Nov 1, 2014

Internet.org, inakuwezesha kutembelea tovuti zilizo maarufu duniani bure.

Hatimaye internet.org imefika Tanzania. Mradi huu ambao ni wa kampuni ya Facebook unakuwezesha kutembelea tovuti nyingi maarufu duniani kama Facebook, Facebook Messenger, Wikipedia, BBC News, Super Sport pamoja na kupata habari mbalimbali za kitaifa bila malipo yoyote ya mtandao. Internet.org inapatikana katika namna mbili, ikiwa kama Android app inayopatikana Google Playstore na pia kama tovuti. Tanzania ni nchi ya pili kupata huduma hii ikitanguliwa na Zambia ambao walianza kutumia huduma hii mnamo mwezi wa Julai mwaka huu.
Kwa Tanzania tovuti zinazopatikana kupitia Internet.org ni;
  • AccuWeather – Utabiri wa Hali ya Hewa
  • BabyCenter & MAMA –Taarifa kuhusu afya ya Uzazi na Watoto
  • BBC News & BBC Swahili – Habari za Kitaifa na Kimataifa
  • BrighterMonday – Tafuta kazi
  • The Citizen – Habari za kitaifa
  • Facebook – Mtandao wa kijamii
  • Facts for Life – Afya na Usafi
  • Girl Effect – Makala na vidokezo kwa ajili ya Wasichana
  • Messenger – Chat katika mtandao wa kijamii wa Facebook
  • Mwananchi –Habari kuhusu Tanzania
  • Mwanaspoti – Habari za Michezo
  • OLX – Matangazo ya Kununua na kuuza bidhaa
  • Shule Direct – Elimu
  • SuperSport – Habari za Michezo
  • Tanzania Today – Habari za Kitaifa Tanzania
  • Wikipedia – Kutafuta taarifa na maelezo mbalimbali.
Kuna utofauti katika huduma hii kwa Tanzania na Zambia, nchini mwetu app ya Internet.org haina uwezo wa kuwezesha Google Search bila malipo tofauti na Zambia, na pia kwa Zambia wana uwezo wa kupata Google Search Results tu lakini si kuendelea kutembelea results hizo. Ikumbukwe pia huduma hii kwa Tanzania ipo chini ya mtandao wa tigo, hivyo basi ni lazima uwe mtumiaji wa mtandao huo ili kuweza kupata huduma hii.


Internet.org ni project iliyoanzishwa August 20,2013 chini ya kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook ikishirikiana na makampuni ya simu ya Samsung, Nokia, Ericsson, Opera Software, Qualcomm pamoja na MediaTek. Lengo kuu la project hii ni kuwezesha dunia kupata huduma muhimu ya internet ya uhakika kwa gharama nafuu zaidi ikiwa imejikita katika nchi zinazoendelea zikiwa ni sehemu kubwa ya bara la Afrika na sehemu ya nchi za bara la Asia. Uzinduzi wa huduma hii kwa Tanzania ni muendelezo wa huduma kama Zero Facebook ambayo ilizinduliwa kipindi cha nyuma.


Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA ya June 2014 inaonyesha kuwa idadi ya watumiaji wa internet Tanzania ni milioni 9.3 ikiwa imepanda kutoka milioni 7.5 mwaka 2012. Hii ni idadi ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya watu Tanzania ambayo inakadiriwa kuwa ni milioni 50.8 kwa mujibu wa ripoti ya World Population.

Project hii italeta msukumo mkubwa sana katika matumizi ya internet yenye manufaa. Tanzania bado tupo nyuma katika matumizi ya internet yenye kuleta manufaa kama kwa ajii ya shughuli za kielimu, kiafya, kiuchumi na nyanja nyingine mbalimbali ukilinganisha na nchi nyingine zilizopo barani Afrika kama Afrika Kusini, Kenya, Nigeria, Egypt na nyinginezo. Elimu zaidi inahitajika kutolewa katika matumizi sahihi ya huduma za mtandao ili kutuletea maendeleo, kuongeza upana wa maarifa na ujuzi, na pia kukuza uchumi wa nchi na pia kwa mtu mmoja mmoja.

Internet inakusaidia vipi katika shughuli zako za kila siku?  Usisite kutoa maoni yako hapo chini.

Download internet.org kwa Android hapa

Ingia internet.org hapa

No comments :

Post a Comment