Nov 15, 2013

BBM vs Whatsapp katika Android OS.

Tangu BBM imekuja katika Android na iOS imeonesha kupata mafanikio sana,ikiwa downloaded zaidi ya mara milioni 25 mpaka sasa.Kabla ya app hii kuja katika OS ya Android,Whatsapp Messenger ndiyo ilikuwa app inayofanya vizuri sana kuzidi Viber,WeChat na social chatting apps nyingine.

 Tuone BBM inaweza chuana vipi na Whatsapp Messenger katika OS ya Android.

 1.JINSI YA KUJISAJILI.
  •  BBM inatumia email na baada ya kujisajili utapewa PIN maalumu yenye mchanganyiko wa namba na herufi ambazo ni nane,mfano.123CD6F7.
  •  Whatsapp Messenger inatumia namba ya simu katika kujisajili.
 Kwa hapa Whatsapp inazidi BBM katika urahisi wa kujisajili.


2.JINSI YA KUALIKA WATU.
  •  BBM hutumia PIN katika kualika watu,ili kumualika mtu lazima uwe na PIN yake au pia unaweza scan Barcode ya BBM PIN katika simu yake.Utapotuma maombi ya kumualika mtu ana machaguo ya kukubali au kukataa kuchat na wewe.
  •  Whatsapp Messenger hutumia namba ya simu na hauhitaji sana kumualika mtu,pale utapokuwa na namba ya mtu huyo basi Whatsapp yenyewe itaitambua namba hiyo ya mtumiaji wa Whatsapp na namba hiyo itaonekana katika listi ya wanaotumia Whatsapp katika simu yako.
  Whatsapp ina njia rahisi zaidi ya kupata watu wa kuchat nao.


 3.MFUMO WA MALIPO. 

  •  BBM ni app ambayo inapatikana bure katika store za Google Play Store na Samsung Apps na pia hamna malipo yoyote katika kuitumia.
  •  Whatsapp nayo inapatikana bure katika Google Play Store lakini utapoanza kuitumia utapewa mwaka mmoja bure wa kuitumia na baada ya hapo itabidi kulipia dola za Kimarekani $0.99 ambazo ni sawa na shillingi 1600 za Kitanzania kwa mwaka ili kuendelea kuitumia.
 BBM inaonekana ni nafuu zaidi kwa sababu yenyewe ni bure kabisa kwa hivyo hamna usumbufu wa kulipia mara kwa mara.


4.USALAMA.

  •  BBM hutumia PIN maalumu ambayo hii ndiyo kama utambulisho wa mtumiaji na endapo utahitaji kuchat na marafiki basi itabidi uwe na PIN za marafiki hao.Kwa hali hii basi utaweza kuchat na wale tu ambao unawahitaji na hamna mtu ataeweza kuona taarifa zako endapo hana PIN yako au hujamkubalia kuchat nae.
  •  Whatsapp hutumia namba ya simu kama utambulisho na hii hufanya kwamba yoyote mwenye namba yako na ana Whatsapp ataweza kuchat na wewe bila kutuma ombi lolote la kuchat na wewe.
 5.JINSI YA KUCHAT.
 BBM na Whatsapp zina mfumo unaofanana katika kuchat,bali zina utofauti katika muonekano wake wa kuchat ila zote zinatumia mfumo wa sms conversation wa bubbles style.

  •  Katika BBM unapotuma sms utaweza kuona kama ipo delivered kwa kuonesha herufi D na kama imesomwa kwa kuonesha herufi R.


  •  Katika Whatsapp huonesha tu pale sms inapokuwa delivered lakini haioneshi kama sms imesomwa au la.Whatsapp huweza kuonesha kama mtu yupo online au mara ya mwisho alionekana saa ngapi,kitu hiki hakipo katika BBM.

         Katika Whatsapp na BBM pia unaweza kuanzisha kundi ambalo utaweza chat na zaidi ya mtu mmoja.Katika Whatsapp huwezi kuongeza mtu katika chat ambayo tayari unachat na mtu fulani bali katika BBM unaweza fanya hivyo.




 Kwa hapa ni vigumu kidogo kusema nani kamzidi mwenzie kwa sababu kila app ina kitu ambacho app nyingine haina.


 6.MTANDAO.
  •  BBM inatumia kifurushi chako cha data cha kawaida,BBM katika Android na BBM katika BlackBerry 10 hazihitaji BlackBerry Internet Service(BIS).Endapo huna kifurushi cha data cha kawaida basi itatumia salio lililopo katika simu.Inafanya kazi kwenye mtandao wa EDGE(E) au 3G,katika sehemu zenye mtandao hafifu BBM imeonekana kufanya kazi kwa shida sana,huchelewa kutuma na kupokea ujumbe wa sms na kutuma picha au video inakuwa ni vigumu kabisa.
  •  Whatsapp pia inatumia kifurushi cha data au salio,lakini hii inahimili hata sehemu zenye mtandao hafifu,hutumia pia E au 3G.
Whatsapp inahimili matatizo ya mtandao kuliko BBM.

   7 .MIPANGILIO(SETTINGS).

 Vitu vingi katika settings za hizi apps mbili vinafanana kama kuweza kuset notifications,kumanage blocked contacts na vingine vingi.
  •  Katika BBM kuna chaguo la kuona ni muziki gani anaosikiliza mtumiaji mwingine,pia kuna updates kama kujulishwa mtu kabadili display picture au status yake.
  •  Mipangilio ya Whatsapp ipo kimsingi sana.
      
 BBM ina mipangilio mingi kuliko Whatsapp kwa hili inafanya BBM iwe rahisi zaidi kadiri unavyotaka wewe.


HITIMISHO:Kiukweli,siwezi kusema aitha Whatsapp au BBM mmojawao ni mshindi.Kila moja ina vitu vyake vizuri na kila moja ina vitu inavyokosa,Whatsapp inapata kuanzia Android 2.2(Froyo) na kuendelea bali BBM inapatikana kuanzia Android 4.0(ICS) na kuendelea kwa sasa.Lakini zote mbili ni apps nzuri sana za kuchat ambazo zinapunguza gharama ya kutuma sms na kutuleta karibu zaidi.Niambie kwa kutoa comments zako,Unaionaje BBM na pia Whatsapp katika Android Smartphone yako.

No comments :

Post a Comment