Sep 10, 2014

Most of us are dissapointed.

"Wengi wetu tumesikitishwa", hivyo ndivyo kichwa cha habari kinavyosema. Siku chache zilizopita niliandika makala kuhusu ni vipi na kwanini iPhone 6 itaweza badili muonekano wa teknolojia ya smartphone. Bahati mbaya sana hili limekuwa tofauti, vitu vingi tulivyotegemea kuviona katika simu hizi mbili za iPhone 6 hatujaviona! iPhone 6 4.7 inch inakatisha tamaa kabisa, battery yake ni karibia na ileile iliyopo katika iPhone 5S. Pixel density ni ile ile ya iPhone 5S hadi iPhone 4, hakuna tofauti kubwa sana katika smartphone hii zaidi ya kuwa na display ya ukubwa wa 4.7inch, processor yenye uwezo zaidi na mengine baadhi. Hakuna display ya Sapphire katika model zote mbili, wametumia Gorilla Glass ambayo wanatumia tangu kuanzishwa kwa iPhone. Labda kwa iPhone 6 plus, angalau kuna vitu vya kuvutia. Display yake ni Full High Definition(HD), 1080p resolution. Camera ina Optical Image Stabilisation(OIS) na pixel density yake ina kiasi cha 401ppi(pixel density per inch). Uwezo wake wa battery ni mkubwa kuliko iPhone 6 4.7 inch.



Ninadhani iPhone 6 Plus ndiyo simu bora kati ya hizi mbili, iPhone 6 4.7 ni sawa na iPhone 5S 2, si hatua moja kwenda nyingine bali ni maboresho katika hatua ileile, mabadiliko ni madogo sana. Si iPhone tu zilizozinduliwa jana, iWatch, smartwatch ya Apple nayo ilizinduliwa, hii imetumia Sapphire display katika kioo chake. Hivi ni vitu vichache baadhi nilivyoviona kwa haraka haraka kuhusiana na event nzima ya Apple. Makala zaidi itakujia siku chache zijazo. 

No comments :

Post a Comment