Jul 22, 2014

Tatu bora ya phablets za kununua.

"Phablet" ni jina ambalo hutumika kwa simu yenye ukubwa wa kioo kati ya inch 5.1 na 6.9. Ambapo device zote zenye ukubwa wa inch 7 na kuendelea katika display yake hutambulika kama tablet. Zile zenye inch 7,8.4 na 8.9 hujulikana kama mini-tablets mfano LG G Pad, Nexus 7,iPad mini n.k. Tangu kuja kwa devices hizi zimeonesha kupata mafanikio makubwa, safari yake ilianzia na Samsung Galaxy Note N7000 mnamo mwaka 2011. Tangu hapo tumeona Samsung wakiendelea na utengenezaji ambapo kwa sasa wana Galaxy Note 3 na makampuni mengine mengi nayo hayako nyuma mfano Htc, Sony, LG, Huawei na mengine mengi. Hii inaashiria kwamba zina wateja wengi katika soko. Kuna baadhi ya watu huwa hawapendi device kubwa sana kama zilivyo tablets na pia hawapendi device ndogo sana mfano iPhones au BlackBerry Z10, hivyo wanakuta kwamba phablet ni chaguo lao sahihi kabisa.


Hii ni tatu bora ya phablet ambazo wewe uliye mpenzi wa phablet ingefaa kununua kati ya hizi. Nimeangalia vitu mbalimbali mpaka kupata listi hii, vitu kama battery perfomance, umaridadi wa display(sharpness according to pixel density), utendaji kazi(processing power), camera na vingine vingi. Tunaanzia na namba tatu.


 3. HTC Desire 816



Phablet
hii imezinduliwa mapema mwaka huu pamoja na Htc One M8. Ina baadhi ya sifa ambazo ni za kawaida ukifananisha na phablet nyingine ambazo zimezinduliwa nayo karibu muda sawa. Lakini, kuna vitu ambavyo nimevipenda. Ina uwezo mkubwa sana wa kukaa na charge ambapo katika matumizi mazito mfano kuperuzi katika internet, kupiga picha n.k hukaa hadi masaa 18. Na kama una matumizi ya kawaida unaenda nayo hadi masaa 28,battery yake ina ukubwa wa 2600mAh.
Inatumia micro simcard(hujulikana kama line za kukata), inasupport 4G(Long Term Evolution,LTE), vipimo vyake ni (156.6x78.7x7.9)mm na iko kioo cha ukubwa 5.5inch. Haina pixel density kubwa sana, hivyo haioneshi sharp kama ilivyo kwa Galaxy Note 3 kwa mfano, ina kiasi cha 267ppi. Pamoja na hilo haimaanishi kwamba iko na kiwango cha chini mno, kutumia display ya IPS-LCD imefanya display kuwa clear na iliyo tulivu. Internal memory haijavutia sana, ina kiasi cha 8GB lakini uzuri ni kwamba unaweza weka microSD card(memory card) hivyo hutakuwa na wasiwasi ni wapi utatunza media files zako kama picha,miziki na movies. Processor yake ina uwezo wa 1.6GHz Quad Core(CPU nne) ikiwa na RAM ya 1.5GB, kiwango hicho si kikubwa sana, lakini ni tofauti katika hali halisi, phablet hii iko haraka sana, huwezi amini kama ni 1.6 GHz unaweza kudhani ni 2.3GHz. Camera
ya nyuma ina 13MP lakini haina perfomance nzuri nyakati za usiku, cha kufurahisha kwa wale wanaopenda selfie hii inafaa sana kwa sababu camera ya mbele ina 5MP. Htc wameleta teknolojia mpya katika speaker za simu zao inayoitwa BoomSound, phablet hii ina teknolojia hiyo ambayo inakupa usikivu mzuri sana wakati wa kusikiliza muziki au unapoongea na simu, speaker hizi zina sauti kubwa na yenye ubora maradufu. Phablet hii inafaa ukizingatia bei yake na kilichomo ndani yake. Kama Htc ni brand yako favourite ya smartphone usisite kununua, na kama pia unatafuta phablet ya tofauti ya nafuu, hili ndo chaguo.



 2. LG G3

 Mimi sio mpenzi sana wa simu za LG. Lakini kuna kitu kimoja kinachonivutia sana sana katika simu ambacho mpaka wengine wameamua kunipa nickname na kuniita "Mr. Pixels" kwa jinsi gani ninavyothamini sharpness ya display katika aina yoyote ya smartphone. Na hapa LG wameikata kiu hii mpaka kupitiliza kiasi, display yake ina pixel density ya 534ppi ambapo ndiyo smartphone iliyo sharp na clear kuliko zote mpaka sasa. Nafurahi sana kuona uvumbuzi wa aina hii, hii inaashiria tunaweza kuendelea kupata display zenye ubora pengine zaidi hata ya hapa siku za mbele bila kuathiri battery life au perfomance ya simu. Ina ukubwa wa (146.3x74.6x8.9)mm, ni fupi na pana kidogo kwa Htc desire 816, kioo chake kina ukubwa wa inch 5.5 ikitumia teknolojia ya TRU-HD IPS display.
Ipo katika version mbili, ile yenye internal memory ya 16GB ina RAM ya 2GB na ile yenye 32GB ina RAM ya 3GB ila zote hizi mbili zina processor yenye uwezo wa frequency ya 2.5GHz ikiwa ni quad core. Nayo pia inatumia micro sim(line ya kukata) ikiwa na version yenye 4G LTE kwa baadhi ya masoko(market dependent). LG siku zote wanajua tengeneza camera yenye ubora, phablet hii ina camera yenye sensor ya 13mega pixels(MP) na ikiwa na camera ya mbele yenye 2.1MP. Battery iko poa sana, ikiweza kukupa hadi masaa 23 ya matumizi mazito ya kila siku. Ina uwezo wa 3000mAh, imeizidi Htc Desire 816 kwa 400mAh lakini kugundua utofauti wao unapozipambanisha kwa swala la battery ni ngumu kidogo. Kitu kimoja ambacho sijawahi furahishwa na hawa Wakorea ni muonekano wa user interface(UI), imekaa kitoto sana(too cartoonish), na katika hii simu kwa kiasi fulani wameweza badili vitu fulani lakini bado mabadiliko makubwa yanahitajika.


1. Sony Xperia Z2

Naweza kuonekana wa ajabu, lakini mapenzi yangu ya dhati katika smartphone game yapo katika BlackBerry, tangu BB OS 4.5 mpaka leo tupo kwenye BB 10 OS. Watu wanasema tu, lakini hawajui undani wa simu hizi na matumizi yake, moyo wangu huwa unajisikia upo nyumbani. Android ni playground kwangu, na playground hii ni Sony peke yake ndiye aliyewahi kunipa kila kile ninachokitaka katika smartphone na itabaki kuwa hivyo. Tangu Xperia line imeanza sijawahi kuona user interface(UI) iliyo na mvuto,maridadi wa rangi na iliyo ya kipekee. Ndio maana Xperia Z2 na namba moja ya phablets bora za kununua katika listi yangu.

Ina sifa ya pekee ukilinganisha na phablets nilizotaja awali, inazuia maji na uchafu kuingia ndani(water and dust resistant), haiishii hapo tu camera yake ina sensor yenye mega pixels 21. Kiasi kikubwa sana, picha inayotoka hapa ni yenye ubora wa hali ya juu sana. Phablet inafaa sana mtu ambae anapiga picha kwa matumizi kama kuedit kwa ubora n.k. Ni ndogo kwa size ya display ukilinganisha na Htc Desire 816 pamoja na LG G3, ina ukubwa wa umbo wa (146.8x73.3x8.2)mm, haijachukua ushindi wa kuwa nyembamba(slim) katika listi hii, ushindi huo ni wa Htc Desire 816. Display yake ina 424ppi, unaweza kuona ni ndogo kwa kulinganisha na LG G3 lakini bado kioo chake kipo very sharp chenye rangi nyingi zenye ubora(rich colors), hii ndo kazi ya Bravia Engine. Internal memory ni 16GB huku ikiwa na RAM ya 3GB pamoja na processor yenye uwezo wa 2.3Ghz. Battery kwa hapa ndiyo kubwa kuliko zote ikiwa na uwezo wa 3200mAh, amini usiamini,unaweza tumia simu hii na kujikuta unaisha na siku mbili mpaka ukasahau kama ni smartphone kwa jinsi ilivyo na uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kwa muda mrefu.

Ni uamuzi wako kuchagua ni ipi kati ya hizi phablet itafaa kulingana na matumizi yako. Kama wewe ni mtu wa kupenda kupiga picha kila tukio linalotokea mbele yako, Xperia Z2 ndiyo chaguo. Unataka screen yenye pixel density kubwa ili uangalie movies na picha katika ubora wa juu zaidi na pengine uweze kujisifia kwamba una simu yenye sharpest screen to date, LG G3 inakungoja na pia kama unataka phablet inayokaa na chaji kwa muda mrefu itayokamilisha kazi zako za kila siku, Desire 816 ndo partner wako katika hilo.

No comments :

Post a Comment