Oct 25, 2014

Hatutakuwa na smartphones zitazoitwa Nokia.

Baada ya Microsoft kununua Nokia, kampuni maarufu duniani iliyokuwa na makazi yake nchini Finland. Microsoft ameamua kuacha kutumia brand name ya kampuni hiyo katika smartphones za Nokia Lumia, na kuanzia sasa simu hizi zitafahamika kwa jina la Microsoft Lumia. Simu mpya zitazotumia Jina la Microsoft Lumia zitazinduliwa hivi karibuni. Miaka kadhaa iliyopita kumekuwa na mahusiano mazuri na ya karibu kati ya kampuni hizi mbili, Nokia alijiunga na Microsoft katika kutengeneza smartphones za Windows Phones ili kuweza kukabiliana na ushindani katika soko ambao kwa sasa unatawaliwa na Google's Android sambamba na Apple's iOS.

Logo mpya itayotumika katika smartphpnes za Microsoft Lumia
Bila ya Nokia kufanya hivi, pengine ingekufa jumla. Hii imesaidia sana katika kufanya Nokia kuwa katika soko la smartphone kwa kupitia simu za Lumia. Ndiyo maana Microsoft kainunua akiiona kwamba italeta faida katika siku za mbeleni. Windows Phone
OS(operating system inayotumiwa na simu za Lumia) inazidi kukua siku hadi siku, muonekano wake(User Interface) unazidi kuwa wa kisasa zaidi ukiwa na features nyingi, store yake ya applications iitwayo
Marketplace inazidi kukua kwa kupata apps maarufu kama Instagram, Pinterest n.k. Umaarufu wa smartphones za Windows Phone
unazidi kuongezeka pia sehemu kama za Asia, Latin Amerika na sehemu nyingine za masoko yanayochipukia(emerging markets) kama Africa na Ulaya Mashariki.

Microsoft ataacha kutumia brand ya Nokia katika smartphones za Lumia tu. Simu nyingine za kawaida kama model za Nokia Asha na features phones nyingine za Nokia zitaendelea kutumia brand name ileile ya Nokia.

No comments :

Post a Comment