Sep 4, 2014

iPhone 6! pengine itakuwa smartphone bora kuwahi kutengenezwa katika historia.

Ni takribani miaka 16 tangu neno "smartphone" kuanza kutumika, aina hii ya simu ina historia ndefu sana ambapo inarudi hadi miaka ya 1970. Umaarufu wake haswa umekuja mnamo mwaka 1998 ambapo kampuni ya Ericsson ilizindua simu inayoitwa Penelope na hapo ndipo neno smartphone likachipuka. Simu hii ilikuwa na uwezo ambao pengine unaweza kusema ni sawa na ule wa kompyuta. Baada ya hapo makampuni mengine mengi nayo yalianza kutengeneza smartphones, mfano BlackBerry, Nokia, Palm, Dell, HP na kadhalika. Miaka imesonga na tumeona mabadiliko mengi sana katika fani hii ya teknolojia, makampuni yanayotengeneza smartphones ni mengi sana kwa sasa, Operating Systems za simu hizi nazo zipo nyingi, watumiaji wa simu hizi nao wanaongezeka kila siku. Karibia kila mtu anamiliki simu hii.
iPhone 6 upande wa kulia ikiwa na iPhone 5S.



Pamoja na hayo yote. Ubora ni swala la kuzingatia sana, ni vipi mtengeneza smartphone hiyo amekuwa mbunifu, amezingatia viwango vinavyotakiwa, amejali vipi wateja wake kutokana na hatari au madhara yanayoweza kutokana na utumiaji wa smartphone hizo na mambo mengine ya kuzingatia. Katika nyakati hizi vinara wakubwa katika biashara ya smartphones ni Samsung na Apple, wakifuatia na kampuni nyingine kama Htc, Sony, Huawei na hawa wengine wanaobaki kama Nokia, Jolla, BlackBerry na msururu mrefu wa majina ya kampuni wanagawana asilimia ndogo inayobaki katika soko la smartphones, maarufu kwa jina la "small players".

Mara kadhaa nimesoma na kuona makala mbalimbali za wataalamu wa teknolojia hii na pia malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa smartphones zinazotumia Android OS, Samsung akilalamikiwa kwamba battery za simu zake hazina kiwango na mara kadhaa zimelipuka wakati wa utumiaji wa simu hizo na kupelekea kuhatarisha maisha yao. Htc analalamikiwa kwa utengenezaji hafifu wa simu zake pengine kuonekana kupuuzia swala hili, simu zao zinakuja zikiwa na matatizo ya hapa na pale(hardware defects). Hayo ni baadhi ya malalamiko yanayohusisha upande wa hardware lakini bado kuna mengi katika software, kampuni kama Huawei na LG zina muonekano mbaya sana wa software katika smartphones zao(User Interface). Hivi ni vitu ambavyo ni kawaida kukumbana navyo katika ulimwengu wa Android. Usishangae kutumia milioni kununua simu na baada ya wiki battery inaanza leta shida, ni ngumu kutegemea kitu cha thamani yote hiyo kupata tatizo hilo.


Hali ni tofauti kwa kiasi fulani katika ulimwengu wa Apple, vitu vingi nilivyotaja mapema katika Android OS ni nadra sana kuvikuta katika smartphones za Apple. Mimi sio mpenzi wa iPhones, ninavutiwa sana na Android OS na BlackBerry lakini napenda kuwa mkweli pale ninapoona kuna ubora katika upande wa pili wa ukuta.  Nadhani "kama Steve Jobs asingetuletea iPhone basi leo tungekuwa tuna smartphones mbaya mno", ikumbukwe kwamba mfano(prototype) wa kwanza kabisa wa simu ya Android ulikuwa unafanana wa BlackBerry, Google alibadili prototype hiyo mara baada ya kuona iPhone, na ndipo akaja na HTC Dream. Unaweza ona kuna pengo hapo katika suala la ubunifu kwa upande wa Google ambao ni wanamiliki Android OS. Ukitazama kwa makini mabadiliko makubwa sana ya smartphones yameanzia mnamo mwaka 2007 ambapo iPhone ya kwanza ilizinduliwa na ndiyo ilikuwa simu ya kwanza yenye full capacitive touchscreen. Baada ya hapo makampuni yote yakafata mkondo huo, na vitu vingine vingi vya software ambavyo Apple aliviweka katika iPhone vilianza kuonekana katika smartphones nyingine kama za Samsung na LG ambazo zinatumia Android OS. Kuiga si kitu kibaya, lakini swala ni kwamba unaiga kwa namna gani,  bila ubunifu wako? kama jibu ni hapana basi hapo ubaya ndo unaanzia.

Kwa miaka mingi kampuni ya Apple imekuwa na mapokeo chanya katika nyanja ya teknolojia ya mawasiliano, na pia imetoa mchango mkubwa sana katika teknolojia hii. Simu za iPhones na tablets za iPad zimesaidia sana kuongeza msukumo wa ushindani na ubunifu katika soko la smartphones, kampuni kama Samsung kila siku, usiku na mchana inafanya tafiti ili kuleta kile kilicho bora katika soko la teknolojia na lengo lao hasa ni kumzidi Apple. Kwa upande wake Apple nae anajitahidi kadiri anavyoweza kuwa tofauti na wenzake anaoshindana nao katika biashara.

Kwa sasa smartphone ya Apple iliyo ya kisasa(latest) ni iPhone 5S na mwezi huu tunategemea kuiona iPhone 6 ikizinduliwa. Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni kuhusu simu hii, picha nyingi zimevuja mtandaoni zikionesha ni jinsi gani itavyokuwa(physical features) na hata sifa(specifications) zake zinafahamika tayari. iPhone 6 itakuwa katika aina mbili tofauti, yenye display ya inchi 4.7 na ile yenye inchi 5.5(hii unaweza kuiita phablet). Apple ameamua kuongeza ukubwa wa display za simu zake ambapo iPhone 5S ina ukubwa inchi 4 tu, ingawa suala hili limeonekana kutowafurahisha watu wengi ambao ni wapenzi wa simu hizi za Apple. Wataalamu wengi wa teknolojia ya smartphone wanasema ya kwamba simu hii italeta mabadiliko makubwa sana ambayo hawadhani kama yamewahi kutokea kabla.

iPhone zilizopo kwa sasa zinalalamikiwa kwa kuwa utunzaji mbovu sana wa chaji, hazikai na chaji kwa muda mrefu ukifananisha na simu za Android kama LG G2,HTC One M7na M8 n.k, izingatiwe kwamba unapotaka linganisha iPhones na simu za Android, kwa upande wa Android ni lazima uangalie simu za hali ya juu(high end devices) tu, kwa sababu Android ana low end(za kiwango cha chini),midrange(katikati) na high end(kiwango cha juu) ambapo iPhones zote ni high ends. Lakini tatizo hili linaonekana ukomo wake ulifikia kwenye iPhone 5s , iPhone 6 itakuwa ni ya tofauti kabisa.

Ni kwanini ninadhani ya kwamba iPhone 6 itakuwa ni smartphone bora sana. Ukiangalia kwa upande wa hardware, itakuwa na kioo kinachozuia display kuharibika cha material ya madini ya Sapphire, madini haya yana sifa ya kuwa na ugumu wa hali ya juu sana. Ni madini ya tatu kwa ugumu hapa duniani, Almasi(Diamond) ikiwa ya kwanza. Mpaka sasa ni simu moja tu iliyopo sokoni inayotumia kioo cha aina hii, inafahamika kwa jina la Kyocera Brigadier. Hata hivyo simu hii haina umaarufu sana ni kwa ajili ya watumiaji wa Marekani tu. Sapphire protection itazuia kabisa matatizo ya kuvunjika kirahisi kwa display za smartphones za iPhones, hii ina maana mtumiaji wa simu ya iPhone 6 hatokuwa na shaka pale atakapo angusha simu yake, ni ubunifu bora sana. Smartphone hii itakuwa na uwezo wa Near Field Communication(NFC), hii ni aina ya sensor katika simu na hutumika hasa katika kuhamisha taarifa mfano. contacts, picha n.k katika simu moja kwenda kwenye simu nyingine kwa kuzigusanisha simu mbili zikiwa zimepeana migongo kila mmoja, unatakiwa kufanya hivi kwa sababu sensor hiyo mara nyingi hukaa nyuma ya simu husika. iPhones zilizopo sasa hivi hazina uwezo huu na hii ndo itakuwa mara ya kwanza katika iPhone 6.
MKBHD akifanyia majaribio moja ya panel za Sapphire zitazotumika katika iPhone 6


Tangu mwaka 2010 ambapo iPhone 4 ilizinduliwa Apple hajawahi ongeza pixel density(PPI) katika smartphones zake, ameifanya karibia vilevile kwa modeli zake zote, si iPhone 4S, iPhone 5 wala iPhone 5S. Ina maana kama anakuja na simu zenye display kubwa inambidi kuongeza resolution ili pixel density ibaki vilevile au iongezeke zaidi. Pixel density na resolution ni vitu vinavyoenda kwa uwiano wa kuongezeka(directly proportional). Pixel density ya iPhone 6 itakuwa ya kiasi cha 416ppi(pixel density per inch), imeongezeka kwa kiasi cha 86ppi ukilingansha na modeli za nyuma ambazo ni takribani 330ppi. Ina maana display itakuwa sharp yenye na yenye rangi zilizo maridadi. Camera itabaki vilevile lakini itaongezeka feature inayoitwa OIS(Optical Image Stabilization), hii inasaidia camera kutoa ubora wa hali ya juu wa picha.

Kitu kingine kinachosubiriwa kwa hamu katika smartphone hii operating system mpya,  itafahamika kama iOS 8. Muonekano wake ni sawa na iOS 7, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo vimeboreshwa hasa katika sehemu ya notifications. iOS 7 haina uwezo wa kuzifanya application ziongee/zishirikiane, mfano upo katika photos application na unataka share picha kwa kutumia Whatsapp, haitawezekana kushare picha ile mpaka ukiwa katika Whatsapp application yenyewe. Ni tofauti katika Android  OSambayo ukiwa katika gallery na unataka share picha au mziki unapobonyeza option ya share inakuletea list ya apps zote zinazoweza share mziki au picha hiyo, katika iOS 7 zinakuja apps zile tu zilizokuja na simu(pre-installed apps) kama Facebook, Twitter, iMessage na email. iOS 8 italeta option kama iliyopo katika Android OS. Kuna feature nyingine ambayo inaitwa continuity na itakuwezesha kuanza kazi katika iDevice moja na kumalizia au kuendelea kwenye nyingine, mfano umeandika makala katika iPhone yako na hujamaliza, unaweza malizia kazi hiyohiyo kwa kuanzia palepale ulipoishia katika iPhone yako kwenye iPad yako au iDevice nyingine yoyote, utahitajika kutumia akaunti moja ya iCloud kwa devices zote hizo.

Tusubiri tarehe 9 mwezi ambayo ndo siku ya uzinduzi wa simu hii. Huu mwezi kuna mambo mengi sana kwa upande wa smartphone world, usiahau pia BlackBerry nae anakuja BlackBerry Passport na Classic, Huawei, Nokia, Asus nao wana vitu vyao vya kuonyesha dunia.

No comments :

Post a Comment