Feb 19, 2015

Pengine Samsung Galaxy S6 itabadili kasumba ya Samsung.

Samsung, jina maarufu sana unapoongelea vifaa vya kielectroniki(consumer electronics). Smartphones, televisheni, kompyuta, mashine za kufulia, mitambo ya mawasiliano, mashine zitumikazo hospitali n.k vyote hivi hawa Wakorea kusini hutengeneza. Huwa nafurahishwa vile walivyo na mikakati mizuri katika kutangaza bidhaa zao duniani kote. Na morali hii ndiyo inawapelekea kuwa moja ya kampuni kubwa sana duniani zenye mafanikio. Lakini, pamoja na mafanikio yote haya; dosari huwa hazikosekani. Kuna baadhi ya dosari ambazo Samsung anatakiwa kuziangalia kwa kina ili kuweza kuzirekebisha.

Hali ilivyo sasa, nyingi ya flagship smartphones za kampuni kubwa umbo lake la nje linaundwa kwa kutumia metali hasa madini ya Aluminium kwa kiasi kikubwa. Si iPhone 6 Plus,  iPhone 6, HTC One M8 wala Huawei Ascend Mate 7, zote hizi zinaundwa na asilimia kubwa ya madini ya Aluminium ili kuboresha uimara wake. Wengi walitegemea pengine hali itakuwa hivyo hivyo kwa Samsung Galaxy S5, Lakini wapi!. Watumiaji wengi wa smartphones za Samsung wamekuwa wakilalamikia suala hili hasa kuanzia uzinduzi wa Samsung Galaxy S4 mnamo mwezi Aprili mwaka 2013. Malalamiko haya yalichochewa pale HTC alipozindua flagship yake ya HTC One M7 mwezi mmoja baadaye ikiwa na asilimia 70% ya Aluminium katika umbo la nje. Sidhani kama kuna mtu yoyote anayependelea kulipa fedha nyingi kununua smartphone iliyo na plastiki ambayo ni rahisi kuvunjika pale simu inapoanguka.

Sio mbaya sana plastiki ikitumika katika laptops, lakini sio katika high end flagship smartphone kama Galaxy S5.

Hali haikuonekana kubadilika, na Galaxy S5 ilikuja katika mtindo ule ule wa plastiki, tena ya kawaida tu. Lakini Samsung hudai kwamba plastiki yake ni imara sana suala ambalo ni tofauti inapofikia katika uhalisia. Mwisho wa mwaka jana, Samsung alizindua smartphones za Galaxy A5 na Galaxy A3 akidai ya kwamba ni smartphones zinazotumia madini ya Aluminium katika utengenezaji wa umbo la nje. Cha kushangaza, ni upande wa pembeni tu ndiyo Aluminium hii ipo na hata hivyo simu hizi hazina kiwango cha kuwa flagship smartphone. Sifa zake nyingi zipo katika smartphone yenye kiwango cha katikati(midrange smartphone). Kuna tetesi mbalimbali katika mitandao zikielezea ya kwamba Galaxy S6 itatengenezwa na umbo la nje la metali kwa asilimia kubwa, lakini hizi ni tetesi tu na hazijathibitishwa. Tusubiri tuone kama safari hii ataweza badilika ili kuendana na wakati katika hili suala.


1 comment :

  1. Casino in St. Louis - JTM Hub
    A 정읍 출장마사지 casino near Saint Louis is open and excited to 김제 출장샵 welcome players 대구광역 출장샵 back to 전라북도 출장마사지 our gaming floor. 경산 출장마사지 Our gaming floor is a diverse lineup of table games such as

    ReplyDelete