Mar 9, 2015

Umuhimu wa smartphone yenye battery inayoweza kutolewa(removable battery).

Watu wengi wanatumia smartphones kwa shughuli mbalimbali, iwe ni kuperuzi mtandaoni, kusikiliza muziki, kupiga picha, kutuma barua pepe au kuchati. Yote haya hutumia nishati kubwa sana ya umeme katika smartphones. Simu hizi hazina uwezo mkubwa wa kuhimili kukaa muda mrefu ikiwa na nishati huku ukiitumia mfululizo. Hii inapelekea uhitaji wa kuipa nishati(recharge) smartphone yako mara kwa mara. Ukiwa ofisini, nyumbani au popote pale palipo na umeme suala la kuchaji simu ni rahisi tu. Lakini inakuwaje upo porini, au sehemu yoyote iliyo haina umeme kabisa na hauna nishati yoyote mbadala?

Si tu uwe katika sehemu isiyo na nishati ya umeme ndipo ushindwe recharge simu yako, kuna wakati umeme hukatika, na suala hili ni kawaida. Ina maana kwamba utakwama katika shughuli uliyokuwa ukifanya. Ni afadhali ukiwa unasikiliza muziki, utaburudika tena baadaye lakini isiwe ni wakati ambao ulikuwa ukisubiri simu muhimu sana na hauna mbadala wa kupata tena mawasiliano. Lakini, pengine ungekuwa simu yenye uwezo wa kubadili battery(removable battery) ungeweza kuepuka zahama hii.
Wengi ya watengenezaji wa smartphones walio na majina makubwa kama HTC, LG, Sony, Apple, Huawei, Microsoft na Xiaomi wanaelekeza nguvu zao nyingi katika kutengeneza simu zilizo na battery isiyoweza kutolewa(non-removable battery) kuliko zile zenye battery ya kutolewa(removable battery). Hutamba ya kwamba simu zao zilizo za hali ya juu(high end smartphones) zina uwezo mkubwa kwa kukaa na charge kwa mrefu, muda wenyewe ni masaa, sio siku kadhaa. Kwa hiyo usitegemee kukaa na smartphone yoyote ile ukiitumia sana na ukategemea itakaa na wewe kwa siku mbili bila kuonyesha taarifa(pop-up notifications) kwamba inahitaji chaji au kukwambia inakwenda kuzima. Samsung yupo tofauti kidogo, simu zake za hali ya chini(low end smartphones) mpaka za hali ya juu(high end smartphones) zina battery inayoweza kutolewa. Ni suala la kubadili tu battery na kuendelea na kazi zako kama una battery ya ziada. 


BlackBerry Z10 ina uwezo wa kubadili battery, lakini BlackBerry
si chaguo kwa walio wengi.
Ukiwa na smartphone iliyo na battery inayoweza kutolewa, kiukweli faida ni kubwa. Pale battery unayotumia inapochoka, ni suala la kununua nyingine na kubadili mara moja na smartphone yako inarudi katika hali yake ya kawaida. Tofauti na simu isiyoweza kutolewa battery yake, itakubidi kulipia pesa nyingi katika kupata battery nyingine na huwezi badili mwenyewe mpaka upate mtu mwenye utalaamu wa kubadili battery hiyo. Na sio tu kwamba kulipia pesa nyingi katika kubadili battery husika, nyingi ya battery hizi huwa hazitengenezwi na kampuni iliyotengeneza smartphone husika na ubora wake huwa haufanani na ule wa battery halisi ya mtengeneza smartphone hiyo. Kuna mambo ambayo si muhimu san kuzingatia katika chaguo la smartphone ambayo mtu anataka nunua mfano rangi yake, umaridadi wa display na mengineyo, haya si mambo ambayo kila mtu hujali. Inapofika suala la battery bora yenye uwezo kila mtu hujali sana.

Sijataja mibadala mingine ambayo inakuepusha na kero ya simu kuzima kila mara kwa sababu ya kuisha chaji.......Power Bank, Huwa sioni kama mbadala bora kwa sababu huongeza mzigo mwingine usio wa ulazima. Inakubidi kubeba simu na power bank kwa wakati mmoja, huondosha uhuru katika matumizi ya simu yako. Battery ya ziada haileti usumbufu wowote zaidi ya kubadili na kuendelea na kazi. Kuna baadhi ya kava za simu ambazo na battery ndani yake inapatia simu yako nishati, hizi kava huwa nene na huongeza uzito katika smartphone, na kuna watu wengine wasiopendelea kabisa kuweka kava katika smartphone, bila shaka hawatotumia kava hii. 

No comments :

Post a Comment