Jul 10, 2015

Uchungu na Utamu wa Android OS, Hasa kwa Watengeneza Smartphone Hizi.

Kwa miaka sasa, ushindani mkubwa umekuwepo kati ya Android OS (inayomilikiwa na Google) na iOS (inayomilikiwa na Apple. Operating System ya Android ni tofauti kidogo na iOS, Android ni mradi huru (open source project), inatumika na  makampuni mengi yanayotengeneza smartphones (OEMs), makampuni kama Samsung, LG, Sony, HTC, Huawei, Xiaomi na kadhalika yapo katika familia hii. Apple's iOS ni mradi usio na chanzo huru/wazi (closed source project), ni devices za Apple pekee ndizo zinatumia OS hii, kama ilivyo kwa BlackBerry OS.

Apple AppStore, Mpinzani mkubwa wa Android pamoja na
Muungano Huru wake uitwao OHA (Open Handset Alliance)

Kwa mwaka jana, stoo ya apps ya Android OS inayofahamika kama Google Play Store imekua kwa kiasi kikubwa hadi kuipita stoo ya Apple, AppStore. Hii ni faida kubwa kwa Android lakini kuna hasara pia katika familia hii. Watengeneza wa smartphones za Android wanashindana wao kwa wao.

Kila mtengeneza smartphone ya Android anafanya kila awezalo kuhakikisha ana muonekano wa tofauti kuanzia upande wa hardware mpaka software, ili mradi tu afahamike yeye ni bora na tofauti unapomlinganisha na wenzake kuanzia upande wa hardware mpaka software. Unaweza dhihirisha hili kwa kuangalia flagship za Samsung na HTC zilizotoka hivi karibuni, Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge na HTC One M9. Pamoja na yote hayo, bado kuna mambo ambayo hayawapendezi watumiaji wengi wa smartphones za Android.

Samsung, kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa kwa aina isiyo ya kuvutia ya muonekano wa operating software yake (User Interface) ifahamikayo kama Touchwiz UI, si hivyo tu! kisicho cha kufurahisha zaidi kuliko vyote ni uwepo wa applications zake zinazokuja na smartphone (pre-installed apps) ambazo huwezi kuzifuta iwapo huna haja nazo (Bloatwares). Sina maana kwamba ni Samsung pekee mwenye mtindo huu wa kujaza bloatwares katika smartphones zake, ni wote katika familia ya Android OS wanafanya hivi lakini Samsung ndiye kinara wa jambo hilo.

TouchWiz katika Samsung Smartphone

Kwa sasa ametambua tatizo hili, ndiyo maana katika Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge, ameboresha User Interface ya Touchwiz kwa kupunguza bloatwares na kwa pre-installed apps zilizobaki una uamuzi wa kuzifuta endapo utakuwa huna haja nazo.

 Tangu kuja kwa teknolojia ya Virtual Reality, kampuni nyingi zinaanza kujaribu kutengeneza uhusiano wa smartphones zao na teknolojia ya Virtual Reality. Ukiangalia Samsung ana Samsung Gear VR Headset, Sony na Project Morpheus, HTC ameungana na kampuni maarufu ya kutengeneza video games inayoitwa Valve katika kutengeneza headset yake ya Virtual Reality inayofahamika kama HTC Vive. Hali hii inaleta ushindani wa hali ya juu kwa sababu kila mmoja anataka kudhihirisha kwamba yeye anajua design bora katika teknolojia husika.

Samsung Gear VR Headset

Ushindani huu ni hasara na tishio kwa kila mmoja katika familia ya Android, yule anayeshindwa kuvutia soko kwa bidhaa alizonazo ni wazi kwamba mauzo yake yatakuwa hafifu. Lakini kwa sisi watumiaji wa smartphones ni faida kwetu kwa sababu yale yote tusiyoyapenda katika bidhaa tunazonunua yatakuwa yanafanyiwa marekebisho mara moja ili kampuni husika kuepuka kukosa wanunuzi wa bidhaa zake.

No comments :

Post a Comment