Jan 3, 2014

Siku chache zijazo itawezekana kupiga simu kwa kutumia BBM katika Android na iOS.

BBM katika LG G2
App maarufu ya kuchat iitwayo BlackBerry Messenger(BBM) inazidi kufanya vizuri sana tangu kutambulishwa katika Android na iOS mnamo mwezi wa kumi mwaka jana. App hii iko vilevile kimuonekano(User Interface) na BBM iliyopo katika simu za BlackBerry zinazotumia BlackBerry OS 10. Kuna vitu baadhi ambavyo vinakosekana katika BBM ya Android na iOS mfano kupiga simu kwa sauti(voice call) na kuwasiliana kwa video(video chat).


Kampuni ya BlackBerry imetangaza kuleta huduma ya kupiga simu kwa sauti katika Android na iOS mwaka huu.Haijulikana ni lini hasa lakini kinachojulikana ni kwamba huduma hiyo itapatikana kuanzia mwaka huu.Utaweza kupiga simu kwa kutumia internet na ili kuwezesha hili itakubidi kuwa na internet yenye kasi ya kutosha na pia kifurushi cha data kikubwa.

Hakuna lolote liliongelewa kuhusu kuleta huduma ya kupiga simu kwa video. Huduma hii itakuja baada ya kuwepo kwa huduma ya simu za sauti kwanza.BlackBerry amekuwa taratibu sana mpaka kuja kuifikisha BBM katika Android na iOS,ilichukua takribani miezi mitano kwa BBM kuonekana baada ya tarehe rasmi ambapo app hiyo ilitakiwa kuzinduliwa.Ucheleweshwaji huu ulichangiwa na BBM fake iliyotoka na kusababisha msongamano katika server ya kampuni hii.Ikabidi waanze tengeneza app tena ili kuepukana na tatizo hilo.Si mbaya!watu walisubiri kwa muda mrefu lakini baada ya app kutoka ilikuwa stable sana na watu wengi waliifurahia na mpaka leo watumiaji wanazidi kuongezeka huku kukiwa na maoni chanya kila kona. kuhusu app hii.

Watumiaji wa BBM katika Android na iOS mkae mkao wa kula kwa huduma hii matata kabisa.

No comments :

Post a Comment