Oct 15, 2014

Njia rahisi unazoweza tumia kuzuia kupotea kwa namba zako za mawasiliano (Contacts)

Huwa inatokea, labda umeibiwa au kupoteza simu yako au unataka kubadili simu  au labda umeifanyia simu yako system restore iwe ni kwa kukusudia, bahati mbaya au hata kwa kutaka kutibu (resolve) tatizo fulani mpaka ikapelekea kufanya hivyo. Unaweza poteza data nyingi, lakini kikubwa na cha muhimu zaidi ambacho hupotea huwa ni namba za mawasiliano (Contacts).

Hali hii inapotokea huleta huzuni na pia hasira kwa baadhi ya watu na hii yote ni kwa sababu ya hasara iliyotokea. Lakini unaweza hifadhi contacts zako na endapo utazipoteza au chochote kutokea basi utaweza kuzipata kirahisi tena. Nitataja njia chache muhimu unazoweza kuzitumia kama ifuatavyo.


ANGALIZO: Hii ni kwa Android Smartphones tu.

1. Tengeneza vCard file (.vcf file)

vCard file ni file ambalo huhifadhi contacts likiwa linajumuisha taarifa  kama
Phone numbers, E-mail addresses, Contact pictures, Street addresses, Family information, Website addresses, Notes n kadhalika.

Hatua za kutengeneza file hili ni hizi:
i. Bofya Menu ya simu yako
ii. Kisha bofya icon ya Contacts/ People
iii. Options/Manage Contacts
iv. Import/ Export contacts
v. Chagua Export to Phone Storage/sdcard
vi. Chagua Google/ email yako
vii. Create/ Export contacts.vcf.Hatua zinaweza tofautiana kulingana na simu yako.

Katika phone storage/ microsdcard yako utakuta kuna file limeongezeka lenye muendelezo (extension) wa .vcf. Unaweza hifadhi file hili mahali popote unapohitaji.
Kurudisha contacts zako unatakiwa kuweka vCard file kwenye simu yako, kisha install

2.  Hifadhi katika account yako ya Gmail (Back up)

Hii ni njia nzuri na ndiyo ninayopendekeza sana kutumia. Inaweza kutokea hata vCard file ulilotengeneza hapo juu likapotea,
Hamisha Contacts kwenda Gmail
ni vizuri kuliweka kwenye account yako ya Gmail kuzuia kupotea kwake.
Hatua ni rahisi
i. Ingia kwenye Gmail account yako kupitia browser yako ya computer.

ii. Juu kushoto, bonyeza Gmail kisha chagua Contacts

iii.Kutoka kwenye hiyo drop-down menu, chagua Import Contacts

iv. Choose File, elekeza mahali ulipoweka vCard file lako.

v. Halafu Import.
Endapo utaingiza Gmail yako kwenye simu,synchronization itafanyika au unaweza fanya manually ili kuhakiksha contacts zinakuwa kwenye account na kwenye simu.
Pia inashauriwa kufanya synchronization muda wowote unapoongeza taarifa yoyote kwenye contacts zako. Synchronisation ipo katika menu halafu ingia katika settings halafu chagua accounts&sync, chagua Google account halafu bonyeza "sync now", contacts zako zote zitakuwa saved katika Gmail account na muda wowote unaweza zipata katika simu yako na hata device nyingine ambayo inatumia Gmail account hiyohiyo.

3. Save contacts kwenye computer yako. 

i. Weka vCard file popote kwenye computer yako
ii. Right-click hilo file kisha chagua "open with"
iii. Chagua contacts.
iv. Anza kusave contacts zako.

*Sharing Is Caring. . .
*Kwa lolote, weka comment yako hapo chini.



No comments :

Post a Comment