Dec 30, 2014

Nokia 1100, inaongoza kwa mauzo duniani katika historia ya simu za mkononi.

Nokia tochi, kitochi, simu ya nyongeza, jiwe; Haya ni baadhi ya majina aliyobatizwa Nokia 1100. Simu hii ni maarufu sana na sidhani kama kuna mtu ambaye hajawahi kuiona machoni mwake. Ilikuwa ikipendwa na watumiaji wengi kutokana na uimara iliyokuwa nao, uwezo maradufu wa kukaa na chaji, na unafuu wa bei yake.
Nokia 1100

Siku hizi tumezoea kuona smartphones kila mahali, maisha yetu yamezungukwa na matumizi makubwa ya smartphones katika kuchat, kuperuzi mtandao, kupiga picha, kusoma vitabu na mengine mengi. Kila mara smartphones mpya hutoka. Leo utasikia HTC One M8, mara kesho iPhone 6 Plus, ukiamka kesho kutwa Samsung Galaxy Note 4 iko sokoni. Lakini pamoja na uzinduzi huu wote na hekaheka za mauzo na manunuzi ya smartphones. Hakuna smartphone yoyote iliyowahi kufikia hata nusu ya
mauzo ya Nokia 1100 kwa dunia nzima, simu ambayo inakuwezesha kupiga simu na kutuma sms tu.

Nokia 1100 ilizinduliwa mwaka 2003, tangu kuzinduliwa kwake imefikisha mauzo ya simu takribani simu milioni 250 duniani kote. Pengine rekodi hii itakaa kwa miaka mingi sana mpaka kuja kuvunjwa na mauzo ya smartphones. Samsung Galaxy S4 iliyozinduliwa mwaka 2013 mwezi machi imefikisha mauzo ya kiasi cha milioni 80, hatutegemei kama mauzo haya yataongezeka siku zozote za mbeleni kwa sababu ishatoka katika mstari wa mauzo na kwa sasa Galaxy S5 ndiye aliye sokoni akiwa na mauzo ya kiasi cha smartphones milioni 11, Galaxy S5 nae ana siku chache tu aondoke na kumwachia nafasi Galaxy S6 tunayemtegemea mapema mwakani. Mwingine ni iPhone 5S, alipata mauzo ya kiasi cha smartphones milioni 52 tu, hakuna anayenunua iPhone 5S siku hizi, macho yote mbele kwa iPhone 6 na iPhone 6 Plus

Kinachofanya smartphones kushindwa fikia mauzo kama ya Nokia 1100 ni hiki; suala la "smartphone bora" na "smartphone inayouza sana(best selling)" ni vitu ambavyo mara nyingi haviendi sambamba. Jaribu kutazama hali ya sasa, unapouliza watu wengi wanaozifahamu smartphones kitaalamu, watakuambia HTC One M8 ni smartphone bora kabisa kwa mwaka 2014. Cha ajabu ni kwamba One M8 ina mauzo hafifu mno. Kwa upande mwingine smartphone kama Samsung Galaxy S5 iko juu sana kimauzo lakini haina sifa za kuvutia kama ilivyo kwa HTC One M8, bado kuna vitu vingi Samsung hakuboresha, mfano mdogo:uimara wa S5.

No comments :

Post a Comment