Feb 11, 2015

Tatizo linalosababisha HTC One M7 kutoa picha mbaya katika mwanga hafifu.

HTC One M7, moja ya smartphones bora kabisa za mwaka 2013, ilizinduliwa mwezi machi mwaka huo. Mpaka leo hii, imo katika chati, na kampuni hii ya Taiwan ipo katika mchakato wa kuandaa software update ya Android Lollipop 5.0 kwa ajili ya HTC One M7. HTC One M8 ambaye ni muendelezo wa M7 tayari ameshapata update hii. Pamoja na kwamba ina ubora katika nyanja nyingi ukilinganisha na wapinzani wenzake wa kipindi hicho kama Samsung Galaxy S4 na LG G2. Lakini, kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa. Mikakati ya kuipa nafasi simu hii katika soko la smartphone ilifeli kwa kiasi fulani hali kupelekea mauzo yake kuwa chini sana ukilinganisha na smartphone kama Samsung Galaxy S4 na pia "kamera yake ina matatizo, ambayo ni sugu". Hili tatizo la pili ndilo linalohusu makala hii.


HTC One M7.
"Ultrapixel camera", teknolojia hii ilionekana kwa mara ya kwanza katika HTC One M7. Smartphones nyingi mfano; Samsung Galaxy S5, Sony Xperia Z3 na kadhalika hutumia camera zinazoundwa na pixels zenye kiasi cha  kuanzia 1 hadi 1.4 micrometer. Ultrapixel camera inaundwa na pixels zenye size ya 2 micrometer kwa kila pixel. Kama nilivyosema awali, aina hii ya teknolojia ilikuwa ndo mara ya kwanza kutumika na hivyo ilikuwa ngumu kutambua madhara yake kwa kina kama hutafanya majaribio ya kutosha.



Simu nyingi sana za HTC One M7 zimekumbana na tatizo la kutoa picha zilizo na ukungu wa rangi ya zambarau (purple) na pink, lilifahamika maarufu kama purple tinting

Picha hizi hasa hutokea nyakati za usiku na katika sehemu yoyote iliyo na mwanga hafifu. Tatizo hili linachangiwa na teknolojia ya Ultrapixel pasipo moja kwa moja (indirect). Tambua ya kwamba, unapoongeza size ya pixel katika camera unaifanya kuhitaji mwanga zaidi katika kutengeneza picha iliyo na ubora, tofauti na camera yenye size ndogo ya pixel, itahitaji mwanga kiasi tu katika kupiga picha. Hivyo, camera ya HTC One M7 inapokumbana na mwanga hafifu au katika sehemu isiyo na mwanga, huanza kuhangaika namna ya kupata mwanga ili kutoa picha bora. Sasa, kinachotokea katika hangaiko hili ni matumizi makubwa ya processor yanayopelekea simu kupata joto(overheat). Joto hili hupelekea kuharibu uchukuaji wa picha (distortion) kwa kutengeneza rangi ya zambarau (purple) na pink na mwisho wa siku picha hutoka ikiwa na rangi hizi. HTC alikubali kuwepo kwa tatizo hili miezi sita baada ya uzinduzi wa smartphone hii. Aliahidi kutoa software update ambayo ingeondoa tatizo hili. Kwa bahati mbaya, simu nyingi zilizopokea update hii hazikuepukana na tatizo hilo na ikawa wazi kabisa suala hili ni tatizo la kifaa (hardware problem).

Picha za HTC M7 zinavyotokea nyakati za usiku.

Uzuri ni kwamba si simu zote za HTC One M7 zina tatizo hili. Model za HTC One M7 zilizo na tatizo hili ni zile zilizotengenezwa kabla ya mwezi wa tisa  mwaka 2013. Tangu HTC kutambua tatizo hili na kuona kwamba software update haikuweza kutatua tatizo alibadili mahali anapotengeneza camera kwa ajili ya smartphones za HTC One M7. Modeli zote zilizofuata baada ya mwezi wa tisa hazikuwa na tatizo hili.


HTC One M8 ni muendelezo wa One M7, ikiwa pia inatumia camera iliyo na Ultrapixels, haijakumbana na tatizo la purple tinting. HTC alijifunza na kugundua vitu vya kuboresha na ameweza kufanikisha teknolojia yake katika HTC One M8.
Je, Unamiliki HTC One M7 yenye tatizo la purple tinting?, usisite kushare nasi ni vipi unaongelea tatizo hili kwa kutoa maoni yako.

No comments :

Post a Comment