Jan 2, 2014

Kuna uwezekano tukaona Sony smartphones zikitumia Windows Phone OS mwaka huu.

Kampuni ya Sony ina mpango wa kuongeza operating system nyingine katika smartphone zake.Kwa sasa Sony anatumia operating system ya Android na simu zinazotumia OS hii zipo katika brand ya Xperia.
Sony Xperia Z,moja ya smartphone maarufu inayozuia maji.

Inasemekana Sony atazindua simu hizi mnamo katikati ya mwaka huu wa 2014.Zitakuwa katika brand ya Vaio.Hapo nyuma kampuni ya Sony ilishawahi kuwa na mifano(prototype) ya simu zinazotumia Windows Phone 7 lakini hazikuwahi kutoka sokoni.

Kampuni hii ya Japan inaonekana kufanya vizuri sana katika upande wa smartphones.Nadhani itakuwa hatua kubwa na muhimu watapoongeza simu za Windows Phone pia.Itaongeza pia mapenzi ya watumiaji kwa simu za Windows Phone.

No comments :

Post a Comment