Mar 4, 2014

BlackBerry; ana mpango wowote wa kurudi tena kutengeneza tablets?

Ni takribani miaka mitatu imepita tangu BlackBerry alipozindua tablet yake ya kwanza iliyokuwa ikijulikana kwa jina la BlackBerry Playbook, kipindi hicho kampuni hii ikijulikana kama RIM BlackBerry ambapo sasa inafahamika kwa jina moja tu, BlackBerry. Tablet hii haikufanya vizuri katika soko na mnamo mwaka jana mwezi wa sita utengenezaji wa modeli zote za tablet hii ulisitishwa jumla. Sababu zilizochangia kutofanya vizuri ni kukosa mvuto, kuwa na apps chache katika store yake, na hata ughali wake pia. Muda zinazinduliwa tablets za iPad ndizo zilizokuwa zimeshikilia soko kisawasawa, Playbook hazikuweza kuonyesha chochote cha zaidi ambacho ni kipya na kizuri kitachowezesha watumiaji wa iPad kuhamia kwa Playbook, au wale ambao ni wapya kutaka kujaribu tablet hii.
BlackBerry Playbook

Pamoja na hayo yote yaliyotokea kipindi cha chuma, historia haimzuii BlackBerry kurudi katika tablets. Hali sasa ni tofauti ukilinganisha na mwaka 2011 ambapo tablet aina moja tu ndiyo ilikuwa ikitamkwa midomoni mwa watu, iPad. Sasa! karibia kila kampuni linalotengeneza smartphones pia linatengeneza tablets. Google anatengeneza Nexus 7, Samsung anatengeneza line ya Galaxy Tab, Microsoft anatengeneza Windows Surface RT tablets, Amazon nae akiwa na Kindle Fire na wengineo wengi. Hii ina maana soko la tablets linalipa kama ilivyo kwa smartphones, wachambuzi wengi wa teknolojia wanasema ya kwamba mwaka huu mauzo ya tablets yanaweza kuzidi mauzo ya kompyuta za kupakata(laptops), unaweza kuona ni jinsi gani soko la tablets lilivyochangamka.

Kama BlackBerry akija na tablet ambayo ni bora, yenye utofauti na pia inayoenda na wakati. Ataweza kufaidika sana kutokana na mauzo. Pamoja na kwamba si kitu rahisi lakini wakiwa na mipango madhubuti wanaweza kuteka soko. Mtandao wa Pocketlint ulifanya mahojiano na Makamu Rais wa bidhaa kimataifa wa BlackBerry, alipoulizwa "Je! mna mpango wowote wa kuleta Playbook nyingine?" alijibu "ndiyo". Aliulizwa swali lingine "Tutaiona katika miezi ya usoni?" alijibu "hapana". Makamu huyu aliendelea kwa kusema, usishangae siku tunaitisha kikao na mnaniona nimeshika tablet yetu mpya, ila kwa sasa hatupo tayari tunahitaji muda mrefu kujiweka sawa.

Muda huu BlackBerry anautumia kujiweka sawa. Anachokiweka mbele kwanza ni kuliweka soko la smartphones za BB10 OS kuwa imara, katika mkutano wa Mobile World Congress walionyesha smartphones mbili ambazo zitakuwa na bei nafuu zinazotumia Operating System ya BB10,smartphones hizo ni BlackBerry Z3 na BlackBerry Q20. Simu hizi ni za kwanza tangu BlackBerry kuingia mkataba na kampuni ya Foxconn. Pengine mwaka huu BlackBerry wanaweza kuona mafanikio kiasi kwa kutengeneza simu ambazo ni nafuu na pia ukizingatia operating system ya BB10 inasupport apps za Android kwa kupitia Android Runtime(ART) ambayo inakuja na update ya software ya BB OS10.2.1.

No comments :

Post a Comment