani kama utasumbuka kuwaza kubadili simu pale toleo lingine likija. Ili kukufanya next time ununue tena simu yao hawaweki battery itayokuridhisha kwa muda mrefu na kukufanya uwaze kukaa na simu hiyo kwa miaka kumi. Si kwamba kusema wanapunguza ubora wa battery, hapana. Ni hali ya kufanya biashara izidi kukua na kupata soko kwa bidhaa zao kila zinapotoka.

No comments :

Post a Comment