Jul 19, 2014

"Nokia kutengeneza Android smartphone", sahau kabisa habari hii.

Hapo mwaka jana mwezi wa septemba kampuni ya Microsoft ilitangaza kuinunua kampuni ya Nokia. Lakini ununuzi huu unahusisha kununua kampuni nzima kama ilivyo, ina maana Microsoft ananunua upande wa huduma na pia wa vifaa venyewe(services and devices). Sasa, dili hili limekamilika na Microsoft anapiga kazi akiwa na Nokia katika umiliki wake, kwa sasa CEO wa Microsoft ni Satya Nadella aliyechukua nafasi ya Steven Ballmer. Muda wakati dili la ununuzi linatangazwa aliyekuwa madarakani ni Ballmer.



Hii ni habari njema kwao Microsoft, lakini! Kwa wale wapenzi wa simu za Nokia zilizozinduliwa miezi kadhaa iliyopita ambazo zinatumia Android OS, kwao ni majanga. Microsoft ametangaza rasmi ya kwamba hatoendelea kutengeneza simu kama Nokia X,XL n.k ambazo zinatumia Android OS na badala yake simu hizi zitahamishiwa katila line ya simu za Lumia ambazo zinatumia Windows Phone OS. Android sio chaguo la Microsoft katika operating system ambayo wanataka kutumia katika simu zao, na ni kwa sababu wana operating system yao ya Windows Phone OS. Kwa upande mwingine hawataki pia kutumia operating system zaidi ya moja katika utengenezaji wa simu zao, kitu ambacho wanafanya kampuni kama Samsung, ana simu zinazotumia Android OS na pia anazo zinazotumia Windows Phone OS na pengine siku za mbeleni ataleta sokoni simu zinazotumia operating system ambayo anaidevelop yeye mwenyewe inayoitwa Tizen OS.

Tamko hili limekuja siku chache baada ya kuzinduliwa simu mpya ya Nokia inayotumia Android OS inayoitwa Nokia X2. Pengine watumiaji wa simu hizi watakuwa na wasiwasi kwamba hatima yao itakuwaje katika upande wa kupata software updates na mengineyo. Microsoft ametamka ya kwamba ataendelea kusupport simu hizi kwa wale ambao tayari washanunua. Kwa hiyo haina haja ya kuwa na wasiwasi wowote.

Kwa mtazamo wangu, nilisikitishwa kidogo nilipoziona hizi simu kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wake. Sikutegemea, kwa sababu habari za Nokia kuja kutengeneza Android smartphone nilianza zisikia tangu mwaka 2011 na nikajua wazi siku simu hiyo itapozinduliwa itakuwa ni yenye kiwango cha hali ya juu(high end). Lakini hali ikawa kinyume, na line nzima ikasheheni simu za kiwango cha chini na kati(low end and midrange smartphones). Haikuwa mategemeo yangu, nikadhani nitaona simu yenye specs kama za Xperia Z2 au Htc One M7. Haikuwa hivyo, na hii imekatisha tamaa watu wengi pia cha ajabu ni kwamba hazina huduma za Google kama PlayStore, Gmail, Hangouts n.k inakubidi kusideload apps za Android kutoka katika store za Yandex au1mobile market,sidhani kama hilo ni wazo zuri.  Hili pengine limepelekea kuwa na mauzo hafifu na hata Microsoft hajaona kama biashara hii ina mafanikio yoyote. Una mawazo yoyote kuhusiana na hili, usisite kudondosha comment yako hapo chini.

No comments :

Post a Comment