Feb 24, 2015

Njia Rahisi Ya Kuwezesha PC Yako Kuwa Wi-Fi Hotspot

Hotspot ni huduma inayopatikana mahali fulani (physical location) inayomuwezesha mtumiaji mwenye kifaa cha kielectroniki kilicho na uwezo wa kutumia wireless connection, kuweza kujiunga na kutumia internet.  Kwa kifupi, ni mahali ambapo unaweza unga laptop, tablet computer au smartphone yako na kutumia internet bila ya kuunga nyaya zozote (wirelessly). Mara nyingi hotspot hupatikana maeneo kama ya vyuo, mahotelini, sehemu za wazi za kujipumzisha au migahawani. Kutokana na ukuaji wa teknolojia, siku hizi smartphone zina uwezo wa kuwa Wi-Fi Hotspot pia.

Wengi wetu tunamiliki smartphones na hivyo suala la kushare Portable Wi-Fi Hotspot kati yetu ni dogo sana, ni kiasi cha kwenda kwenye settings na kuwasha tu, lakini mambo hayapo hivyo kwenye upande wa kompyuta. Watumiaji wengi wa PC hutumia Wi-Fi kutoka sehemu fulani lakini hukwama pale linapokuja jambo la kuwezesha PC zao kuwa hotspot. Kuwezesha PC kuwa Wi-Fi Hotspot inawezekana, lakini huhitaji utaalamu kidogo katika kuweza fanikisha jambo hili. IIi kufanikisha
jambo hili wengine huchagua kucheza na configuration settings na kuwezesha hotspot "manually" na wengine hubidi kuweka software mbadala kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Si mara zote machaguo hayo hufanikiwa, kwa mfano, software kama Connectify ambayo kazi yake kubwa ni kuwezesha huduma ya hotspot katika PC hukumbana na tatizo la kushindwa kuwa installed katika kompyuta husika kutokana na kukosa vigezo (incompatibility issues). Si hivyo tu, hata wakati wa kuitumia inaweza isikupe kile ambacho ulitarajia, pengine kasi ya internet ikawa ni ndogo.

Upo umuhimu wa kuwezesha PC kuwa na hotspot, kwa mfano,  kwa wale ambao wanatumia vifaa vyenye uwezo wa kutumia wireless connection (Wi-Fi) kama vile tablet au hata simu unaweza kutumia modem kuunga internet kwenye kompyuta kisha kuwezesha kompyuta hiyo kuwa hotspot ili kuunga vifaa vyako pia viweze kutumia internet. Pia unaweza kutumia njia hii kuunga internet kwenye kompyuta zaidi ya mbili pamoja na vifaa vingine kadhaa kutoka katika chanzo kimoja (hotspot).

Njia rahisi na mbadala ya kuwezesha hotspot kwenye PC yako ni kwa kutumia software inayoitwa Baidu PC Faster inayotolewa na Baidu International. PC Faster ni utility software ikiwa na features kama cleaner, antivirus engine na speedup tools bila kusahau feature tunayozungumzia, Wi-Fi Hotspot tool. Huna sababu ya kuanza kuwaza kuhusu gharama ya software hii au kwa wale wengine kuanza kutafuta "njia mbadala" za kuipata, kama ilivyo kwa bidhaa nyingine za Baidu International na hii pia ni "Free Forever, with no hidden or in-app payments", ikimaanisha "Bure milele, bila malipo yoyote yaliyofichwa" (kama wasemavyo wenyewe).

Baidu PC Faster Home Screen

Hauhitaji utaalamu wowote katika kutumia software hii, baada ya kuidownload na kuinstall, ifungue na nenda kwenye sehemu inayoonyesha Wi-Fi Hotspot au unaweza kupitia shortcut ya Wi-Fi Hotspot itayokuwepo kwenye desktop, utahitaji kuweka Wi-Fi name pamoja na password,  Baada ya hapo start Wi-Fi.

Baidu Wi-Fi Hotspot

Features ndani ya Baidu Wi-Fi Hotspot
  • Mwonekano (User Interface) mzuri na rahisi kutumia. 
  • Uwezo wa kudhibiti vifaa vilivyounganishwa (blocking and blacklisting devices).
  • Kutuma na kupokea makabrasha (files) baina ya vifaa vilivyounganishwa.

Link:
Je, umetumia na imekufaa? Usisite kutoa maoni yako, pia mjulishe na jirani pengine na yeye itamfaa.

No comments :

Post a Comment