Sep 13, 2014

Baadhi ya mambo unayoweza fanya ili kuepuka kununua smartphone feki.

Watu wengi hujikuta katika wakati mgumu pale wanapohitaji kununua smartphone, haijalishi ni kwa mara ya kwanza au wanapotaka upgrade kutoka smartphone moja kwenda nyingine. Hali hii huja kutokana na kuwa na maswali mengi akilini, Operating System gani inayofaa?, smartphone ipi ina camera bora?, ipi yenye battery inayodumu muda mrefu baada ya kuchaji mara moja tu?, brand ipi ina reputation nzuri katika soko?, hayo ni mambo machache tu, yapo mengi sana. Lakini kuna jambo moja ambalo wengi wetu tulio wanunuzi wa simu hutakiwa kujiuliza, na pengine kushindwa kuzingatia swali hili inaweza leta huzuni na masikitiko makubwa katika manunuzi yetu. "Je! smartphone ninayotaka kununua ni original?". Nitaeleza njia baadhi unazoweza kutumia ili mwisho wa siku katika manunuzi yako jibu la hili liwe "NDIYO" .


1. Sehemu unapofanyia manunuzi.

Hili ni moja ya jambo la kuzingatia sana, kila mtu katika eneo analoishi hujua ni sehemu ipi wanapouza vitu vya kielectroniki ambavyo si original na pia wapi unaweza pata vitu original. Kama huna uhakika katika kujua ni duka lipi linalouza simu original ni bora ukaenda katika mawakala waliothibitishwa kuuza simu husika. Maduka haya hutangazwa katika redio, kwenye TV, mabango ya barabarani, katika mtandao n.k. Pia kama unamfahamu mtu mwenye kufahamu sehemu zinapouzwa simu original ni bora kumuuliza mtu huyo. Siku hizi kuna smartphones feki hasa za Android ambazo zinafanana kabisa kimuonekano na original smartphones, hasa simu za Samsung. Kama hauna ufahamu wa kujua duka wanalouza simu original na unanunua duka lolote tu lililo mbele ya macho ni rahisi sana kuangukia katika mikono ya simu feki. 

2. Kutumia code special kufanyia majaribio ya simu.

Kujua duka au wakala anayeuza smartphone original si jambo la kutosha kukuthibitishia wewe kupata smartphone original. Mfumo wa simu za kawaida(features phone) mfano. Nokia 105(maarufu kama Nokia Tochi) ni tofauti kwa kiasi kikubwa na smartphones. Smartphones zina vitu vingi sana katika utengenezaji wake, zina sensors mbalimbali ambazo hutumika katika simu kwa matumizi tofauti. Inatakiwa unaponunua simu hii sensors zote ziwe zinafanya kazi, ni ngumu kujua kama sensors hizi zinafanya kazi vizuri au la kuangalia simu kwa juujuu. Kila mtengeneza smartphone hutoa code maalumu ambayo utatumia kuona taarifa mbalimbali zinazohusiana na smartphone hiyo na pia kuweza fanya majaribio mbalimbali katika kujua kama simu hiyo ni original. Kuna baadhi ya smartphones feki zitazoweza kukupa taarifa mbalimbali utapoweka code hizi, si sensors zote zitakubali, na inatakiwa majaribio yote yafaulu, likifeli hata moja ujue simu hiyo aitha ni feki au ni original lakini ina matatizo(manufacturing defects), hufai kuinunua. Hizi ni baadhi ya code unazoweza tumia.

  • HTC *#*#3424#*#*
  • Sony *#*#7378423#*#*
  • Samsung *#0*# au *#0589#(kupima sensor ya mwanga) au *#0588#(kupima proximity sensor)
  • LG 2945#*# au 2945*#01*#
  • Huawei *#*#4636#*#*
  • Kwa simu za BlackBerry zinazotumia BlackBerry 10 OS mfano. Q10,Q5,Z3 n.k, hautatumia code bali katika menu kuu ya simu itakutana na app inaitwa BBVE(BlackBerry Virtual Expert), hapa utaweza kuona taarifa mbalimbali kuhusu smartphone yako na pia kutest sensors zote pamoja na touchscreen.
3. Kuangalia muonekano wa Operating Software(OS).

Kama una ufahamu kidogo tu katika smartphone, muonekano wa OS ya simu utakupa jibu kama ni original au feki, hata kama mtengeneza simu feki kaweka kila kitu katika muonekano wa OS(User Interface, UI) unaofanana na simu original ila bado kuna vitu vitashindikana kuwa performed, mfano kuiconnect simu kwenye server ya mtengenezaji halali wa simu pale unapotaka update software au kutuma error report, kwa simu feki zote swala hili haliwezekani. 

4. Kuangalia muonekano wa nje(physical appearance).

Njia ya nne na ya tatu zinahitaji kidogo kuwa na uelewa katika smartphones ndipo itakuwa rahisi kuweza kutambua kiurahisi ipi ni smartphone original na ipi ni feki, simu nyingi feki hutengenezwa kwa malighafi hafifu sana, mfano plastiki yake huwa ni ya kiwango cha chini maandishi ya logo huandikwa yakiwa yamefifia na hata display huonekana isiyo ya kuvutia kabisa. Camera yake huwa ni ya kawaida, mfano Samsung Galaxy S4 na Note 3 feki huwa na kamera yenye megapixel 3.2, ambapo simu original hazina uwezo mdogo kama huo, utapopiga picha itatoka hafifu sana(blurred). Unapopata mashaka na muonekano wa nje wa smartphone, asilimia ni kubwa sana kwamba smartphone hiyo ni fake.



No comments :

Post a Comment