Mar 20, 2015

Facebook Messenger, inataka kuwa M-PESA ya dunia.

Karibia wamiliki wote wa simu nchini hutumia huduma za kipesa kama M-Pesa, Tigopesa, Airtel Money na zinginezo kuweza pata huduma za kutuma na kupokea pesa, na siku hizi inawezekana hadi kutunza pesa zako katika huduma hizi, huduma kama M-Pawa iliyopo katika M-Pesa inakuwezesha kufanya muamala huu. Huduma za kibenki hazitumiki sana kama ilivyokuwa zamani, na hasa pale linapokuja suala la kuhitaji kutuma na kupokea pesa kwa urahisi zaidi na kuokoa muda wako.


Unaweza linda muamala huu kwa Touch ID katika devices za iOS.




Huduma nyingi za simu nilizotaja hapo juu ni maarufu katika nchi nyingi za Afrika, na ndipo pia zilipozaliwa. Nchi zilizoendelea kama Marekani na nyinginezo wanatumia huduma za tofauti kidogo, ingawa kuna baadhi ya nchi mfano zilizopo Ulaya Mashariki zimeanza kutumia huduma zinazofanana na kama tunazotumia sisi.

Google Wallet, Paypal, Amazon Payments na kadhalika ni huduma maarufu za mtandao zinazotumika katika nchi zilizoendelea. Facebook, mtandao wa kijamii maarufu sana duniani nao unajikita katika kutoa huduma za malipo kama kampuni nilizotaja hapo juu. Lakini kuna utofauti kidogo katika namna ambayo Facebook atatoa huduma hii ukilinganisha na kampuni kama Paypal. Huduma ya kutuma na kupokea pesa itatolewa na Facebook kupitia Instant Messenger(IM) app yao inayofahamika kama Facebook Messenger. Utofauti uliopo katika huduma hii ukilinganisha na nyinginezo ni kwamba utaweza kutuma pesa ndani ya chat uliyonayo na mtu husika. 

Huduma hii inafanya kazi kwa namna hii: Katika chat uliyonayo na mtu fulani utaona alama ya "$" ambapo baada ya kuibonyeza utakuambia kuingiza kiasi unachotaka kutuma, kama unafanya huduma hii kwa mara ya kwanza utahitajika kuingiza taarifa za kadi yako ya benki(bank credit card). Na ukiwa wewe ndiyo mtumiwa pesa, utaona ujumbe unaokuambia kwamba umepokea pesa, na utahitajika kuingiza taarifa za kadi yako ya benki ili kukuwezesha kupokea pesa hizo kama unafanya muamala kwa mara ya kwanza, kwa mara zitazofuata hutahitajika kuingiza taarifa hizo tena. 

Utapotuma pesa itahama hapohapo lakini itachukua siku mbili hadi tatu pesa ile kuhamia na kupatikana katika akaunti ya yule uliyemtumia, inategemea na uharaka wa miamala ya benki utakayotumia. Iwapo una wasiwasi kwamba mtu mwingine anaweza chukua simu yako bila ruhusa na kujihamishia pesa, unaweza kuweka namba ya siri(PIN number) ambayo utatakiwa kuingiza kila mara unapotuma pesa. Huduma hii inasupport matumizi ya fingerprint scanner katika devices za Apple kama iPhone 6 Plus. Huduma hii itakuja katika miezi michache usoni, ila itaanzia Marekani na kuendelea kusambaa sehemu zingine duniani kadiri siku zinavyokwenda.

No comments :

Post a Comment