Oct 29, 2014

"Kila iPad ni Tablet" na "Si kila Tablet ni iPad".

Kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko katika matumizi ya maneno haya mawili, iPad na Tablet. Hapa kuna mambo mawili ambayo hujitokeza mara kwa mara. Kuna wale ambao huita Tablet yoyote iliyo mbele ya macho yao "iPad" na wengine hudhani kwamba iPad si "Tablet", hawa wote wanakosea. Lakini, kabla ya kwenda mbali sana tujue kwanza maana za haya majina mawili.


TABLET - nI kifaa cha kielectroniki chenye ukubwa wa kioo(display) kuanzia inchi 7 hadi inchi 20(Panasonic washawahi toa tablet ya aina hii). Ina uwezo kama smartphones nyingine, kuna zile zinaweza kuweka sim card na kufanya mawasiliano kama ya simu na zile zisizo support sim card, hizi hutumia wireless internet(Wi-Fi) na zinafahamika kama WiFi only tablets, hutumia WiFi tu kwa mawasiliano, huwezi piga simu wala kutuma sms(no GSM communication). Mfano wa tablets ni kama Nexus 7, iPad mini 2, iPad Air, Kindle Fire HD n.k.

iPad - Ni tablets zinazotengenezwa na kampuni ya Apple. Zipo katika muundo mbalimbali, model zake hutofautiana katika sifa(features) kama
kioo(display), battery, camera, processing power n.k. Hutumia operating system(OS) sawa na ile inayotumika katika simu za iPhone, inayojulikana kama iOS. Kinachofanya tablets hizi kuonekana za tofauti na tablets nyingine mfano zile zitumiazo Android OS kama Nexus 7, LG G Pad n.k ni bei ya mauzo, iPad hugharimu pesa nyingi sana kulinganisha na tablets nyingine. Cha kushangaza, si kwamba gap la bei linaenda sambamba na gap la sifa(specifications), ni kinyume. Apple iPad Mini 2 ni takribani laki moja na nusu zaidi kwa Nexus 7(ukilinganisha kwa model za WiFi only). Lakini kwa specs, Nexus 7 iko mbali sana.......

Kwa maana hizo mbili hapo juu, sidhani kama utaweza  kuita tablet yoyote "iPad" tena.... Lakini bado kuna swala moja ambalo si watu tu wanakosea, hata makampuni makubwa yanakosea pia. Kuitofautisha iPad na Tablets nyingine, makampuni makubwa kama Walmart, Bestbuy na mengineyo huweka iPad katika kundi la pekee, Tablets nyingine zote zinazosalia huwekwa katika kundi moja la "Tablets". Hii si sahihi kabisa!



Amazon pia alikuwa akifanya kitu hiki katika tovuti yake, uzuri ni kwamba alitambua kosa hili na akabadilika. Kwa bahati mbaya, Walmart, Bestbuy na wengine wengi hawajarekebisha kosa hili. Kwa wewe....... Rekebisha!


No comments :

Post a Comment