Jul 18, 2015

Fahamu uzuri wa kutumia app ya Google Photos.

Google I/O ni moja kati ya matukio makubwa kabisa katika ulimwengu wa teknolojia hasa katika upande wa bidhaa za kieletroniki zinazotumiwa na watu (consumer electronics) hususan smartphones, tablets na smartwatches, bila kusahau internet inayounganisha vitu (Internet Of Things). Ni mkutano unaokutanisha si tu developers bali hata wadau na watu wengine ambao ni wafuatiliaji wa teknolojia kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Google hutumia mkutano huu kutambulisha teknolojia, bidhaa pamoja na huduma zake mpya. Mkutano huu hufanyika kila mwaka katikati ya robo ya pili ya mwaka (mid quarter two).

Makala hii inalenga kuelezea moja ya huduma iliyotambulishwa mwaka huu katika mkutano huo uliofanyika Mei 28 na 29 huko San Francisco, CA, USA. 
Google Photos ni huduma kutoka Google inayowezesha kuhifadhi picha pamoja  na videos, pamoja na kwamba huduma hii sio mpya sana lakini kwa mwaka huu imefanyiwa maboresho makubwa kiasi kwamba huduma hii sasa inakuwezesha KUHIFADHI PICHA PAMOJA NA VIDEOS ZAKO ZOTE BILA MALIPO, BILA KIKOMO (FREE & UNLIMITED).

Kila mtu anaweza kutumia huduma hii kwa sababu inapatikana katika sehemu(platforms) tatu, Android, iOS pamoja na Web nikimaanisha kwamba kama mtu hana smartphone au tablet ya Android, pia akiwa hana iPhone au iPad bado anaweza kupata huduma hii kupitia browser ya kompyuta yake bila kuangalia mfumo (OS) anaotumia (Windows/ Mac OSX/ Linux). 


Kabla ya kuanza kuhifadhi (upload/back up) picha na videos  katika Google Photos mtumiaji hupaswa kuchagua namna ambavyo angeweza kuhifadhi picha na videos hizo, na hapa machaguo yapo mawili;

i. Ubora wa hali ya juu(High Quality)
   Hapa picha na videos zote zitahifadhiwa katika ubora wa hali ya juu, kigezo      kikubwa ni kwamba kama picha hiyo imepigwa katika kamera yenye zaidi ya          MegaPixels 16 na video ipo katika ubora wa 1080p (Full HD) au zaidi basi          itapunguzwa ukubwa wa faili lakini muonekano wake utahifadhiwa vilevile          (retaining visual quality). 
   Lakini kwa picha iliyopigwa kwa kamera yenye 16 MP au chini yake na video        yenye ubora uliochini ya 1080p, vitahifadhiwa bila kupunguzwa. 
   Kumbuka: Hili ndilo chaguo ambalo halina kikomo katika kuhifadhi.

Machaguo kabla ya kuanza upload


ii. Halisi(Original)
  Katika chaguo hili picha na videos zitahifadhiwa kama zilivyo, bila kupunguzwa   ukubwa wake pasipo kujali imepigwa katika kamera yenye MPs ngapi au ipo katika  ubora upi,ila hasara hapa ni moja, hutoweza kuhifadhi picha na  videos unlimited. Hapa utaweza kuhifadhi kulingana na nafasi (storage)    iliyobaki kati ya 15 GB zako katika akaunti yako ya Google.

Huduma hii ya kuhifadhi inawezesha  kuwa na mahali ambapo utaweza kuweka picha na videos zako kiusalama zaidi, huna sababu ya kutembea nazo katika smartphone yako kwa kuwa zinaweza kupotea pia zinajaza nafasi. Sambamba na kuhifadhi, Google Photos pia inakuwezesha kufanya editing na sharing kirahisi. Pia ili kuhakikisha kwamba kila picha au video inahifadhiwa, chaguo la auto back up linapatikana.  


Kama nilivyosema hapo mwanzo huduma hii inapatikana katika sehem tatu

1. Android :App inapatikana PlayStore au Bonyeza HAPA

2. iOS : App inapatikana AppStore au Bonyeza HAPA

3. Web/ Kompyuta : Tumia "https://photos.google.com" au ingia HAPA
  
Google Photos Help Center : HAPA

Je, imekusaidia? Hakikisha inamsaidia na rafiki yako pia,  Share!!  & Comment!!


twitter : Afgreen Wireless @afgreenwireless

facebook : Afgreen Wireless

No comments :

Post a Comment