Jul 21, 2015

Fahamu Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Katika PC Yako

Siku si nyingi katika blogu hii tuliandika kuhusu namna ya kupakua videos za Youtube katika smartphone ya Android kwa kutumia app ya OGYoutube,  Unaweza kusoma makala nzima "Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Ukiwa na App Inayoitwa OGYoutube" HAPA. Kwa upande wa PC, tulielezea kwa kugusia tu. Makala hii itakuelezea namna rahisi ya kupakua videos kwa upande wa PC kwa undani zaidi.

Katika makala iliyopita tuliandika namna ambavyo watumiaji wa PC hupakua videos hizo, tuligusia program maalum kwa kazi hiyo kama vile Internet Download Manager (IDM) na  Free Youtube Downloader kutoka Wondershare. Pia njia nyingine ya kupakua videos hizo ni kuweka extensions kwenye browser ambazo zinafanya kazi hiyo, extensions hizi zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome (Chrome Webstore) kwa ajili ya browser ya Chrome lakini pia hata variants zake zinanufaika na store hiyo, pia kwa wale watumiaji wa Firefox, extensions (add-ons) zinapatikana kupitia Menu kuu ya browser hio.

Hapa ningependa kuelezea njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi katika kupakua videos za Youtube, ambayo haihitaji program ya nje kuongeza uwezo wa browser wala haihitaji extension yoyote, njia hii ni kupitia browser yenye uwezo wa ndani (built-in functionality)  wa kupakua videos hizo, na browser ninazozungumzia hapa ni Baidu Browser pamoja na Spark Security Browser. Hizi ni browser mbili ndugu, nikimaanisha kwamba zote zinatengenezwa na kampuni moja, Baidu Global.

Ni rahisi kupakua videos kwa kutumia browsers hizi, kwa upande wa juu kulia ndipo vinapokaa vifaa (tools) za browser hizo, tofauti moja kubwa kati ya browser ndugu hizi ni kwamba katika toleo la hivi karibuni la Baidu Browser (version number 43) uwezo wa kupakua torrents umeondolewa, hivyo kama ungependa kutumia browser hizi kwa kupakua torrents chagua lililobaki ni kutumia browser ya 
Spark Security Browser. Ndiyo, unaweza kutumia browser hiyo pia kwa kupakua torrents moja kwa moja katika PC yako.

Namna Ya Kutumia Browser Hizi. 

1. Kwa kupakua videos, sehemu inayohusika ni Media Download, Baada ya mtumiaji kuwa katika video husika anayotaka kuipakua, Media Download itakupa tangazo kwamba imegundua kuwa kuna video ya kuipakua. Bofya hapo.


Muonekano wa Baidu Browser 

2. Orodha ya video zote zinazopakuliwa na zilizopakuliwa zinahifadhiwa kwenye Download Manager.

Baidu Browser baada ya kugundua video

3. Kwa wanaopenda kutumia browser hii kwa kupakua torrents, ni rahisi. Nenda katika torrents husika unayotaka kuipakua, kisha bonyeza sehemu ya kupakua torrents hio (Download Torrent) kisha browser husika itagundua na itakupeleka mahali ambapo ungependa kuhifadhi faili hilo la torrent.


Mwonekano wa Spark Security Browser

Pakua (Download) Baidu Browser HAPA au tembelea HAPA

Pakua (Download) Spark Security Browser HAPA au tembelea HAPA




Je, imekusaidia? Hakikisha inamsaidia na rafiki yako pia,  Share!!  & Comment!!


twitter : Afgreen Wireless @afgreenwireless

facebook : Afgreen Wireless


No comments :

Post a Comment